Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku Shahada ya Uzamivu katika Uchumi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Lameck Mwigulu Nchemba katika mahafali ya 47 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam  Jijini Dar es Salaam jana
 
Waziri wa Katiba na Sheria ambaye pia alikuwa amidi wa shughuli za sherehe za chuo Kikuu cha Dar es Salaam akimkabidhi mrithi wake Profesa Boniventure Rutinwa zana ya kutumikikia nafasi hiyo wakati wa mahafali ya 47 ya Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam. 
 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandara akitoa neno la shukrani mara baada ya zoezi la kuwatunuku degree zao wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wahitimu wakiwa katika nyuso za furaha kufuatia kuhitimu masomo yao kama walivyokutwa na mpiga picha wetu katika mahafali ya 47 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo.
 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Lameck Mwigulu Nchemba mara baada walipokutana katika mahafali ya 47 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo Jijini Dar es Salaam. Mwigulu Nchemba nimiongoni mwa wahitimu waliotunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Uchumi katika mahafali ya 47 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika leo Mlimani City. 
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Serikali waliotunukiwa Shahada ya Uzamivu katika Mahafali ya 47 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Lameck Mwigulu Nchemba na Mkurugenzi Mkuu wa Mamala ya Usimaizi wa Mifuko ya Hifadhi za Jamii (SSRA) Dkt. Irene Isack. 
Picha na MAELEZO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...