Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa PAUL MAKONDA ameandaa tamasha la kuwakaribisha Wanafunzi wa Mwaka wa kwanza kwa Vyuo Vikuu vya Mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo, kuwaepusha kuingia kwenye makundi hatarishi. 

Tamasha hilo linalotaraji kufanyika eneo la Maegesho Mliman City litatawaliwa pia na Burudani kutoka kwa Wasanii Mbalimbali ambapo vyombo vya Habari vya TBC, CHANNEL TEN NA E FM wamejitolea kulibeba tukio hilo la kipekee. RC MAKONDA amesema hayo wakati wa Mkutano na hafla ya kupata Chai na Maraisi wa Vyuo Vikuu vya Mkoa wa Dar es salaam pamoja na Viongozi wa Asasi za Kiraia. 

Katika Mkutano huo Vyuo vikuu vimeunga Mkono kampeni ya ujenzi wa Ofisi za Walimu kwa kuchangia Mifuko 25 ya Saruji na kuahidi kuendelea kuunga mkono kampeni hiyo. Aidha RC MAKONDA ametoa nafasi kwa Vyuo vikuu kumuweka kikaangoni kwa kufanya mdahalo wa kubadilishana mawazo na kuelezana changamoto.

RC MAKONDA pia amesema anao mpango wa kuandaa Shindano la Uongozi Wanafunzi wa Vyuo vikuu kwa lengo la kuwajengea Wanafunzi uwezo wa uongozi bora na namna ya kupatia majibu changamoto ambapo Mshindi atapata ofa ya kusoma Bure Chuo cha Diplomasia. 

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi kanda Maalumu ya Dar es Salaam LAZARO MAMBOSASA amewaomba Wanafunzi wa vyuo vikuu kutoa taarifa kwa jeshi la Polisi pale wanapobaini uwepo wa Wahalifu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...