WABONGO WOTE UGHAIBUNI, HUSUSAN MAREKANI, TUNA MAJONZI MAZITO -PICHANI - KUONDOKEWA NA WAPENDWA WETU WALTER MAZULA (28) NA VONETHA NKYA (27) WALIOUWAWA KIKATILI KWA KUPIGWA RISASI HUKO DETROIT, MICHIGAN WIKIENDI HII.

MIPANGO INAFANYWA KUSAFIRISHA MIILI YA MAREHEMU NYUMBANI. NA JUMUIYA YA WATANZANIA MAREKANI IMEFUNGUA AKAUNTI MAALUMU KWA AJILI YA MICHANGO YA KUWEZESHA USAFIRISHAJI HUO, NA HII HAPA CHINI NDIYO MAELEZO KAMILI JUU YA MCHANGO HUO NA STORI NZIMA KAM A NILIVYOWEZA KUIKUSANYA MIMI


Ndugu Watanzania mnaoishi Atlanta Jumuiya ya Watanzania wenzetu wa Detroit, Michigan inasikitika kutangaza vifo vya watanzania wenzetu wawili: Vonetta Nkya na Walter Mazula.Mipango ya kusafirisha miili ya marehemu bado inapangwa.

Wandugu kama inavyojulikana kwamba gharama za kusafirisha miili nyumbani ni kubwa; tunaomba msaada wako wa hali na mali.

Hapa chini kuna "Bank Account Information"PCS National BankWalter Mazula & Vonetta Nkya Trust FundAccount #: 686-910-1756Routing #: 291-07-0001Kwa wale waishio Atlanta; Ikiwa kwamba unataka kutoa mchango wako bila kutumia hiyo account hapo juu, tafadhali mpigie simu Bashir Chuma @ 404-423-6321Tunatanguliza shukrani zetu za dhati.

Kwa taarifa zaidiBryan Mazula (248) 730-0249Belinda Nkya (443) 600-2135Rahma Baraka (443) 621-1683

MUNGU AZIWEKE ROHO ZA MAREHEMU PAHALA PEMA PEPONI, AMINA

TWO TANZANIANS SLAIN IN DETROIT


From Muhidin Issa Michuzi in New York

Two Tanzanians were shot dead over the weekend by unknown assailants in Detroit, Michigan, and so far no motive of the murder has been established nor suspects apprehended.

Tanzania’s Ambassador to Washington, Mr Andrew Mhando Daraja, confirming the reports here last night named the deceased as the late Walter Mazula and Vonetha Nkya.

Mr Daraja said the two met their violent deaths in the East side of Detroit late Saturday afternoon.

“We have contacted the Detroit police and they have promised to give us a full report on the shooting in two days time.

“What I can tell you at the moment is that the bodies have been released to the family and preparations to fly them home are in top gear”, said the envoy.

He added that an official from Tanzania’s embassy in Washington, Mr Edward Sokoine, has been dispatched to Detroit to offer any assistance needed.

Reports from Detroit have it that the Police department there has offered a 4,000 US Dollar reward to whoever will give information that will lead to the arrest of the perpetrators.

It is suspected that the cold-blooded slaying of the two who are said to have been close friends was pre-arranged. Their bodies were found at two different places.

The reports say that the late Walter was shot five times in the neck and head before his body was thrown at the road side.

It is reported that Vonetha was shot twice in the head and later on the car in which she and Walter were driving was torched, burning her body beyond recognition.

The news of these deaths has hit the Tanzanian community in the US especially hard and most of them expressed profound shock and could not comprehend why it has happened.

They told the Daily News that the deceased were some of the most endearing persons who ran a peaceful life both in the US and back home.

The late Walter who died at the age of 28 had graduated from the Walsh College in Troy, Michigan, according to family sources.

Vonetha was a finalist at the same college and was to graduate in December this year. She was 27.

