Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

KATIBU Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu),Profesa Faustine Kamuzora amesema jukwaa la usimamizi wa maafa la Taifa linahitaji utashi wa kisiasa,uwajibikaji kisheria ,uelewa wa umma ,elimu ya kisayansi  na mipango makini ya maendeleo ili kutekeleza majukumu yake.

Profesa Kamuzora amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua jukwaa la Usimamizi wa Maafa la Taifa lililofanyika kwa mara ya kwanza jijini Dar es Salaam.

“Jukwaa hili ni chombo cha kisheria hapa nchini kwa ajili ya kutathmini na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Serikali kuhusu majanga ya aina zote, hivyo linaundwa kwa kuzingatia kifungu cha 40 cha Sheria ya Usimamizi wa maafa namba 7 ya mwaka 2015,” amesema Profesa Kamuzora.

Amesema jukwaa hilo linakutana kwa mara ya kwanza toka sharia hiyo ianze kutumika hapa nchini, hivyo jukwaa linatoa fursa ya utaratibu wa usimamizi wa maafa kwa ushirikiano wa wataalam wa fani mbalimbali kwa kujumuisha sekta ya umma na sekta binafsi, mashirika ya kimataifa na Umoja wa Mataifa.

Ameongeza jukwaa linawajibu wa kushughulikia changamoto za kijamii ,kiuchumi na mazingira ya kufanya kazi kwa ushirikiano ili kufanikisha kujumuisha upunguzaji wa madhara ya maafa katika mipango na sera za maendeleo ya Taifa na katika misaada ya kibinadamu.
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustine Kamuzora akizungumza alipokuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa kikao cha kwanza cha Jukwaa la Taifa la Usimamizi wa Maafa leo Jijini Dar es Salaam. Jukwaa hilo limejumuisha wadau mbalimbali kutoka sekta za umma na sekta binafsi ambao kwa namna moja wanajishughulisha na masuala ya kukabiliana na maafa na majanga.
 Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa toka Ofisi ya Waziri Mkuu Bigedia Jenerali Mstaafu Mbazi Msuya akielezea jambo wakati wa ufunguzi wa kikao cha kwanza cha Jukwaa la Taifa la Usimamizi wa Maafa leo Jijini Dar es Salaam. Jukwaa hilo limejumuisha wadau mbalimbali kutoka sekta za umma na sekta binafsi ambao kwa namna moja wanajishughulisha na masuala ya kukabiliana na maafa na majanga.Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara hiyo Bashiru Taratibu, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustine Kamuzora na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maafa Ukanda wa Afrika (UNISDRI) Julius Kabubi.
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustine Kamuzora akiteta akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa kikao cha Jukwaa la Taifa la Usimamizi wa Maafa leo Jijini Dar es Salaam. Jukwaa hilo limejumuisha wadau mbalimbali kutoka sekta za umma na sekta binafsi ambao kwa namna moja wanajishughulisha na masuala ya kukabiliana na maafa na majanga.(Picha na: Frank Shija – MAELEZO) 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...