Jovina Bujulu- MAELEZO

Serikali imewataka wachapishaji wote nchini waliojiandikisha kwa Msajili wa Makampuni ( BRELA) na Mamlaka ya Mapato (TRA), kufika katika ofisi ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali ili wajiorodheshe na watambuliwe na Serikali na wananchi kabla ya Machi 30 mwaka huu.

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali ndugu Cassian Chibogoyo alipokuwa akizungumzia kuwepo kwa wimbi kubwa la wachapishaji hewa nchini.

Chibogoyo amesema kuwa hatua hiyo inafuatia uwepo wa utitiri wa wachapishaji ambao hawatambuliki na Serikali, kwa sababu baada ya kujiandikisha kwa mamlaka husika kama kampuni, utawakuta wana mitambo ya uchapishaji ambayo mara nyingi wanaitumia kuchapisha nyaraka bandia za Serikali bila kuwa na kibali kutoka katika mamlaka yenye dhamana ya uchapishaji.

“Kwa sasa tumeanzisha utaratibu maalum wa kuwatambua wachapishaji ambapo wanatakiwa kujiorodhesha kwa Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, hii ni kutokana na kuwepo kwa uchapaji holela na bandia wa nyaraka za Serikali” alisema Chibogoyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. hivi Fair Competition Commission iko wapi jamani, yaani wewe mpiga chapa mkuu kazi zoote za Serikali unapewa wewe bila tenda wala nini halafu bado private sector waje kujiandikisha kwako kwani Brela na TRA wanafanya shughuli gani?? Kila siku kila mtu anaibuka na lake hivi private sector watabaki kweli kwa hali hii?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...