Na Rhoda Ezekiel -Kigoma.

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, ambae pia ni mlezi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kigoma,Abdallah Burembo amewaagiza Viongozi wapya wa Chama hicho Mkoani Kigoma kuhakikisha Wanayarudisha majimbo ya Kigoma mjini na Kakonko na kata zote zilizochukuliwa na upinzani .

Aidha amewataka kufanya kazi ya chama ya kusimamia ilani ya chama cha mapinduzi kwa kuwatuma kazi Viongozi wa serikali, na kuwakagua kama Wanatekeleza pamoja na kuwaacha Wabunge kufanya wajibu wao na kuacha Makundi makundi katika siasa kwa kuwaweka Wana CCM pamoja ilikuhakikisha ushindi wa majimbo yote kigoma .

Wito huo ameutoa  jana, baada ya kutangaza matokeo ya uchaguzi wa Mkoa katika Mkutano Mkuu wa Mkoa wa Kumchagua Mwenyekiti wa Mkoa , Mjumbe wa baraza kuu taifa NEC na wajumbe wa halmashauri kuu ya Mkoa, ambapo Burembo aliwapa pole viongozi hao waliochaguliwa kwakuwa Wanakazi kubwa ya kuhakikisha Majimbo yanayotawaliwa na chama tawala yaendelea kuwepo na kuyarudisha yale yote yaliyo chini ya upinzani pamoja na kata zote.

Hata hivyo katika uchaguzi huo nafasi ya Mwenyekiti wa Mkoa ilichukuliwa na Amandusi Nzamba aliewashinda wenzake watano kwa kura 371 akifatiwa na Hamis Betese kura 249 akifuata aliekuwa mwenyekiti wa zamani Amani Kabour 97, Philipo Tabhiliho kura mbili na Antony Mpozemenya tisa,pamoja na nafasi ya Mjumbe wa baraza kuu taifa ilichukuliwa na Kilumbe Ngenda alie shinda kwa kura 426 kati ya Wagombea wenzake Asha Baraka na Atanasi dyoya.

"Tutawapima viongozi mliochaguliwa pamoja na viongozi wa serikali kutokana na ushindi tutakao upata hatuwezi kishindwa katika uchaguzi wakati Dc upo Mkurugenzi Upo na Mkuu wa Mkoa upo, serikali ni ya chama cha mapinduzi waliopo chini ya serikali wanaitumikoa serikali na kutekeleza ilani yetu kama kuna mtendaji au mkurugenzi hafuati utekelezaji wa ilani tutawatoa tuambieni wanao sababisha sisi tushindwe kuaminika hatuwezi kukubari tuyakose majimbo haya tunayataka kwa gharama yoyote ile", alisema Mwenyekiti wa jumuia ya Wazazi.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...