Their bodies are expected to be flown to Dar es salaam for burial either on Sunday or Monday, depending on the availability of flights.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 73 mpaka sasa

 1. Nimepokea habari hizi kwa masikitiko makubwa sana.Nilikuwa namfahamu vizuri Walter Mazula na alikuwa ni kijana mmoja mpole sana.Kwa niaba ya Radio Butiama nachukua nafasi hii kutoa pole kwa familia za Walter na Vonetha.

  Radio Butiama tumeongelea hili tukio na mnaweza kupitia kupata habari zaidi.

  http://www.butiama.podomatic.com


  Radio Butiama
  http://www.butiama.podomatic.com
  Wasilisha - Fahamisha - Elimisha

  ReplyDelete
 2. Kwa kifupi habari hii inasikitisha sana kwa kweli na pia naomba kuuliza hivi $4000 inatosha kweli? Mbona ukicompare na incidence zingine kama hizi unakuta kwamba they offer more money for anyone with information ambayo kwa kweli inasidia kuhamasisha watu kwenda kutoa information zozote walizonazo. Pamoja na kwamba murder crimes are high in Detriot ila I hope this issue will be taken seriously and justice will be served. Pia nimepata habari kwamba raisi amesema serikali itagaramia usafirishaji wa miili ya marehemu Michuzi unaweza kutupa information zaidi kuhusuiana na hili? May God Almighty rest the souls of Walter and Vonetha in eternal peace.

  ReplyDelete
 3. Mungu aziweke roho za marehemu mahari pema peponi. AMEN

  ReplyDelete
 4. May the Almighty rest their souls in eternal peace. This is very disturbing news. I knew Walter and I know his relatives. May God give them strength in this trying time. Amin

  ReplyDelete
 5. Kwa kweli hili ni jambo la kutisha mno inasikitisha kukatisha maisha ya vijana wadogo ambao ni hazina kwa familia zao.

  Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi - AMEN

  ReplyDelete
 6. REST IN PEACE WALTER AND VONETHA MAY GOD REST U PEACE..

  ReplyDelete
 7. Mungu awalaze kwa amani. Amina.

  ReplyDelete
 8. Mnaweza kuja ku sign kitabu cha rambi rambi hapa:

  http://home.insight.rr.com/duesville/waltermazula.htm

  Radio Butiama
  www.butiama.podomatic.com
  Wasilisha - Fahamisha - Elimisha

  ReplyDelete
 9. Kwa kweli habari hii inasikitisha sana!Ndugu yangu Bryan pole sana tutamisi sikuzote mdogo wetu Walter.Dada Nkya Pole sana.Mungu awajalie nguvu nyingi wakati huu wa masikitiko makubwa.
  Ahsanteni

  ReplyDelete
 10. hii story ni disturbing sana. Binafsi naona hii story haipo sawasawa. there is something missing here. MOTIVE.

  majambazi walikuwa wanataka kuwaua? Kuna beef? Madawa a kulevya?

  ReplyDelete
 11. i am devastasted.i knew walter.i knew vonetha.i cannot even begin to imagine ukatili wa kiasi hiki binadamu tunatoa wapi.anon,i agree.this story is just not right.why would anyone do that to them?

  ReplyDelete
 12. its so sad...may the almight creator rest them into eternal peace....amen

  ReplyDelete
 13. i miss walter and vonetha family friends chilin gymkhana club again huku i love there family i feel for them Brian , gorge stay strong i will always pray for you guys and your family much love from missouri

  ReplyDelete
 14. Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, nilikuwa nawajua ndgu zangu hawa Bryan, George na familia yote, jamani kwa watu wote tunaomjua ndugu yetu walter ni mtu asiye kuwa na kujumuisha na mambo yeyote ya ajabu havuti sigara, hanywi pombe ni mtu wa nyumbani so zaidi ya kuomba mungu polisi waweze kupata chochote tusianze kutoa maneno tofauti
  RIP Walter,Vanneta

  ReplyDelete
 15. May allah rest their soul in peace amen...

