Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya vijana wenye umri wa miaka 17 maarufu kwa jina la Serengeti Boys Leo Jamatano wamefanya mazoezi kujiweka tayari na mchezo wao wa kesho na Timu ya U17 ya Burundi.
Serengeti Boys itakuwa kambini Bukoba hadi Aprili 2, mwaka huu ambako inatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya timu vijana ya Burundi kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba mkoani hapa Kagera. Michezo hiyo itaanza kuchezwa Machi 30, 2017 na kurudiana Aprili mosi, mwaka huu.
Serengeti Boys ambayo inajiandaa na michuano Afrika huko Gabon itarejea Dar es Salaam Aprili 2, mwaka huu ambako imepangwa kucheza na Ghana Aprili 3, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mchezo huo utatanguliwa na hafla ya kuagwa kwa kukabidhiwa bendera.
Serengeti Boys ni timu
ya vijana ambayo imefuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika
zitakazofanyika Gabon kuanzia Mei 14, mwaka huu. Timu hiyo imepangwa
Kundi ‘B’ pamoja na mabingwa watetezi Mali, Niger na Angola. Ina lengo
la kurejea na Kombe la Afrika kwa vijana.
Na ikitokea imekosa
nafasi hiyo angalau ikafika nusu fainali ambako kwa mafanikio hayo
itakuwa tayari ina tiketi mkononi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia
huko India, Novemba, mwaka huu.
Serengeti Boys watacheza mchezo wao wa kwanza leo jioni katika uwanja wa Kaitaba na tayari timu ya U17 ya Burundi ambayo imeingia Bukoba hii jana jioni kwenye muda wa saa 11, ila hawakuweza kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Kaitaba kutokana na uchovu wa safari yao na hivyo kutoa taarifa kuwa watafanya asubuhi saa moja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...