Wanaume wa
jamii ya Kihadzabe wanaoishi kwenye pori la Myembe lililopo ndani ya Mamlaka ya
Hifadhi ya Ngogorongoro upande wa Ziwa Eyasi wakipanda mti wa mbuyu kurina
asali. Kabila la Wahazabe ni moja ya jamii za wawindaji na wakusanyaji wanaopatikana
Tanzania ambao chakula chao kikuu ni nyama, matunda, mizizi na asali.
HONGERA
KIONGOZI: Bwana Julius Indaya (katikakati) kiongozi wa jamii ya Wahadzabe
wanaoishi upande wa Ziwa Eyasi akivishwa ngozi ya nyani na wenzake mara baada
ya kufanikiwa kumkamata mnyama huyo kwa ajili ya kitoweo cha siku. Kwa
utamaduni wa kabila la Wahadzabe kuvishwa ngozi ya mnyama ni ishara ya pongezi
kwa mtu aliyefanikisha kukamatwa mnyama wakati wa uwindaji. Picha na Abuu Kimario - Bodi ya Filamu Tanzania
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...