Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo (wa pili kulia) alifanya ziara ya kukagua maendeleo ya Awamu ya tatu ya kazi za upanuzi wa mtambo na mfumo wa CHALIWASA ambao chanzo chake ni mto Wami. 

Katika ziara hiyo Mhandisi Kalobelo alitembelea kazi mbalimbali za mradi ikiwemo shughuli za upanuzi wa chanzo, ujenzi wa matenki, ulazaji mabomba pamoja na majengo ya ofisi. 

Mradi huu unaojengwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji  kupitia na DAWASA unahusisha ujenzi wa Matenki 19, ulazajiwa mabomba ya ukubwa mbalimbali kwa kilometa 1, 203, ujenzi wa vizimba 351 vya kuchota maji pamoja na upanuzi wa mtambo wa kusafisha maji wa CHALINZE. Lengo ni kuongeza uzalishaji kufikia mita za ujazo 900 kwa siku kutoka mita za ujazo 500.

Kazi hii itakapokamilika, wakazi waliopo maeneo ya Manga hadi Tengwe katika Mkoa wa Tanga; mji na vitongoji  vya wa Chalinze na baadhi ya maeneo ya Bagamoyo na Kibaha katika mkoa wa Pwani watafaidika.
 Mradi pia utanufaisha baadhi ya maeneo ha Mkoa wa Morogoro ikiwa ni pamoja na  maeneo ya Kizuka A na B, Ngerengere, Kinoko A and B, Tukamisasa, Lulenge, Visakazi hadi Bwawani  pamoja na Sangasanga A na B, Hadi utakapokamilika, mradi utagharimu dola za Marakani 41,362,023.43 ambazo ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya India kupitia Benki ya EXIM ya India. Mradi utakamilika mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...