Na John Mapepele

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina amekitoza faini ya Shilingi milioni mia moja Kiwanda cha Sunflag Tanzania Limited cha jijini Arusha baada ya kukutwa na makosa mawili ambayo ni kuzalisha na kuuza nyavu bila kuwa na leseni kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na kuzalisha na kuuza nyavu ambazo ziko kinyume na matakwa ya Sheria ya Uvuvi namba 22 ya mwaka 2009.

Kulingana na maelezo ya Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho Ajay Shah, kiwanda kimekuwa kikitengeneza vyavu hizo haramu kwa miaka mitatu mfululizo sasa ambapo inakadiliwa kuwa tayari kimeshatengeneza tani 1296 nyavu hizo zenye thamani ya shilingi bilioni nne.

Akitoa taarifa kwa Waziri Mpina, Kiongozi wa kikosi kazi cha kutokomeza uvuvi haramu katika kanda ya Ziwa Victoria, West Mbembati amesema kuwa tarehe 17/1/2018 walifika kwenye kiwanda hicho na kukamata marobota 584 yenye thamani ya milioni mia kufuatia maelekezo ya Waziri Mpina yaliyotolewa Mjini mwanza hivi karibuni baada ya mfanyabiashara Dastan Venanti kukamatwa na nyavu hizo zenye thamani ya milioni sitini na tano ambazo nyaraka zilionyesha alinunua katika kiwanda hicho.

Akipokea taarifa hiyo Waziri Mpina alisema mkakati uliopo kwa sasa ni kuwabaini watengenezaji na wasambazaji wote wa zana haribifu za uvuvi ikiwa ni pamoja na vyavu zisizoruhusiwa kisheria ambapo amesema hatua za kali za kisheria dhidi yao zitatumika ili kudhibiti uvuvi haramu kwenye maji(mito,maziwa na bahari) ya nchi yetu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Sunflag cha mjini Arusha, Ajay Shah, akiongoza zoezi la kuchoma nyavu haramu za dagaa zilizo chini ya sentimita 8 (marobota 584) zenye jumla ya shilingi milioni mia moja zilizokamatwa kwenye Kiwanda chake na Kikosi Kazi Maalum cha Kutokomeza Uvuvi Haramu nchini kilichoundwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Joelson Mpina kwenye dampo la takataka nje kidogo ya jiji la Arusha leo.(Na John Mapepele)
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Joelson Mpina (mwenye kofia) akikagua chumba cha baridi cha kuhifadhia samaki (Cold room) cha kampuni ya Alpha Choice mjini Arusha leo akiwa katika operesheni maalumu ya kudhibiti uvuvi haramu kulia ni mmliki wa kampuni hiyo Yussuf Khatry. 
Marobota 584 ya nyavu haramu yaliyotengenezwa na Kiwanda cha Sunflag cha mjini Arusha yenye thamani ya shilingi milioni 100 wakitekea kwenye dampo nje ya jiji la Arusha leo. Marobota hayo alikamatwa na Kikosi Kazi Maalum cha Kutokomeza Uvuvi Haramu nchini kilichoundwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Joelson Mpina ambapo uteketezaji huo uliongozwa na mmliki wa kiwanda hicho Ajey Shah.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Joelson Mpina (mwenye kofia) akisikiliza taarifa ya ukamataji wa marobota 584 ya nyavu haramu yaliyotengenezwa na Kiwanda cha Sunflag cha mjini Arusha yenye thamani ya shilingi milioni 100 kutoka kwa kiongozi wa Kikosi Kazi Maalum cha Kutokomeza Uvuvi Haramu nchini West Mbembati aliye kulia, kushoto mwakilishi wa Afisa Tawala wa Mkoa wa Arusha David Lyamongi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...