Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) Gianni Infantino tayari amewasili nchini Tanzania majira ya saa 9 usiku wa kuamkia leo (22/02/2018) akiwa ameambatana na Rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) Ahmad Ahmad. 
 Ugeni huo umepokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na Waziri wa Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe aliyeambatana na Mkurugenzi wa michezo, Yusuph Singo, Rais wa TFF Wallace Karia, Mwenyekiti wa Baraza la Michezo na Mjumbe wa Heshima wa CAF na FIFA Leodagr Tenga, pamoja na viongozi wengine. Mara baada ya kuwasili, Dkt. Mwakyembe amefanya mazungumzo mafupi na Rais huyo wa FIFA Viongozi hao wakuu wa FIFA wanahudhuria mkutano wa kawaida wa kila mwaka ambao mwaka huu unafanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Tanzania. Hii ni mara ya kwanza kwa mkutano huu kufanyika Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...