Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
Kesi ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili Mlimbwende wa Tanzania mwaka 2006 na msanii maarufu wa Filamu nchini,  Wema Sepetu  itaendelea kusikilizwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka Januari mwaka kesho.

Kesi hiyo iliyoko katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo ilipaswa kuendelea kusikilizwa  mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo Wakili wa Serikali, Costantine Kakula alieleza kuwa wapo tayari kwa ajili ya kuendelea na ushahidi na wana mashahidi wawili.

Hata hivyo wakili wa utetezi, Devotha Kianga aliyekuwa akimuwakilisha wakili Peter Kibatala aliomba kesi hiyo iahirishwe hadi tarehe nyingine
kwa kuwa wakili Kibatala  ambaye anamtetea, wema na wenzake wawili, yuko Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi kwenye kesi namba 85 ya mwaka 2016.

Kutokana na maelezo hayo, Hakimu Simba aliiahirisha kesi hiyo hadi Januari 10, 2018.

Washtakiwa wengine wanaoshtakiwa pamoja na Wema, ni Angelina Msigwa  na Matrida Seleman Abbas. Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.

Inadaiwa  kuwa  Februari 4, 2017 katika Makazi ya Wema huko Kunduchi Ununio  washtakiwa hao walikutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.

Kwa upande wa Wema yeye anadaiwa kuwa Februani Mosi, 2017 katika  eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam,  alitumia dawa za kulevya  aina ya Bangi.

Wema ni miongoni mwa watu waliotajwa na Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda wakituhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya.

Inadaiwa kuwa Februari 3, 2017, Wema alijipeleka mwenyewe katika Kituo cha Polisi Kati ambapo alikamatwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...