Shirika la Rafiki Social Development Organization – SDO la mkoani Shinyanga leo Jumanne Agosti 15,2017 limezindua Mradi wa ulinzi wa mtoto, haki za watoto na utawala utakaotekelezwa kwa kipindi cha miaka miwili katika kata 30 kwenye halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga,Shinyanga Vijijini na Kahama Mji.

Uzinduzi wa mradi huo umefanyika katika ukumbi wa Ibanza Hotel Mjini Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro. 

Akizungumza wakati wa kuzindua mradi huo,Matiro alilitaka shirika hil0 kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa jadi la sungusungu,serikali,viongozi wa dini,kimila na wananchi. “Niwapongeze sana Rafiki SDO kwa kupata mradi huu muhimu kwa ajili ya ulinzi wa watoto,sote tunatambua kuwa vitendo vya ukatili wa watoto vimekithiri katika jamii,serikali pekee haiwezi kumaliza vitendo hivi,lazima tushirikiane ili watoto wetu wawe salama”,alisema Matiro. 

“Natamani kusikia mashirika yanajitokeza kuanzisha miradi kwa ajili ya kupambana na vitendo vya ulawiti wanavyofanyiwa watoto wetu,taarifa nilizo nazo ni kwamba baadhi ya watoto wa kiume waliopo katika shule za msingi wanafanyiwa mchezo mbaya wa kulawitiwa,tena wanafanyiwa na watu wazima,hili halikubaliki lazima tushirikiane kumaliza tatizo hili”,aliongeza Matiro. 

“Naomba mashirika yanayojihusisha na masuala ya watoto yajitokeze na kuanzisha miradi ya kusaidia watoto wanaolawitiwa,tunapaswa kuwalinda watoto hawa,kinachotakiwa ni ushirikiano japo changamoto katika kesi za ukatili ni wazazi na walezi kumaliza kesi kienyeji”,alisema Matiro. 
Wa kwanza kushoto ni Afisa Ustawi wa jamii Manispaa ya Shinyanga John Nhabi,akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro,Mkurugenzi wa Shirika la RAFIKI SDO,Gelard Ng’ong’a na Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima (wa kwanza kulia) wakiwa katika ukumbi wa Ibanza Hotel Mjini Shinyanga wakati wa uzinduzi wa mradi wa ulinzi wa mtoto, haki za watoto na utawala .
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa ulinzi wa mtoto, haki za watoto na utawala utakaotekelezwa na Shirika la Rafiki SDO kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la kuhudumia watoto “Save The Children International” kwa hisani ya shirika la Maendeleo la nchini Sweeden – SIDA. 
Wadau wakiwa ukumbini wakati wa uzinduzi wa mradi huo. 
Wadau mbalimbali wa masuala ya watoto kutoka kata 30 za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini,Manispaa ya Shinyanga na Kahama Mji ambako mradi huo utatakelezwa wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...