Kamati ya Maadili iliyokutana Januari 18, 2018 imepitia shauri lililowasilishwa na Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF wakiwatuhumu viongozi wanne kwa makosa ya kughushi na udanganyifu wa mapato kwenye mchezo namba 94 kati ya Ndanda FC na Simba uliochezwa Disemba 30,2017.

Shauri la kwanza lililomuhusu Katibu msaidizi wa Ndanda Ndugu Selemani Kachele,Kamati imegundua kuwa mtuhumiwa aliitwa wakati wa kuhesabu mapato kuthibitisha deni dhidi ya Ndanda lenye thamani ya Shilingi Milioni mbili laki mbili na elfu hamsini(2,250,000),deni ambalo TFF waliagiza wakatwe kwenye mapato ya mechi hiyo,Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Mtwara alithibitisha kuwa alimuita kuthibitisha uhalali wa deni hilo baada ya Muhasibu wa Ndanda kugoma kulipa deni hilo ambalo linahusu pango la Ndanda kwa Mama mwenye Nyumba.

Hata hivyo Kamati ilimuhoji zaidi na akashindwa kutoa uthibitisho wa kulipwa kwa deni hilo na hakuna kumbukumbu zozote zinazoonyesha kuwa deni hilo limelipwa.Kamati imempa onyo kwa mujibu wa kifungu cha 6(1)(a) kanuni za maadili ya TFF toleo la 2013 na imeiomba Sekretarieti ya TFF ifuatilie kama deni hilo limeshalipwa ili kuepusha ulipaji wa Zaidi ya mara moja.

Shauri la Pili lilimuhusu Muhasibu msaidizi wa Simba Ndugu Suleiman Kahumbu.Kamati haikuendelea na tuhuma dhidi yake baada ya Sekretarieti ya TFF kuamua kuondoa shauri dhidi yake kwa kuwa alitoa ushirikiano na kutosheka kuwa hana hatia na badala yake alitumika kama shahidi wa upande wa washtaki.

Shauri la tatu lilimuhusu Katibu mkuu wa Chama cha soka Mtwara Ndugu Kizito Mbano.Kamati ilimuhoji mtuhumiwa na alikiri kuwepo kwa mawasiliano na msimamizi wa kituo Ndugu Dunstan Mkundi kuhusu nia ya kughushi fomu ya marejesho ya mapato ya mchezo kati ya Ndanda FC na Simba SC.

Ndugu Kizito Mbano hakutoa taarifa yoyote ile wala kuonyesha ushirikiano kwa Sekretarieti ya TFF na Bodi ya Ligi wakati yeye akiwa msimamizi msaidizi wa kituo na Katibu Mkuu wa Chama cha Soka cha Mkoa wa Mtwara,hivyo Kamati imemkuta na hatia na imemuhukumu kutojihusisha na shughuli za Mpira wa Miguu kwa kipindi cha miaka Mitano(5) kwa mujibu wa kifungu cha 73(7) cha kanuni za maadili TFF toleo la 2013.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...