Na Sixmund J. Begashe 

Serikali ya Uswisi imeamua kuinga mkoni Serikali ya Jamhuuri ya Muungano wa Tanzania katika mapambano dhidi ya Rushwa kwa kuziwezesha program tano kiasi cha Dola za kimarekani 100,000 ambazo ni takribani Shilingi milioni 220/= ili ziweze kutoa elimu kwa njia za burudani ya mapambano dhidi rushwa nchini.

Akizungumza kabla ya kusaini mikataba ya program hizo, Balozi wa Uswisi hapa nchini Mh ARTHUR MATTLI amesema kuwa Tanzania kwa sasa inafanya vizuri zaidi katika mapambano dhidi ya rushwa ukilinganisha na nchi nyingi barani Afrika hivyo wameona ni vyema ikaungwa mkono katika mapambano haya.

Balozi Mattli ameongeza kuwa hadi sasa takwimu zinaonesha kuwa katika nchi za Afrika mashariki Tanzania inaongoza katika mafanikio yanayotokana na mapambano dhiri ya rushwa hivyo serikali yake imeona nivyema ikaunga mkono jitihada hizi kwa kuziwezeshwa program zitakazo toa elimu juu ya madhara ya rushwa kwa kupitia sanaa ili watanzania waweze kuipokea nakuielewa elimu hiyo kwa urahisi zaidi.

Akizungumza baada ya kusaini makubaliano ya kupokea fedha za kuendesha programa ya Museum Art Explosion, kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Bw Saimon Maliti pamoja na kuishukuru Serikali ya Uswizi kwa kutambua jitihada za Makumbusho ya Taifa katika kuelimisha jamii juu ya mambo yanayo wahusu, amemwakikishia Balozi huyo kuwa fedha walizo pata zitatumika kama zilivyo kusudiwa na si vinginevyo.

Nae Mkurugenzi wa Elimu kwa Jamii wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) Bw EKWABI MUJUNGU ameishukuru Serikali ya Uswizi kwa kuiunga mkono Serikali ya Tanzania katika mapambano dhidi ya Rushwa na kuahidi kufanya kazi kwa karibu na Taasisi zilizo wezeshwa na Ubalozi huo ili kuhakikisha malengo yaliyokusudia ya kupambana na rushwa yanafanikiwa.

Taasisi zilizo wezeshwa ni pamoja Makumbusho ya Taifa kupitia Program ya MUSEUM ART EXPLOSION AGAINST CORRUPTION, Tanzania House of Talent (THT), Kijiji Studii Tanzania, Goba Africa LTD na Art in Tanzania.
 Katikati ni Balozi wa Uswisi nchini mh ARTHUR MATTLI akizungumza na viongozi wa program zilizowezeshwa na Ubalozi huo katika mapambano dhidi ya rushwa nchini.


 Balozi wa Uswisi nchini mh ARTHUR MATTLI akizungumza na viongozi wa program zilizowezeshwa na Ubalozi huo katika mapambano dhidi ya rushwa nchini.

 Katikati ni Balozi wa Uswisi nchini Mh ARTHUR MATTLI  na kulia ni Mkurugenzi wa Mkumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw Achiles Bufure wakishuhudia Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Bw Saimon Maliti akitia sahii makubaliano ya fedha za kuendeshea program ya Museum Art Explosion kwa mapambano dhidi ya rushwa



Kulia ni Mkurugenzi wa Elimuli kwa Jamii wa TAKUKURU Bw Ekwabi Mujungu na Muanzilishi wa THT Bw Ruge Mutahaba wakimsikiliza kwa Makini Balozi wa Uswisi nchini Mh  ARTHUR MATTLI(ayupo pichani)  . 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...