MANISPAA ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, imetiliana saini mkataba wa sh.bilioni 5.56 na kampuni ya ukandarasi ya CRJE ya nchini China kwa ajili ya kuanza ujenzi wa kiwanda cha kuchakata taka kuwa mbolea aina ya mboji .

Kiwanda hicho ambacho kitakuwa na uwezo wa kuchakata takaka tani tano (5) hadi 100 kwa siku kitajengwa katika eneo la Mabwepande.Akizungumza wakati wa hafla ya utilianaji saini, Dar es Salaam, Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Banjamin Sitta amesema kuwa kiwanda hicho ambacho ujenzi wake unaanza rasmi leo kitakuwa na uwezo wa kuchakata taka ngumu na laini kuwa mbolea aina ya mboji.

Amesema manispaa imekuwa ikitumia kati ya sh.milioni 500 hadi 600 kwa mwezi kugharamia uzoaji wa taka ambazo hizo taka hazizalishi chochote.Sitta amesema Manispaa ya Kinondoni inazalisha tani 22,000 kwa siku hivyo kutumia fedha nyingi kuwalipa makandarasi.

Amesema zaidi ya wananchi 1000 wanatarajiwa kunufaika na ajira kupitia kiwanda hicho.Aidha amesema hatua hiyo kubwa ya kuitikia sera ya taifa ya kuelekea uchumi wa viwanda na kinondoni tunakuwa kuzalisha mbolea aina ya mboji ambayo haina madhara katika udongo ukilinganisha na mbolea za kemikali,”.

Meneja wa Kanda wa kampuni ya CRJE, Bai Haochen amesema, ujenzi wa kiwanda hicho unaweza kuchukua muda wa miezi 12 hadi 18.
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Banjamin Sitta na Meneja wa Kanda  wa kampuni ya CRJE,  Bai Haochen wakitiliana saini ya makubaliano ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata taka na kuwa mbolea leo jijini Dar es Salaam.
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Banjamin Sitta akizungumza na waandishi wa habari juu ya makubaliano na kampuni ya ukandarasi wa ujenzi wa kiwanda cha kuchakata taka kuwa mbolea leo jijini Dar es Salaam.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Banjamin Sitta na Meneja wa Kanda  wa kampuni ya CRJE,  Bai Haochen wakibadilishana hati za makubaliono leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...