Tunapenda kutaarifu Umma kuwa kuna mtu aliyefungua ukurasa katika mtandao wa kijamii wa ‘Twitter’ kwa kutumia jina la Mhe. Charles Mwijage (MB), Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji na kuweka taarifa kuwa “Kilichotokea kwa Clouds Media ni kitendo cha kinyama na wala si uungwana kabisa tunajenga nchi ya viwanda na si ya kutishana”
Wizara inakanusha taarifa hiyo ya kizushi iliyosambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii yenye lengo la kuleta chuki na kuchafua jina la Waziri pamoja na Wizara yetu kwa ujumla.
Wizara inachukua hatua za kisheria kuwatambua wale wote waliohusika na kutengeneza ukurasa huo bandia.
Tunatoa wito kwa wahusika wote kuacha mara moja kusambaza taarifa hii potofu.

IMETOLEWA NA
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI,
WIZARA YA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI
 22 March, 2017

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...