Akiongea jijini Dar es Salaam mapema leo, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Rosalynn Mworia amesema “Vodacom Tanzania PLC inatarajia kupokea maombi mengi ya kununua hisa katika kipindi cha wiki hii.
Pia kutokana na ushauri kutoka Serikali ya Tanzania na  makundi mbalimbali muhimu ya kijamii yanayohitaji kuwekeza wakiwemo Wabunge, makundi ya watumishi wa kada mbalimbali wa serikali na maofisa wa vyama  vya Ushirika kutoka sehemu mbalimbali za nchi, tumewasilisha maombi na kupata idhini kutoka Mamlaka ya Soko la mitaji na dhamana(CMSA) kuongeza muda wa zoezi la kuuza hisa kwa kipindi cha wiki tatu hadi kufikia Alhamisi ya tarehe 11 Mei, 2017. 
Mkurugenzi huyo alisema kuongezeka kwa muda wa mwisho wa kununua hisa utawezesha wanaohitaji kununua hisa  kwa makundi binafsi na taasisi zilizoomba muda uongezwe kushiriki kikamilifu katika mchakato huu. Tunatoa shukrani za dhati kwa watanzania ambao wamejitokeza kuwekeza kupitia kununua hisa na tunawakaribisha ambao bado hawajanunua hisa kuchangamkia fursa hii katika kipindi cha muda mfupi wa nyongeza.

Mgawanyo na mchanganuo wa umiliki wa hisa inapendekezwa utafanyika kuanzia Mei 19, 2017 na kuendelea kabla ya kumaliza mchakato wa mwisho wa kujisajili katika Soko la Hisa la Dar es Salaam katika tarehe iliyopangwa ya Juni 6, 2017.”
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Rosalynn Mworia akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati alipokuwa akitangaza kwa kampuni yao kuongeza muda wa zoezi la kuuza hisa kwa kipindi cha wiki tatu hadi kufikia Alhamisi ya tarehe 11, Mei 2017.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria kwenye mkutano huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...