WATU zaidi ya 800 wamejitokeza kupima afya ya magonjwa yasiyoambukiza katika Viwanja   vya Tandale Wilayani Rungwe ambapo Tamasha la Ngoma za asili linalojulikana kwa Tulia Traditional Dances Festival 2017 lililoandaliwa na Naibu Spika Dk. Tulia Ackson linafanyika.

Akizungumzia hili, Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya (NHIF) Afya Ofisi ya Mbeya, Isaya Shekifu alisema pamoja na kuenzi utamaduni wamegundua kuwa watu wengi hawana utamaduni wa kufika Hospitalini kwa ajili ya kupima afya zao kwa ajili ya kupata ushari na tiba ya magonjwa yasioambukiza ambayo ni tishio kubwa kwa afya za wengi.

Alisema Mfuko uliona utumie fursa ya mashindano ya Ngoma za asili kwa ajili ya kuwafikia watu wengi ili waweze kupima na kupatiwa ushauri na elimu juu ya magonjwa mbalimbali ikiwemo Sukari, shinikizo la damu na unene ulipitiliza.
Alisema wananchi wengi wamehamasika na kujitokeza kupima na kupata ushauri kutoka kwa madaktari waliopo katika viwanja hivyo.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa NHIF, Bi. Anjela Mziray alisema pamoja na kupima afya katika mashindano hayo ambayo huduma hutolewa bure pia Mfuko unahamasisha na kusajili watoto wa chini ya umri wa miaka  18 na huduma ya bima ya afya. Huduma hii inajulikana kwa jina la Toto Afya Kadi.

Alisema zoezi la kuandikisha linafanyika kiwanjani hapo na kadi kutolewa ndani ya muda mfupi kwa mchango wa shilingi 50,400 tu kwa mwaka kwa kila mtoto ambapo mtoto atapata matibabu kwa mwaka mzima katika Zahanati,Vituo vya Afya na Hospitali zote zilizosajiliwa na Mfuko huo Tanzania nzima.
Aidha alitoa wito kwa wazazi na Walimu kuchangamkia fursa hiyo kwa kuwa shule nyingi za bweni zinakabiliwa na changamoto ya matibabu kwa wanafunzi hivyo kila mwanafunzi akiwa na Bima ya afya itamrahishia kupata matibabu kwa uhakika akiwa shuleni na hata wakati wa likizo.

Nao baadhi ya Wateja waliojitokeza kupata huduma katika Banda la Bima ya Afya, Staford Mwakasapa na Mwalimu Elizabeth Sekile ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Wilaya ya Rungwe wamepongeza utaratibu huo na kuongeza kuwa huduma kama hiyo inapaswa kusambazwa katika kila mikusanyiko.
Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa NHIF, Anjela Mziray akizungumza na waandishi wa habari.

Walisema watu wengi hawana utaratibu wa kwenda Hospitali kupima afya zao hadi waugue hivyo huduma ya kutembelea na kutoa elimu napaswa kusogezwa na kuwa endelevu ili kuokoa afya za wananchi.

Hata hivyo walitoa wito kwa Serikali kuhakikisha wateja wenye kadi za matibabu ya Bima ya Afya wanapata huduma zote zinazostahili ikiwemo upatikanaji wa Vifaa tiba pamoja na madawa kwa wagonjwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...