Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
Upande wa mashtaka katika kesi ya uchochezi kupitia mtandao inayomkabili mfanyabiashara Yericko Nyerere umeeleza kuwa katika ushahidi wa kesi hiyo, wanatarajia kuwaita mashahidi sita na kutoa vielelezo vitatu.

Wakili wa Serikali, Clara Charwe ameeleza hayo leo Novemba 21 mwaka huu baada ya kumaliza kumsomea maelezo ya awali (PH) mshtakiwa huyo mbele ya   Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage.

Katika kesi hiyo, Nyerere anashtakiwa kwa kuchapisha 
maneno yenye nia ya uchochezi kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook.

Akisomewa maelezo hayo, Yericko alikubali maelezo yake binafsi ikiwa ni jina lake, yeye ni Mfanyabiashara na kuwa alipelekwa mahakamani na kusomewa Mashtaka na kukanusha Mashtaka yote yanayomkabili.

Yericko anadaiwa  kuwa  Mei 28, 2017 kwa nia ya kuwachochea Watanzania alichapisha maneno kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook yasemayo;

Maazimio ya Baraza Kuu yalikuwa (1) Katiba Mpya (2) Tume Huru (3) Bunge (4) Haki ya Kikatiba ya kuishi (Ben Saanane) (5) Haki ya Kikatiba ya kukutana na kuzungumza (Mikutano ya Hadhara ya Kisiasa) Hayo ndio yatahubiriwa katika Operesheni Ukuta.

Baraza Kuu limeridhia kwa kauli moja kwamba vita rasmi ya kulikomboa taifa imezinduliwa na kama wewe Mtanzania unaogopa kulitetea taifa hili ni bora uka kaa kando, nenda huko CCM ambako michemsho na supu vipo kwa wingi…kufa kwetu ni ukombozi wa Tanzania…..

Yaani sasa tunarejesha siasa za jino kwa jino, uso kwa uso, mguu kwa mguu, weka mguu ni weke ugoko… Ni mwisho kuishi kinyonge, ni mwisho kulalamika, ni mwisho watu wetu kutekwa au kuuawa, ni mwisho watu wetu kuzuiwa kufanya mikutano ya hadhara…Tunasema sasa ni single touch double manifestational.” Mwisho wa kunukuu. Yericko yupo nje kwa dhamana.
Kesi hiyo itaanza kusikilizwa Decemba 16 mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...