Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani Mhe. Filberto H. Sanga akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi ya sikukuu ya Idd El Fitri  kwa niaba ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Malaika Kids kilichopo Mkuranga leo.Kutoka kushoto ni Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Utawala na Rasilimali Watu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abdullrahaman Mdimu na Afisa Tarafa ya Mkuranga Clement Muya.
 Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Utawala na Rasilimali Watu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Bw. Abdullrahaman Mdimu akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi ya sikukuu ya Idd El Fitri  kwa niaba ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Malaika Kids kilichopo Mkuranga leo. Mhe. Rais ametoa zawadi ya mchele kilo 150, mbuzi pamoja na mafuta ya kupikia lita ndoo mbili.Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria kutoka Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Mohamed Magati, Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto H.Sanga na Afisa Tarafa ya Mkuranga Clement Muya.
 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani, Filberto H. Sanga akimkabidhi zawadi ya shilingi elfu kumi mmoja wa watoto wanaolelea katika Kituo cha Malaika Kids wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi ya sikukuu ya Idd El Fitri  kwa niaba ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kilichopo Mkuranga leo. Mtoto huyo amepewa zawadi hiyo kufuatia kujibu swali la Mkuu wa Wilaya huyo lililotaka kufahamu watoto hao wanataka kuwa wakina nani katika maisha yao ambapo mtoto huyo alisema anataka kuwa Rais. Anayeshuhudia ni Meneja maarufu kama Baba Mlezi wa Kituo hicho James Kallinga.
 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani, Filberto H. Sanga akiwakabidhi watoto wa Kituo cha Malaika Kids kilichopo Mkuranga zawadi ya sikukuu ya Idd El Fitri  kwa niaba ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo. Mhe. Rais ametoa zawadi ya mchele kilo 150, mbuzi pamoja na mafuta ya kupikia lita ndoo mbili.
 Mkuu wa Kituo cha Kulelea watoto cha Malaika Kids kilichopo Mkuranga, Pwani James Kallinga akitoa neon la shukrani kwa niaba ya watoto wa kituo hiyo mara baada ya kukabidhiwa zawadi za Idd El Fitri zilizotolewa na na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya kituo hicho leo.  Kutoka kulia ni Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Utawala na Rasilimali Watu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Bw. Abdullrahaman Mdimu, Afisa Tarafa ya Mkuranga Clement Muya na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani, Filberto H. Sanga. Picha zote na Frank Shija – MAELEZO, Mkuranga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...