Na  Bashir  Yakub
Kutelekezwa  ni  pamoja  na  kunyimwa  huduma  za  muhimu  ambazo  kama  mke  alistahili  kupata. Huduma  muhimu  ni  kama  chakula, mavazi  ,  makazi,  matibabu, hela  ya  kujikimu  kwa  matumizi  ya  kawaida  ya  mwanamke,  pamoja  na  kila  hitaji  ambalo  kama  mwanamke  alitakiwa  kulipata.
Ifahamike  kuwa  habari  ya kutelekeza  inawahusu  wote  mke  na  mme  kwa  maana  ya kuwa  mme  anaweza  kumtelekeza  mke  halikadhalika  mke  anaweza  kumtelekeza  mme. Hata  hivyo  makala  yatazungumzia   mme  kumtelekeza  mke  ambapo sura  ya  29 ,  Sheria ya  ndoa  iliyofanyiwa  marekebisho  mwaka  2010  itarejewa.

1.AINA  ZA  KUTELEKEZA.    
( a ) Aina  ya  kwanza ni  kutelekeza  ambako  mume  anaondoka  kabisa  ndani  ya  nyumba  ambayo  alikuwa  akiishi  na  mke  wake kama  wanandoa  na  kwenda  kuishi  kwingine. Haijalishi huko  alikoenda   panajulikana  ni  wapi au  hapajulikani  suala  la  msingi  ni  kwamba  hayupo  katika  makazi  yake  ya  kawaida  ya familia.
Aidha  ikiwa  hayupo  nyumbani  lakini  kwa  sababu  za  msingi  na za  kisheria  huko  sio  kutelekeza.  Sababu  hizo  ni kama  kuwa  jela, kuwa  hospitali, kuwa  amehamishiwa  sehemu  nyingine kwasababu  ya  matibabu   kwa  mfano  wengine  huamishiwa  mikoani, na pia  kuwa  vitani  labda  baadae  mkapoteza  mawasiliano  na  mazingira  mengine  ya  dharula  za  kibinadamu  na  ambayo  siyo  ya  makusudi   hayawezi  kuitwa  kutelekeza.

( b ) Aina  nyngine  ya kutelekeza  ni   hatua  ya  kuwa  mme  na  mke  wanaishi  wote  katika  nyumba   moja  au  chini  ya paa  moja lakini  mume  huyo  hajishughulishi  na  kutoa  matumizi  au  matunzo  kwa  mke  huyo  kwa  namna  yoyote  ile. Hajui  anakula  nini,  hajui  anavaa  nini, hajui  anapata  vipi  matibabu,  kwa ufupi  hajui  lolote  zaidi  ya  kumuona  tu  kama  binadamu  wengine  ambao  anawaona  mitaani  na  hana  uhusiano  nao.
Pia kuishi  chini  ya  paa  moja  lakini  vyumba  tofauti  nako  ni kutelekeza    hata  kama   mke  anapewa  matumizi  yote  yanayostahili. Zaidi,  hata  kulala  chumba  kimoja  lakini  vitanda  tofauti  kwa  muda  mrefu  tena  kwa  makusudi  kwasababu  ya  mgogoro  wowote  nako  ni kutelekeza.  Lakini  pia  kulala  kitanda  kimoja  bila  kushiriki  tendo  la  ndoa kwa  makusudi  kwa muda mrefu   bila  sababu  za  msingi  za  kiafya au  vinginevyo nako  ni  kutelekeza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...