Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Khamis Juma amewataka wahitimu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kujiendeleza katika fani ya Sheria kwa kuwa na hitaji na hamu ya kujiendeleza zaidi toka kiwango kimoja cha elimu hadi cha juu zaidi. Prof. Juma ameyasema hayo mjini Lushoto katika mahafali ya 17 ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama ambapo wahitimu 150 walitunukiwa Stashahada ya Sheria na wengine 142 walitunukiwa Astashahada ya Sheria.

Amesema kwamba wahitimu hao na wasomi wengine wa sheria nchini hawana budi kuzingatia kasi ya sasa ya maendeleo ya dunia na umuhimu wa elimu katika ulimwengu wa leo na kongeza kwa kutokana na hali hiyo ni lazima wajiendeleze zaidi katika fani hiyo. “ Ninawaasa popote pale mtakapokuwa someni na kujiendeeleza na jifunzeni mambo mapya kila siku, karne hii ya 21 ni karne ya teknolojia na habari , ni karne inayowategemea wahitimu wanaojiendeleza na kujifunza kila siku, jiendelezeni hadi kufikia viwango vya juu kulingana na kushindana na yeyote yule duniani , kumbukeni kuwa ajifunzae haachi kujua, naomba mtambue kuwa kujifunza ni kwekeza,” alisisitiza Jaji Mkuu

Mhe. Jaji Mkuu pia amewaasa wahitimu hao kuwa watakapopata kazi wahakikishe wanafanya kazi kwa bidii, uaminifu na kwa wakati ili kulinda maslahi ya Taifa na hivyo kuwa mabalozi wazuri wa Chuo. Awali akimkaribisha Jaji Mkuu katika mahafali hayo, Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa Mhe. John Mrosso amesema ndani ya miaka miwili chuo kimepata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kujielekeza katika masuala ya utafiti na ushauri ambapo inao wanataaluma 22 ambao wamejikita katika eneo hilo na kuwezasha wahitimu wa chuo hicho kupata ajira serikalini na kubuni vyanzo mbalimbali vya mapato ili kujiendesha.

Nae Mkuu wa Chuo hicha Mhe. Jaji Dkt. Paul Kihwelo alisema katika mwaka huu chuo kimefanikiwa kutoa wanafunzi 26 waliopata daraja la kwanza hali ambayo imetokana na kujitoa kwa wahadhiri na kujituma kawa wanachuo hao na hivyo kukiletea sifa chuo.

Amesema kama chuo wamepanga kuimarisha kitengo cha mafunzo, kuimarisha vyanzo vya mapato, kujenga uwezo wa watumishi ili kuhakikisha kinatekeleza kwa vitendo dhamira ya kuanzishwa kwa chuo ya kuboresha utendaji kazi wa Mahakama kupitia mafunzo kwa Maafisa wa Mahakama pamoja na wasaidizi wao na wadau wote wa sekta ya sheria nchini.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Khamis Juma akizungumza na wahatimu na wageni waalikwa katika mahafali ya 17 ya chuo cha uongozi wa Mahakama Lushoto ambapo wahitimu 292 walitunukiwa Stashahada na Astashahada za Sheria.
Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Jaji Dkt. Paul Kihwelo akizungumza kitu wakati wa mahafali ya 17 ya chuo hicho pembeni yake ni a na mgeni rasmi Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof Ibrahim Juma
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Jaji Mst. wa Mahakama ya Rufaa Mhe. John Mrosso akizngumza wakati wa Mahafali ya 17 ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto
Baadhi ya Wahitimu wa Stashahada ya Sheria wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Jaji Mkuu wa Tanzania wakati wa mahafali ya 17 ya chuo hicho baada ya kutunukiwa Stashahada zao
Baadhi ya Wahitimu wa Astashahada ya Sheria wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Jaji Mkuu wa Tanzania wakati wa mahafali ya 17 ya chuo hicho baada ya kutunukiwa Astashahada zao

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...