Ofisa wa Benki ya NMB Tawi la Temeke, Latifa Ayoub Dadah (kushoto)
akimkabidhi mpira wa miguu mmoja wa viongozi wa michezo wa Shule ya
Msingi Wailes kwa ajili ya shule hiyo. Mpira huo umetolewa na Benki ya
NMB kama zawadi kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Wailes mara baada ya
elimu ya masuala ya fedha na akiba iliyotolewa na benki hiyo. Wa kwanza
kusho to ni Mwalimu wa Taaluma wa Shule ya Msingi Wailes, Zabibu Wasia
akishuhudia.
Ofisa wa Benki ya NMB Tawi la Temeke, Latifa Ayoub Dadah (kushoto)
akitoa elimu ya masuala ya kifedha na akiba kwa wazazi na wanafunzi
walioshiriki mafunzo ya programu ya wajibu ya NMB katika Shule ya Msingi
Wailes ya jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wachezaji vijana (kulia) wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Azam
kupitia kituo chao cha michezo akimkabidhi mpira wa pete mmoja wa
viongozi wa michezo wa Shule ya Msingi Wailes kwa ajili ya shule hiyo.
Mpira huo umetolewa na Benki ya NMB kama zawadi kwa wanafunzi wa Shule
ya Msingi Wailes mara baada ya elimu ya masuala ya fedha na akiba
iliyotolewa na benki hiyo.
Mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Wailes akijibu swali kwenye
mafunzo ya programu ya wajibu iliyotolewa na Benki ya NMB shuleni hapo.
BENKI
ya NMB imetoa elimu ya masuala ya kibenki na umuhimu wa kujijengea
utamaduni wa uwekaji akiba kwa wanafunzi na baadhi ya wazazi wa Shule ya
Msingi Wailes iliyopo Temeke jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na wanafunzi wa Shule ya Msingi Wailes walioshiriki mafunzo hayo ya
kifedha, Ofisa wa Benki ya NMB Tawi la Temeke, Latifa Ayoub Dadah
alisema NMB inaendelea kutoa elimu ya masuala ya kifedha ikiwa ni pamoja
na kujifunza mbinu za kuweka akiba kwa ajili ya maisha ya baadae.
Alisema
elimu hiyo inatolewa kupitia Programu maalum ya Wajibu ambayo hutoa
fursa kwa watoto, vijana na wazazi kujifunza masuala ya kifedha ili
kumjengea mtoto utamaduni wa kujiwekea akiba, elimu ambayo watoto wengi
hawapati fursa ya kujifunza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...