Na
Mathias Canal, Kaskazini Pemba
Umoja wa Vijana wa
Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umesema kuwa Jukumu la kuleta maendeleo ya kiuchumi
katika jamii ni la kila mwananchi sio jukumu la serikali pekee.
UVCCM imesema kuwa
jukumu la serikali ni kuwaonyesha wananchi fursa zilipo na namna bora ya
kuzichanganua ikiwa ni pamoja na kufanya kazi ili kukuza uchumi wa mtu mmoja
mmoja na jamii kwa ujumla wake sambamba na kuwezeshwa kupata mikopo katika
vikundi vyao vya ujasiriamali.
Kauli hiyo imetolewa na
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka
Hamdu Shaka leo Agosti 16, 2017 alipokuwa akizungumza na wanachama wa Chama Cha
Mapinduzi na jumuiya zake katika mkutano wa ndani uliofanyika katika ukumbi wa
Jamhuri Wilayani Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Alisema kuwa vijana ni
nguvu kazi ya Taifa hivyo wanapaswa kutumia nguvu zao vizuri kwa kufanya kazi
ili kujikwamua kiuchumi katika familia zao badala ya kukaa maskani kujadili
mambo yasiyokuwa na tija kwao.
Aliongeza kuwa UVCCM
inaunga mkono vijana kukaa maskani kwa maslahi mapana ya mjadala wa Maendeleo
yatakayopelekea kujikwamua kiuchumi ikiwa ni pamoja na kujiunga katika vikundi
mbalimbali vya ujasiriamali.
Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka akizungumza jambo pamoja na mwl,Ally khatibu Hassan Mkuu wa shule ya msingi Michekweni wakati akikagua jengo la Ujenzi wa maktaba pamoja na madarasa ya Shule ya Msingi Micheweni. wakati wa ziara ya kikazi visiwani pemba.
Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka akiwa Shumba mjini akikagua sehemu itakayo jengwa jeti
Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka akigagua ujenzi wa ofisi ya ccm tawi la njuguni inayojengwa na mwakilishi Jimbo
Afisa mipango wa halmashauri ya konde (pili kushoto)akitolea ufafanuzi juu ya ujenzi wa soko la mboga mboga la samaki pamoja na mbogamboga kwa Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka akiwa katika ziara ya kikazi visiwani pemba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...