Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amepiga marufuku dawa za serikali kuonekana zikiuzwa kwenye maduka ya watu binafsi kwani serikali haitaki kuingia kwenye matatizo ya uhaba wa dawa kwenye sehemu zake za kutolewa huduma ya afya. 

Dk. Ndugulile amepiga marufuku dawa za serikali kuonekana zikiuzwa kwenye maduka ya watu binafsi wakati wa ziara yake ya kikazi katika wilaya ya Shinyanga, Februari 21,2018 akikagua shughuli za huduma za afya zinavyotolewa kwa wananchi pamoja na kutoa hamasa kwa jamii kujiunga na Bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa.

Dk. Ndugulile alisema katika bajeti ya mwaka wa fedha (2017-18) serikali kwenye bajeti ya wizara hiyo ya afya imetenga jumla ya shilingi bilioni 270, tofauti na mwaka wa fedha (2015-16) ambapo zilikuwa milioni 30 hivyo hawatarajii kusikia sehemu za kutolewa huduma zake za kiafya kuwa zina upungufu wa dawa.

Akiwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga na Kituo cha Afya cha Kambarage manispaa ya Shinyanga na kukagua bohari za dawa, Dk. Ndugulile alitoa tahadhari kwa wauguzi kuwa ni marufuku dawa hizo za serikali kukutwa zinauzwa kwenye maduka ya watu binafsi na ikibainika watachukuliwa hatua kali.

“Serikali ya awamu hii ya tano imedhamiria kuboresha huduma za afya hapa nchini, na ndio maana hata bajeti yake imetolewa ni ya fedha nyingi hivyo sisi kama wizara husika hatutarajii kuwepo kwa upungufu wa dawa kwenye sehemu za huduma za afya”,alieleza.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa katika bohari ya dawa kwenye kituo cha afya kata ya Kambarage mjini Shinyanga. Picha zote na Marco Maduhu na Steve Kanyefu
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa ameshika kopo la dawa katika bohari ya dawa kwenye kituo cha afya Kambarage mjini Shinyanga na kusisitiza kuwa dawa zenye nembo ya dawa za serikali MSD hazitakiwi kutoka nje ya hospitali za serikali.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akimsalimia mgonjwa katika kituo cha Afya Kambarage mjini Shinyanga huku akiangalia dawa alizopewa mgonjwa na kupiga marufuku wagonjwa kuambiwa dawa hakuna na kwenda kununua kwenye maduka ya dawa ya watu binafsi.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulileakikagua chumba cha upasuaji katika kituo cha afya Kambarage mjini Shinyanga, na kuagiza jengo hilo lifanyiwe marekebisho ili kuendana na hadhi ya chumba cha upasuaji, sababu haliridhishi kuendana na huduma ambayo itakuwa ikitolewa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...