  ReplyDelete
 16. Mbelwa kawaua nini? Kuna fununu yuko maeneo ya Chicago.

  Rest in Peace!

  ReplyDelete
 17. Jamani kweli duniani kuna watu wasio na roho kabisa, wanawaua ndugu zetu wanaojishughulisha na maisha yao na kwenda shule kujiendeleza zaidi then dreams zote zinafutwa kwa upuuzi, Mungu uwe na ndugu wote wakati wa wakati huu mgumu, Amen

  ReplyDelete
 18. Ni msiba mzito kwa watanzania wote.Mungu azilaze pema peponi roho zao na kuwapa nguvu ndugu,jamaa na marafiki popote walipo.

  ReplyDelete
 19. GOD BE WITH ALL THE RELATIVES AT THIS HARD TIMES THAT THEY ARE GOING THROUGH.

  Jamani ndugu zangu kweli ni huzuni kwa kutokwa kwa ndugu zetu hawa tuliokuwa nao tokea Olympio, Uganda na huku Detroit we cry for both of you. Its scary lakini hapohapo inanifanya niwaze kwamba kwa sisi tulio huku na ubalozi wetu inabidi tuwaweke hawa polisi wa huku kwenye kona na tuwaulizie juu ya maendeleo ya kesi hii kwa sababu ninavyojua mimi ukiwa na mweusi na juu ya hilo muafrika hawa watu wako very quick kuiweka hizi kesi kwenye kapu la cold cases.

  Kwa ninachojua japo motives hakuna kwa sasa kwa sababu Walter na fiancee wake hawakua na maadui wanaojulikana, lakini kuna mtu aliipokea simu ya marehemu kabla haijajulikana kikamili kilichotokea, kitu ambacho kinawezesha kuanzia investigation so kwa ubalozi na sisi wote wa huku tunaoweza tusiiache hii kesi iende hivihivi tufanye kwa wapendwa wetu angalau kuwe na mtu atakaye wekwa ndani for this.
  RIP Walter & Vonetha
  pEACE

  ReplyDelete
 20. Mungu awalaze mahali pema Mbinguni. Amen.

  Jamani nani kawaua kikatili hivyo? Kisa ni nini jamani? Navyofahamu huko Detroit kuna crime sana kushinda sehemu zingine USA. Lakini kisa cha kumpiga mtu risasi tano kichwani na kuchoma moto maiti? Hayo mauji si ya kawaida na ni gangland style. Tuombe polisi na FBI watafanya kazi yao na muaji au wauaji watakamtwa.

  Pole sana kwa familia za Mzee Nkya na Captain Mazula.

  ReplyDelete
 21. Folks, you shouldn't forget that these tragic double murders happened in the USA where of all Americans, the life of Blacks (leave alone Africans) is still relatively cheap.

  Thus there's a pretty good chance that this case would go unsolved simply because the victims racial background is African. Furthermore, too many people of African descent get murdered every week in Detroit (and indeed in most major cities in America) for the Detroit Police Dept. to give to give priority to Black vs Black homicides. On the other hand, had the victims here been White, then you would be doggone sure that the cops would have already found suspect(s), and the story would have been all over TV networks and on cyberspace.

  PS: As per today, there's not a single independent news source on the internet that has written about the story: not even from the website of Detroit Police Dept.

  ReplyDelete
 22. Anony Mbaya,

  Ni kweli kabisa kuwa maisha ya mtu mweusi hapa USA haina thamani ukilinganisha na wazungu. Hata hapa Boston mweusi akiuawa ni bahati kusikia habari kwenye TV au kwenye gazeti. Lakini mzungu akiuwawa utasikia kwa siku kadhaa na miaka! Au ua mbwa au paka habari itakuwa kwenye TV na magazetini. Kwa kweli kama tunataka Polisi wa 'solve' hayo mauaji itabidi serikali ya Tanzania na ubalozi zetu zifuatilie kwa makini. La sivyo itakuwa ' JUST ANOTHER COLD CASE!'

