Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma akisalimiana na watumishi wa Mahakama ya wilaya ya Nzega alipowasili kukagua shughuli za Mahakama. Jaji Mkuu ameanza ziara ya kikazi katika mkoa wa Tabora na Kigoma ambayo ni Kanda ya Tabora.
Na Lydia Churi-Tabora

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewataka Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo nchini kusimamia mabaraza ya kata yaliyoanzishwa kwa Shjeria yam waka 1985 kwa kuwa mabaraza hayo ni sehemu muhimu katika mfumo wa utoaji haki kutokana na kazi yake ya kusuluhisha na kupatanisha mashauri madogo madogo ya jinai na madai.

Akizungumza na Watumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Igunga na Nzega pamoja na Mahakama ya Mwanzo ya Ziba na Nyasa mkoani Tabora, Jaji Mkuu amesema mfumo wa utoaji haki kupitia mabaraza ya kata unawaunganisha wananchi tofauti na pale kesi inaposikilizwa Mahakamani ambapo mar azote aliyeshindwa hujenga uadui na aliyeshinda.

Jaji Mkuu amesema endapo mabaraza ya Kata yatasimamiwa ipasavyo ni wazi kuwa idadi ya kesi zinazofunguliwa kwenye Mahakama za Mwanzo nchini itapungua kwa kiasi kikubwa kwa kuwa kesi nyingi zitaamuliwa kwenye mabaraza hayo kwa njia ya usuluhishi na upatanishi. Aliongeza kuwa kesi zote zinazosajiliwa nchini asilimia 74 ni za Mahakama za Mwanzo.

Amesema ili kuimarisha mfumo wa utoaji haki kupitia mabaraza ya kata, Mahakama ya Tanzania imeandaa mpango wa mafunzo utakaowakutanisha Mahakimu pamoja na wajumbe wa mabaraza ya kata.
Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma akizungumza.
Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Godfrey Ngulupa akimpokea Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma alipowasili ofisini kwake Nzega.
Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma akimkabidhi Mkuu wa wilaya kitabu kinachoelezea Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania pamoja na Jarida la Mahakama alipofika ofisini kwake kumtembelea .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...