Na Teresia Mhagama.

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewaagiza watendaji wa TANESCO kuhakikisha kuwa hawakati Umeme bila sababu maalum na hivyo kuwaondolea wananchi adha ya kukosa nishati hiyo.

Naibu Waziri aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya kukagua mradi wa TEDAP unaohusu upanuzi na ujenzi wa vituo vya kupozea Umeme na njia za Umeme ambapo vituo vya kupozea Umeme alivyovitembelea ni Mbagala, Gongo la Mboto, Kipawa na City Centre.

“Umeme ukatike pale inapostahili tu, na endapo tatizo linatokea mfano kwenye mifumo ya Umeme ni muhimu mkatoa taarifa mapema kwa wananchi,” alisema Subira Mgalu.

Aliongeza kuwa ukatikaji wa Umeme unasababisha malalamiko kutoka kwa Wananchi kwani kukosekana kwa nishati hiyo kunaathiri shughuli nyingi hasa za kimaendeleo na kiuchumi zinazowaingizia kipato.

Aidha Naibu Waziri aliwaagiza watendaji wa TANESCO wanaosimamia mradi huo wa TEDAP jijini Dar es Salaam, kuhakikisha kuwa kazi hiyo inakamilika tarehe 15 Desemba, 2017.

Vilevile alieleza kuwa utekelezaji wa miradi hiyo unaendelea vizuri na kwamba kukamilika kwake kutaboresha hali ya upatikanaji wa Umeme katika jiji la Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, (wa kwanza kushoto) akiwa katika eneo la Mbagala jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kukagua mradi wa uboreshaji wa Vituo vya Umeme na ujenzi wa njia za Umeme jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Meneja Mradi wa Usafirishaji na Usambazaji Umeme kutoka TANESCO, Mhandisi Emmanuel  Manirabona.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, (wa pili  kushoto) akikagua mitambo ya Umeme katika kituo cha City Centre jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kukagua mradi wa uboreshaji wa Vituo vya Umeme na ujenzi wa njia za Umeme jijini Dar es Salaam.Wengine katika picha ni watendaji kutoka TANESCO.
 Baadhi ya mitambo ya Umeme katika kituo cha Mbagala  jijini Dar es Salaam iliyojengwa chini ya mradi wa uboreshaji wa Vituo vya Umeme na ujenzi wa njia za Umeme jijini Dar es Salaam.
 Miundombinu ya kusafirisha Umeme  wenye Msongo wa kV 132 iliyojengwa katika eneo la Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa Vituo vya Umeme na ujenzi wa njia za Umeme jijini Dar es Salaam.

HABARI  ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...