Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
CHAMA cha Kutetea Abiria (Chakua) kimewaomba abiria wanaongia katika kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani  cha ubungo kutoa sh. 200 kwa ajili ya kusaidia chama hicho.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam,Mratibu wa chama hicho, Monday Likwepa amesema kuwa chama kimekuwa na msaada mkubwa kwa abiria hivyo chama kinahitaji kujiendesha na wadau ni abiria kuchangia kiwango hicho.

Amesema kuwa kiwango hicho  walichopanga kitasaidia kuendesha shughuli za ofisi pamoja na kuweza kushughulika na matatizo ya abiria pale wanapopata usafiri.

Likwepa amesema kuwa abiria wamekuwa wakipata matatizo na kukimbilia chakua hivyo kwa utaratibu wa kuchangia wanawajibu kudai haki zao pale wanapopata usumbufu.

Aidha amesema kuwa wataendelea kutoa elimu zaidi juu ya uchangiaji wa fedha hiyo katika kituo cha ubungo ili wananchi wajue  uchangiaji huo na pamoja na faida zake.
Mratibu Mtendaji wa Chama  Cha Kutetea Abiria(Chakua), Monday Likwepa akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuchangia abiria  wanaosafiri katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo sh.200 kwa ajili kuendesha shughuli za utetezi wa abiria pale anapopatwa na tatizo. Kushoto ni Mratibu mtendaji wa Chakua, Elias Kalinga na kulia ni Mwenyekit wa wa Taifa wa Chakua, Hassan Mchanjawa.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...