Wananchi Wilayani Handeni wametakiwa kutilia mkazo suala la kuwapeleka watoto kupata chanjo mara zinapotangazwa ili kuendana na msemo wa kinga ni bora kuliko tiba.

Rai hiyo ilitolewa wakati wa uzinduzi wa wiki ya chanjo ya polio wenye kauli mbiu ya “jamii iliyochanjwa ni jamii yenye afya” uliofanyika katika Zahanati ya Mumbwi iliyopo Katika Kijiji cha Mumbwi kata ya Komkonga.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe mbaye pia alikuwa mgeni rasmi alieleza kuwa Serikali inajitahidi kutoa chanjo bure hivyo wananchi pia wanao wajibu wa kuhakikisha wanapeleka watoto wao kupata chanjo hizo kwaajili ya ustawi wa afya za watoto.

“Halmashauri ya Wilaya ya Handeni inazo chanjo za kutosha, chanjo mkoba na chanjo tembezi zitafika kwenye maeneo ambayo bado hayana zahanati ili kuhakikisha watoto wote Wilayani Handeni wanachanjwa” alisema Mh. Gondwe.

Aidha , aliwataka Maafisa Tarafa, Watendaji Kata na Vijiji kuweka agenda ya usafi na mazingira, afya na bima kuwa ndelevu katika viko vyao vya Vijiji.Akizungumzia suala la malaria kwenye siku ya maadhimisho ya siku ya malaria duniani Mh. Gondwe alisema kila mwanachi anawajibu wa kutunza mazingira na kutokomeza mazalia ya mbu ili kutokomeza kabisa ugonjwa huo.

“Chanjo zinatolewa bure,vipimo vya malaria vinatolewa bure na baadhi ya dawa za malaria bure lakini ni vyema kila mwananchi kuwa na bima ya afya ili kuepuka gharama za matibabu na kuhakikisha kuwa suala la afya haliwi tatizo kwenye Wilaya ya Handeni”alisema Mh.Gondwe.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh Godwin Gondwe akizindua zoezi la utoaji chanjo Kwa watoto kwa kumpatia mtoto matone ya chanjo ya polio.

Mh Godwin Gondwe akiwa kwenye picha ya pamoja na walezi wahakikishe watoto aliowapatia chanjo huku akiwa amembeba mtoto ikramu mbarouk Mara baada ya kutoa chanjo Kwa watoto wao.
Viongozi mbalalimbali kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Handeni wakiongozwa na mkuu wa Wilaya Mh Godwin Gondwe wakiwa wamebeba watoto waliopatiwa chanjo
Baadhi ya wazazi waliojitokeza kuleta watoto wao kupatiwa chanjo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...