Na Said Nwishehe,Globu ya Jamii

MWENYEKITI wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika,Dk.Titus Kamani amesema Serikali kupitia tume hiyo ni awaelekeza viongozi wa Vyama vya Ushirika kutojihusisha kuuza mali za vyama hivyo pasipo kuzingatia sheria.

Hivyo amesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kuuza mali za vyama hivyo na kufafanua ili kudhibiti hali hiyo Ofisi za Mrajisi wa vyama vya ushirika imekuwa ikichukua hatua ikiwa pamoja na kuwaondoa viongozi wanaokiuka sheria.

Dk.Kamani amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anaelezea udhibito wa mali za ushirika na mpango wa makusanyo na mauzo ya mazao makuu matano ya kimkakati kupitia mfumo wa ushirika.

Amesema vyama vya ushirika nchini vinaendeshwa kwa kuzingatia sheria ya vyama vya ushirika namba 6 ya mwaka 2013.Hivyo vyama vinapaswa kuzingatia sheria wanapotekeleza majukumu yao.Dk.Kamani amesema Serikali kupitia Tume ya Maendeleo ya Ushirika inaelekeza viongozi wa vyama hivyo kuwa makini kuzingatia sheria.

Amefafanua vyama vina haki ya kumiliki mali na kuuza mali hizo pale itakapoona inafaa kwa kuzingatia shetia iliyopo.Pia mali zinazomilikiwa na vyama zinapaswa kuwa zimerasimishwa ili kuleta uhalali wa umiliki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...