Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
Kijana
mzalendo, Omary Kombe amejipanga kutembea kutoka Kimara hadi Kivukoni
siku ya Jumamosi, Januari 20, 2018 ili kuunga mkono juhudi za Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli katika
kuliletea Taifa maendeleo.
Kombe
ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na
Waandishi wa Habari juu ya nia ya matembezi yake pamoja na mpango wake
wa kutoa tuzo kwa Rais Magufuli itakayojulikana kama ‘Tuzo ya Kiongozi
Mzalendo’.
Kombe
amesema kuwa Rais Magufuli amekuwa ni kiongozi makini, mwenye uthubutu,
mwenye msimamo thabiti na mzalendo wa kweli kwani amefanya mambo
mbalimbali yakiwemo ya kuimarisha mfumo wa ulipaji kodi, kubadilisha
sheri kandamizi za madini, kukomesha vitendo vya ujangili katika mbuga
za wanyama, rushwa na dawa za kulevya pia kurejesha nidhamu kwa
watumishi wa umma.
“Kubwa
kuliko yote, Serikali ya Awamu wa Tano kwa ujumla imekuwa ikihamasisha
kwa vitendo kuhusu ujenzi wa Tanzania ya Viwanda na kupelekea nchi kuwa
na uchumi wa kati hivyo kwa niaba ya vijana wazalendo napenda kumpongeza
kwa kufanya matembezi, kumpa tuzo ya kiongozi mzalendo pamoja na kutoa
msaada katika hospitali ya Ocean Road iliyopo jijini hapa,” alieleza
Kombe.
Kijana Mzarendo,Omary Kombe akizungumzana na waandishi wa hawapo pichani juu ya kutembea kutoka Kimara hadi Kivukoni siku ya Jumamosi, Januari 20,mwaka huu ili kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli katika kuliletea Taifa maendeleo, Mwenyekiti Mwenza Kamati ya Kutoa Elimu ya Unyonyaji kwa Watu Wenye Ualbino, Maiko Lugendo.
Mwenyekiti Mwenza Kamati ya Kutoa Elimu ya Unyonyaji kwa Watu Wenye Ualbino,Maiko Lugendo akimkabdhi Kijana Mzarendo,Omary Kombe t-shirt atakayo vaakesho kwaajili ya matembezi hayo.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...