  ReplyDelete
 23. Lakini si mlijua toka zamani kuwa nchi kama USA, UK, France, Holland, Belgium, Italy, Spain,n.k
  Kote kule kwenye more than 3rd generation black peoples and immigrates ujue ni nchi ya holliday tu! Ni afadhali NIRUDI KWETU BONGO!!! Ni wakatili tu! Mmeng'ang'ania jina na uoga wa kuanza mwanzo hata wapopo na waarab wanawashinda. Mnateswa na kuuliwa kama kuku hamsemi ukweli tu!
  Wewe nchi gani developed kama huna kazi au shule basi ushakuwa masini, mpaka utafute hela kama bongo. Greencard kutoa kwa kaya, wakati kila binadamu anayeingia nchini appart from a turist, hata kama huna ID, lazima upate matibabu ya bure, elimu, makazi na mshahara kwanza kabla ya yote!
  Huko mpaka mfight, poleni sana ndio maana mnaishia kusafisha, na kuuza.....au......

  ReplyDelete
 24. wee Hapo juu hebu acha PUMBA zako sasa aaah.....
  watu wako kwenye maombolezo wewe unaanza kuongea nonsense.Kama huna la kusema then nyamaza.
  RIP Walter and Vonneta.

  ReplyDelete
 25. Kuwa msibani hakuna maana ya kwamba watu wasiambiane ukweli.Ukweli ni kwamba maisha ya mtu mweusi Marekani yanasikitisha.Ray Kapalata ameuawa,muuaji wake tunasikia bado yupo Marekani.The case is already cold! Hawa ndugu zetu kina Walter na Vonneta nao itakuwa hivyo hivyo,dalili zishaanza kuonekana.

  ReplyDelete
 26. Jamani mi nawaomba ndugu zanguni wabongo najua tunaweza kuwa na feelings tofauti kutokana na tulivyokuwa tunawajua hawa ndugu zetu na hivyo kuguswa kwa level tofauti, lakini naombeni hata kwa nyie mliokuwa hamumjui au hamjaguswa sana na msiba huu jamani tuachane na mawazo na kukosoana na kurushiana maneno ndugu na tulio karibu tunaingia huku na kweli inauma kuona kwamba kuna mtu ataanza kusema na kutoa maneno yasio ya maombolezi.
  Kama mmoja wa watu walio karibu na Brian na familia yote nawaombeni toeni pole lakini maoni jamani sio wakati wake

  ReplyDelete
 27. poleni wote mnaousika na msiba huu mimi naishi cape town nimeguswa sana na wa tanzania wenzetu RIP both
  capetonian

  ReplyDelete
 28. Nakubaliana na anony wa 9.46am. Jamani, tafadhalini kama hamna cha maana cha kuongea basi bora mnyamaze. Huu msiba umegusa wengi na kwa level tofauti na bado watu tuna majonzi sana, sasa basi hayo mambo ya maisha ya mtu mweusi bla bla bla sio wakati wake huu. Tuheshimu familia za marehemu na ndugu, marafiki na wote walioguswa na msiba huu. Asanteni.
  R.I.P Walter and Vonetha

  ReplyDelete
 29. Poleni sana sana !! Jambo la kinyama sana Thanks Michuzi kwa taharifa - toka East sussex UK

  ReplyDelete
 30. Daima, watu wanaheshimu familia ya marehemu. Kwa hiyo una maana wamekwisha kufa hivyo basi tena hao waliyowaua waachiwe? Watu wasipofuatilia kipindi hiki ni kweli itakuwa cold case na wataua wengine. Wabongo wanatakiwa waandamane Detroit polisi na ku-demand hao wauaji wakamatwe.

