Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imezitaka pande wa zote mbili, ule utetezi na wa mashtaka kufanya kazi kwa kishirikiana kwa ukaribu ili kufuatilia jalada la kesi inayomkabili rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF), Jamal Malinzi na wenzake lilirudi kutoka (DPP). ambalo liko huko kwa zaidi ya muda wa siku 37.

Maagizo hayo yametolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri leo Novemba 17/2017 baada upande wa mashtaka kusema upelelezi katika kesi hiyo haujakamilika.

Mwendesha Mashtaka wa Takukuru,Leonard Swai aliiomba mahakama kupanga tarehe nyingine dhidi ya kesi hiyo kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wake bado haujakamilika.Swai alidai kuwa jalada la kesi hiyo bado lipo kwa DPP na kwamba uongozi wa Takukuru na kwamba wanalifuatilia.

Wakili wa utetezi, Abraham Senguji Senguji alidai kuwa kama upande wa Mashtaka hauwezi kukamilisha upelelezi waiondoe kesi hiyo chini ya kifungu cha 91(1) cha mwenendo wa makosa ya Jinai.

Amedai kuwa kutokana na mgongano wa ofisi ya DPP na Takukuru wanaoumia ni wateja wao ambapo wameshtakiwa kwa makosa ambayo hayana dhamana.Mahakama ipo kwa ajili ya kuangalia haki za upande wa Mashtaka na utetezi. Hivyo kama hawajamaliza kupeleleza waiondoe kesi hiyo mahakamani na pale watakapokamilisha upelelezi, wawarejeshe ili kesi iendelee.

Akijibu hoja hizo, Wakili Wa Takukuru Leornad Swai alidai wakimaliza uchunguzi ni lazima jalada liende kwa DPP alipitie na atoe maelekezo kama upelelezi uliofanywa unajenga kesi ama la.

Hata hivyo aliongeza kudai kuwa makosa ya kughushi yanahitaji utaalam katika kuyathibitisha na yanachukua muda mrefu katika uchunguzi

Kesi imeahirishwa hadi Novemba 30,2017.

Katika kesi hiyo, washtakiwa wengine ni Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mhasibu wa shirikisho hilo, Nsiande Mwanga.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 28, yakiwamo ya utakatishaji fedha wa Dola za Marekani, 375,418.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...