Serikali Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa imetangaza kuwachukulia hatua
kali wazazi
na viongozi wa serikali za vijiji
na vitongiji aambao watasaidia kutorosha
wanaume wanaowapa mimba wanafunzi katika
maeneo yao .
Agizo
hilo limetolewa na mkuu wa wilaya ya Kilolo
Mhe. Asia Abdallah wakati wa ziara yake
ya kutembelea shule za msingi
na sekondari katika kata ya Ilula
wilayani humo leo. Amesema kuwa imekuwa ni
kawaida ya wazazi kwa kushirikiana na baadhi
ya viongozi wa serikali za vijiji na
vitongoji kupokea pesa kutoka
kwa wanaume wanaowapa mimba wanafunzi kisha kuwatorosha.
Mkuu huyo
wa wilaya alisema kuanzia sasa mzazi ama
kiongozi atakayebainika kushiriki kupokea pesa
au kumtorosha mtuhumiwa wa
mimba kwa wanafunzi atakamatwa na kufikishwa
mahakamani pasipo huruma.
Hivyo alitaka kila mzazi na kila
mwananchi kuhakikisha wanakuwa sehemu
ya ulinzi wa watoto hao wa kike na
pale inapobainika kuwa mwanaume ana mahusiano na wanafunzi
kuchukua hatua haraka ya kumfikisha
kwenye vyombo vya sheria .Aidha alisema
kazi ya viongozi
wa serikali za vitongoji na vijiji ni
kuwalinda watoto hao wa kike dhidi
ya wabakaji kwa kuwakamata
na kuwafikisha polisi huku wazazi hawana sababu
ya kukaa chini ya watuhumiwa hao wa mimba kwa
lengo la kumalizana nje ya vyombo vya sheria .Mkuu wa wilaya ya Kilolo mkoa wa Iringa Mhe. Asia Abdallah akizungumza na wanafunzi wa kidato cha kwanza shule ya sekondari Ilula leo |
Walimu wa shule ya sekondari Ilula na wanahabari wakiwa katika kikao cha mkuu wa wilaya ya Kilolo leo |
Mkuu wa wilaya ya Kilolo mkoa wa Iringa Mhe. Asia Abdallah akifurahia jambo na wanafunzi wa kidato cha kwanza shule ya sekondari Ilula leo
|
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...