  ReplyDelete
 31. INNA LILLAH WAINNA ILLAH RAJIUNA.
  MBELE YAO NYUMA Yetu TUNAWAFUATA.AWE MWENYEZI MUNGU WAJAALIE MAPUMZIKO MEMA PEPONI AMINA.

  ReplyDelete
 32. Mnaweza kuja hapa ku sign kitabu cha rambi rambi.

  http://home.insight.rr.com/duesville/waltermazula.htm

  Radio Butiama
  www.butiama.podomatic.com

  ReplyDelete
 33. Of course I want whoever did this to be brought to justice. I guess hukunielewa, kuna mtu hapo juu ambaye anaongelea mambo ya watu tuko huku tunaonewa hatutaki kusema and whatnot ( have no time to repeat what he/she said). For that ndio nasema kuwa wakati huu hizo habari si muhimu yameshatokea sasa. Kuhusu kufuatilia muuaji/wauaji hawa, hiyo no doubt. Walter was a friend and I have been deeply touched by this tragedy.

  ReplyDelete
 34. DUUUUU!!!HUU NI MSIBA WA TAIFA ZIMA LA TANZANIA BARA NA VISIWANI.
  POLENI SANA FAMILIA ZA MAREHEMU HAWA,NA POLENI SANA KWA WATANZANIA WENZANGU POTE MLIKO.

  KESI HII NILAZIMA IFUATILIWE KWA KARIBU ZAIDI.KWANI HATUJUI CHANZO NI NINI NA NANI KAHUSIKA NA MAUAJI HAYA YA KIKATILI.

  KWANZA NAOMBA FAMILIA YA MAREHEMU ITOE RUHUSA YAKUENDELEA NA UCHUNGUZI HUU.

  MIILI YA MAREHEMU NI LAZIMA ICHUNGUZWE NA TUPATE ALAMA ZA VIDOLE(FINGER PRINTS) ZA WAHUSIKA.
  KISHA ZIINGIZWE KWENYE DATABASE KISHA TUTAJUA NI NANI.

  PILI:TUPATE CAMERA RECORDS YA SAFARI ZA HILO GARI KATIKA MITAA YOTE YA DETROIT.

  TATU:CREDIT CARDS ZA MAREHEMU ALIZITUMIA WAPI???WEEK MOJA ILIYOPITA KABRA HAWAJAFARIKI.

  NNE:TELEPHONE RECORDS ZA MAREHEMU WOTE NILAZIMA ZIPATIKANE WEEK MOJA KABRA YA KUFARIKI

  TANO:MTANDAO WA MAREHEMU NILAZIMA UCHUNGUZWE KWA KARIBU ZAIDI.

  SITA:BANK STATEMENTS ZA MAREHEMU NILAZIMA ZICHUNGUZWE.KAMWANDIKIA NANI CHECKS ???NA NIKWA AJILI YA NINI???

  SABA:CREDIT REPORT ZA MAREHEMU NI NANI ANAWADAI ?????

  NANE:POLISI WA DETROIT NI LAZIMA WATOE TAARIFA KAMA MAREHEMU WALIKWISHA TOA MALALAMIKO YA AINA YOYOTE.(POLICE REPORT)

  TISA:WATANZANIA WOTE DUNIANI TUCHANGE PESA ILI TUMWAJILI DR. HENRY C. LEE NI MTAALAMU DUNIANI WA KUFUATILIA KESI ZA AINA HII.

  MWISHO-NASIKITIKA SANA KWA KURUDIA KUZIANGALIA PICHA ZA MAREHEMU WAKIWA PAMOJA.POLENI SANA FAMILIA YA MAREHEMU WOTE NA MUNGU ATAZILAZA MAHARI PEMA -AMENI

  ReplyDelete
 35. Aliyosema Mr. Fumbuka ni ya kweli kabisa. Familia za marehemu zifuatilie kwa makini na pia wa-contact vyombo vya habari USA. Great Van Susteren (japo anapenda kesi za wazungu blonde and blue eyes). Pia tuchange pesa za kuongeza Rewards za kukamatwa kwa hao walioua akina Walter. Ama kweli tuna majonzi kwa vifo vya Walter na Vonetha.

