MKUU wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu amekabidhi nyumba 12 za walimu wa shule ya Sekondari ya Minyughe na Wembere huku akiwaasa walimu kumpa nguvu rais dokta John Pombe Magufuli kwa kuzitunza ili zidumu na kama sehemu ya kuunga mkono jitihada zake za kuwatumikia wananchi.

Nyumba hizo zimejengwa kupitia mpango wa serikali wa kuendeleza shule za sekondari(SEDEP II) uliogharimu shilingi milioni 300 hadi kukamilika kwake.

Akikabidhi nyumba hizo Mtaruru alimshukuru rais dokta Magufuli kwa dhamira yake njema ya kuwahudumia watanzania ili wawe na maisha mazuri ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)ya mwaka 2015 iliyoeleza uboreshaji wa elimu ikiwemo mazingira ya kufundishia.

“Tukio hili ni ushahidi tosha wa namna ilani ya CCM inavyotekelezwa kwa vitendo,nyumba hizi zitasaidia kuwasogeza walimu karibu na mazingira ya shule na hivyo kuwapa utulivu wa kuandaa masomo yao hali itakayosaidia kuongezeka kwa ufaulu kama moja ya maazimio ya mkutano wa wadau wa elimu uliofanyika mwezi disemba mwaka jana lakini pia itaondoa kero ya walimu kuhangaika mitaani,”alisema Mtaturu.

Aliwataka walimu kuendelea kuiamini serikali wakati inaendelea kushughulikia kero,stahili na madai yao na kuwapongeza kwa ushirikiano walioutoa kwa wakandarasi uliorahisisha mradi huo kukamilika kwa wakati.

Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akizindua rasmi nyumba zilizojengwa kwa ajili ya walimu wa shule za sekondari za Minyughe na Wembere baadhi ya aliofuatana nao ni mwenyekiti wa CCM wilaya Hassan Tati mwenye shati la kijani na Diwani wa kata ya Minyughe Saddack.  Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akikagua nyumba 12 za walimu baada ya kuzizindua.

Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akiwa kwenye picha ya pamoja na   viongozi wa wilaya,kata na walimu waliokabidhiwa nyumba kwenye shule ya sekondari ya Minyughe. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...