Ndugu Catherine Nyakao Ruge
KUHUSU
UTEUZI WA CATHERINE NYAKAO RUGE KUWA MBUNGE WA VITI MAALUM KUPITIA
CHAMA
CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO
Kwa
mujibu wa Ibara ya 78(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ya mwaka 1977 ikisomwa pamoja na Kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Taifa
ya Uchaguzi, Sura ya 343, Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kikao chake
cha tarehe 04 Mei, 2017 imemteua Ndugu Catherine Nyakao Ruge kuwa Mbunge
wa Viti Maalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kujaza nafasi iliyoachwa
wazi na Mhe. Dkt. Elly Marco Macha.
Tume
ya Taifa ya Uchaguzi imemteua Ndugu Catherine Nyakao Ruge baada ya
kupokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ambaye kwa mujibu wa Kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya
Uchaguzi, Sura ya 343, alitaarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwepo
nafasi wazi ya Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na
Maendeleo, baada ya aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Dkt. Elly
Marko Macha kufariki dunia na hivyo kuwepo nafasi wazi.
Imetolewa leo tarehe 04 Mei, 2017 na:-
Kailima, R.K
MKURUGENZI WA UCHAGUZI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...