Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Marlin Komba amesema hamtambui mtu anayejiita nabii Tito na kwamba hajasajili kanisa lake katika ofisi ya msajili wa taasisi za dini, na kwamba Serikali imeona vitendo anavyovifanya ‘nabii’ huyo kupitia mitandao ya kijamii na imeanza kuchukua hatua.
“Ninachoweza kusema ni kwamba hakuna mtu anayezuiwa kuongea hapa nchini, mwache aongee anavyoweza ila Serikali imeshaona anachokifanya na yanayoendelea mitandaoni hatua zinachukuliwa dhidi yake,” amesema Komba.
Kauli hii imekuja kufuatia kusambaa kwa video mbalimbali zikimuonyesha ‘nabii’ huyo akitoa mafundisho yake huku akinywa vilevi pamoja na kufanya matendo ambayo ni kinyume cha maadili ya dini, jambo ambalo limeonekana kuwakera wadau wengi wa dini.
Kwa upande wao viongozi mbalimbali wa dini wameonyeshwa kukerwa na kulaani vitendo anavyovifanya mtu huyo anayejiita ‘nabii’ na kusisitiza kuwa hakuna dini inayoruhusu hayo.
Askofu Msaidizi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Mchungaji Chediel Lwiza amesema kuwa, kutokana na vitendo anavyofanya, mtu huyo hapaswi kujiita mtumishi wa Mungu.
“Huyo hawezi kuwa mtumishi wa Mungu na wala hafanyi huduma ya kanisa. Ni vyema watu kama hawa wafuatiliwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao. Natumaini Wizara ya Mambo ya Ndani ambayo ndani yake ina ofisi ya msajili wa taasisi za dini itafanya kazi yake,” amesema Mchungaji Lwiza.
Naye Msemaji wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Rajab Katimba amesisitiza Serikali na viongozi wa dini kuingilia kati suala hilo na kueleza kuwa, hakuna kitabu chochote cha dini kinachohamasisha ulevi na ukosefu wa maadili.
“Hilo suala linakwenda tofauti na dini na mila na desturi zetu pia. Dini zinatakiwa kuleta amani na kuhamasisha watu waheshimiane si kuzungumza mambo yanayokiuka maadili yetu. Naona ipo haja ya viongozi wa dini na Serikali kuingilia suala hili na waende mbali zaidi kwa kuongea naye huenda hafahamu anachokifanya,” amesema Rajab Katimba.

Source- JF
 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro akimsikiliza mhubiri wa kujitegemea ajiitaye Nabii Tito ambaye ametiwa mbaroni na Jeshi la Polisi mkoani Dodoma kwa tuhuma za kutoa maneno yaliyo kinyume na maadili. Nabii Tito anashikiliwa nan a jeshi hilo kituo cha kati mjini Dodoma. Taarifa kamili itafuata baadaye.
Nabii Tito akiwa chini ya ulinzi Central Police Dodoma leo. Ifuatayo hapo chini  video iliyopigwa mwaka 2013 wakati "akihubiri" mitaani jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Imeandikwa kwenye bibilia kuwa Many will come in my Name. Tunawaona siku hizi manabii kila kona. Imekuwa ni njia ya kujitafutia maisha ya juu na mali za kujitapa.These are the false prophets mentioned in Mathew 24:11 And many false prophets will arise and mislead. Mathew 7:15 yatuonya tujihadharishe na hawa jamaa ambao wajidai kuwa ni manabii kumbe ni mbwa mwitu waroho.
    Karibu Nchi zote zina sheria zinazolinda haki za dini na kuabudu, they are exploiting this kindness.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...