NA HAMZA TEMBA - WMU-DODOMA
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Ngailonga Hasunga
leo tarehe 18 Oktoba, 2017 ameripoti rasmi Makao Makuu ya Wizara hiyo yaliyopo
Mtaa wa Kilimani, Makao Makuu ya Nchi, Mjini Dodoma.
Mhe. Hasunga amepokelewa na
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Gaudence Milanzi na kuingia ofisini
kwake kwa mara ya kwanza ambapo amesaini kitabu cha wageni na baadaye akapata
fursa ya kuzungumza na watumishi wa Wizara hiyo waliopo Dodoma.
Akizungumza na watumishi
hao baada ya kutambulishwa, Mhe. Hasunga aliwaomba ushirikiano katika
kufanikisha majukumu ya Wizara ambayo ni kuhifadhi na kusimamia matumizi
endelevu ya maliasili na malikale, na kuendeleza ufugaji nyuki na utalii.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kushoto)
akikaribishwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Gaudence Milanzi (katikati)
alipowasili kwa mara ya kwanza katika ofisi ya makao makuu ya wizara hiyo zilizopo
mtaa wa Kilimani mjini Dodoma leo. Kulia anaeshuhudia ni Mkurugenzi wa Idara ya
Utawala na Rasilimali Watu, Tutubi Mangazeni.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence
Milanzi (kushoto) akimtambulisha Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Japhet
Hasunga (kulia) kwa watumishi wa Wizara hiyo kabla ya kuzungumza nao leo mjini
Dodoma.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kushoto)
akizungumza na baadhi ya watumishi wa wizara hiyo baada ya kuwasili kwa mara ya
kwanza katika ofisi ya makao makuu ya wizara hiyo zilizopo mtaa wa Kilimani mjini
Dodoma leo.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...