Na David John -Mwanza.

KATIBU wa Chama cha Michezo wilaya ya Nyamagana Daddy Gilbert amewataka wanasiasa kuacha tabia ya kuitumia michezo pindi wanapotafuta nafasi za uongozi na wakishapata hawana habari.
Amesema wanasiasa wengi wamekuwa wakitumia michezo kama tiketi yao ya kutaka uongozi na wakifanikiwa hawanahabari na michezo jambo ambalo halipendezi.

Kiongozi huyo wa michezo ametoa dukuduku lake hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo walifika katika ofisi za chama cha soka wilaya hiyo kutaka kujua namna walivyojipanga kuendeleza michezo.
Daddy amesema anakerwa na baadhi ya wanasiasa ambao wanatumia michezo kupata uongozi na pindi wanapofanikiwa hawajari tena.

"unajuwa kama wenzetu wanasiasa wangekuwa wanatuunga mkono naamini hata kwa hapa Mwamza tungefika mbali ,lakini bahati mbaya wakishapata wanachokipata hawana muda tena na sisi". amesema Daddy.

Pia bosi huyo wa chama wilaya ametoa rai kwa wananchi wa mkoa wa mwanza kujitokeza katika viwanja vya michezo hususani uwanja wa Nyamagana ambapo ligi ya Willya kutafuta timu zitakazo cheza ligi ngazi ya mkoa.

"kama mmavyoona hapa kuna ligi ya Wilaya ambayo imeshirikisha timu 25 inaendelea lakini mwamko wa mashabiki Kama mnavyoona."amesema Daddy.
Mwenyekiti wa Chama cha Soka wilaya ya  Nyamagana Daddy Girbat( kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mwandishi wa Habari hizi David John leo mara baada ya kumtembelea ofisini kwake ulipo uwanja wa michezo wa Nyamagana. Mkoani mwanza

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...