kabla ya miss tz hii ya miaka hii, kulikuwepo na mashindano ya ulimbwende hasa yaliyohusu mavazi na mitindo kama vile farida fashion, miss mirinda na kadhalika. baadhi ya kinadada waliokuwa wakitamba sana ni hawa. kuna mdau alitaka kumuona stella tingisha ambaye ni huyo kulia.

PS: NAPENDA KUTOA SHUKRANI KWA WOTE MNAONITEMBELEA NA KUFIKIA SASA ZAIDI YA 15,000. KWA KWELI NIMEHEMEWA NA SINA CHA KUWALIPA ZAIDI YA KUWAAHIDI PICHA NA HABARI ZAIDI KWANI NINA HAZINA YA PICHA KUMI KWA SIKU KWA MIAKA 25 IJAYO - NA HAPO NI ZA MAKTABA, SIJAPIGA MPYA...

ASANTENI SANA HATA NYIE MNAOTUMIA BLOGU LETU HILI KWA KUTOA LUGHA CHAFU. MUNGU AWAJAALIE NA AZMA ZENU INSHAALAAH ZITATIMIA.

AMINA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kwa haraka haraka tu nina weza kusema yafuatayo kwa wahusika wanao taka kumkatisha tamaa Ndugu Michuzi:

    1: Eidha ni watu ambao nao wana blog za picha hivyo wanataka kumuaribia Ndugu Michuzi umaarufu wake ili watu waende ktk blog zao.

    2: Ni watu wanao mjua ndugu Michuzi na kuleta chuki zao Binafsi.

    3: Inawezekana hao watu wapo ktk sekta moja ya uandishi wa habari na wanamjua Ndugu Michuzi na kuleta chuki zao Binafsi kutokana na mawazo yao yaliyopo Vichwani mwao.

    4: Wamekosa hekima na Busara na mafundisho mema ya maisha ktk dunia hii toka wakiwa wadogo, Ambapo inatakiwa kila binadamu kuheshimiana na kupendana.

    5: Ina wezekana wana matatizo ambayo yana wafanya kuacha kazi zao za msingi na kuanza kusema watu, kutumia lugha za matusi na kutaka kumkatisha tamaa ndugu Michuzi.

    Mwisho, Ndugu Michuzi wewe ni mtu mzima ninge kuomba hachana na hawa watoto wadogo wenye matatizo ktk maisha yao, na siku zote kumbuka ktk maisha kuna watu kama hao wanao taka sisi tukate tamaa ktk maisha tuliyo nayo sasa cha msingi ni kwa sisi kufanya kazi kwa bidii na kuzidi kupata mafanikio ktk hii dunia. Mungu awabariki.

    Nashukuru,
    ©2006 MK

    Nota Bene:

    Watanzania tuache tabia mbaya za kutaka kurudisha maendeleo ya watu wengine kwa chuki zenu binafsi.

    Tuishi kwa amani, kupendana na kusaidiana na tunaweza kupata maendeleo mengi makubwa kama mataifa mengine.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...