Taarifa tulizopokea hivi
punde zinaeleza kwamba mmoja wa wanamuziki nguli nchini, Shaaban Dede, amelazwa
katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam kupatiwa matibabu.
Kwa mujibu wa msemaji wa
Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania (CHAMUDATA), Dede amelazwa wodi ya Mwaisela
Namba 5 kitanda namba moj, ambapo wadau wa muziki wameombwa kwenda kumjulia hali huku wakimuombea
apate nafuu haraka. Taarifa hiyo haikumesema Dede anasumbuliwa na matatizo gani.
Shaaban Dede ni
mwanamuziki mkongwe ambaye anajulikana kwa sauti yake tamu pamoja na tungo
zilizosheheni kila aina ya ladha.
Kwa ufupi Dede alizaliwa
Mkoa wa Kagera mwaka 1954 ambako alianza kupenda muzikiakiwa bado mdogo kabisa
na bendi yake ya kwanza kujiunga nayo ilikuwa ni ya TANU ambayo makazi yake
yalikuwa Biharamulo, mjini Bukoba.
“Mwaka 1974 alijiunga na Bendi ya Polisi na mwaka 1975 akajiunga
na Tabora Jazz ambako alikaa kidogo kabla ya kuhamia 1976 nilihamia Dodoma
Internationl Band mwaka 1976 ambako alidumu
kwa miaka mitatu.
Mnamo mwaka 1979 alijiunga na bendi ya Msondo wakati huo
ikijulikana kama JUWATA JAZZ ambako alidumu
mpaka mwaka 1982 alipoahamia Mlimani
Park Orchestra wana SIKINDE ambako alikaa kwa mwaka mmoja kabla ya kujiunga na Bendi
ya Bima a.k.a BIMA LEE. Mnamo mwaka 1987
Deded alirudi tena Msondo ambako alikaa kidogo na baadaye akahamia tena Sikinde. Hata
hivyo mwaka 20111 akarejea tena Msondo ambako yuko hadi hii leo.
Globu ya Jamii inamtakia
apate nafuu haraka gwiji wa muziki Shaaban Dede. Tutaendelea kuwaletea taarifa
za maendeleo yake kila zitapopatikana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...