Ziara ya kutembelea nchi ya Israel iliyoandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania na kuhususisha viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii imeanza kuzaa matunda ambapo mtaalamu wa mfumo wa mawasiliano kutoka Israel, Dkt Norma Kortiat amewasili nchini kwa ajili ya kutoa mafunzo yanayohusiana na jinsi ya kutangaza utalii wa Tanzania kwa njia ya kidigitali “Digital Marketing”. 

Mafunzo hayo yanategemewa kuwawezesha watumishi kuongeza ufanisi kwa wa kutumia teknologia mpya katika kuvitangaza vivutio vya utalii vya Tanzania. Mafunzo haya ya siku mbili yameanza leo tarehe 21-22 yanafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam ambayo yanahudhuriwa na watumishi Kutoka Idara ya Utalii , Bodi ya Utalii, Mamlaka ya Wanyama Pori,Mamlaka ya Hifadhi za Taifa, Mamlaka ya Bonde la Ngorongoro, Wakala wa Huduma za Misitu na kamisheni ya Utalii Zanzibar.
Dkt. Noam Koriat akitoa mafunzo kwa watumishi wa Wizara ya Utalii na Taasisi zake katika ukumbi wa mikutano wa Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Watumishi wakimsikiliza Dkt. Noam Koriat wakati wa mafunzo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...