  Na pia Reward ya Kumkamata Mbelwa aliyemwua Ray Kapalata. Mbelwa bado anakata mitaa ya USA kwa vile polisi hawajali.

  ReplyDelete
 36. Poleni Ndugu, Marafiki, Watanzania mlioko Ughaibuni, na wengine walioko Nyumbani.
  Mungu atawapa nguvu na moyo, pia ataziweka roho za marehemu mahali pema.
  Wavuvi wote tumestushwa na hizi habari.

  ReplyDelete
 37. Asanteni sana watu wote mliochukua muda wenu na kutoa maoni na pole kwetu, kama rafiki wa karibu wa Brian,Walter,George na familia ya Nkya natoa shukhurani kwa niaba zao.
  Mbili we all hope kwamba polisi na wapelelezi wa DPD watafuatilia hii issue na sisi huku tunaahidi kukaa nao kwa karibu na kutoa ushirikiano wote wanaoitaji juu ya info za marehemu, kwa sasa tunatoa nguvu zetu zote kwa shughuli na maandalizi ya kusafirisha hii miili yao ikiwezekana this weekend ili wazazi na familia zao wote wapate nafasi ya kuwapumzisha wapendwa wao.
  Kwa wale mnaotaka na wenye uwezo wa kusaidia katika shughuli hii tunawaomba mfanye hivyo kwa kutumia connection iliyotolewa hapo juu na kwa maswali yoyote au info zaidi please dont hesitate kupiga hizo simu zilizotolewa hapo juu
  Kwa mara nyingine asanteni sana. pEACE
  RIP Walter na Vonetha

  ReplyDelete
 38. poleni sana ndugu zanguni

  ReplyDelete
 39. wabongo mmejawa na umbeya sana tunaomboleza msiba wa ndugu zetu sasa wewe sijui alexander fumbuka ghafla umekuwa fbi unaanza kuelekeza kazi zao mmeambiwa msubili mtapata lipoti hivi karibuni lakini mmeanza umbeya.tulinza mboro tutapata riport soon.

  ReplyDelete
 40. I dont know them but it seems they were very good people.

  May Almight God rest their souls in peace.

  ReplyDelete
 41. Poleni.

  Hivi ni kweli daily news inavyosema kuwa ni separate incidents?
  http://www.dailynews-tsn.com/page.php?id=3645

  ReplyDelete
 42. Bwana ametoa , na Bwana ametwaa.Mungu awalaze pema peponi.Amen

  ReplyDelete
 43. tafadhali ndugu Kabada Kadinda toa maoni yako lakini matusi huu si wakati wake na huu msiba si mahali pake kabisaa, kama una hamu sana ya kutukana subiri itakapokuja midahalo inayostahili. hbnlaw

  ReplyDelete
 44. we kabada unapenda sana kubadilisga watu wanchofuatilia na kiswahili chako cha (lipoti,msubili), kajifunze kwanza sehemu za kutumia r na l then njoo wakati mwingine, usianze matusi sasa hivi

  ReplyDelete
 45. Nipigo kwa taifa kwani ndio tu vijana walikuwa wamechipukia.Walaaniwe hao waliofanya mauaji ya kinyama.Mpumzike kwa amni wapendwa wetu......AMIN

  ReplyDelete
 46. Mnaweza kupitia kwenye hii site ya msiba kupata habari zaidi kuhusiana na mipango ya kusafirisha miili.Pia mnaweza kuona ratiba ya Ijumaa na Jumamosi.


  http://home.insight.rr.com/duesville/waltermazula.htm

  Radio Butiama tunaenda Michigan siku ya Ijumaa na tutawaletea habari zaidi.

  shukran

  Radio Butiama
  www.butiama.podomatic.com
  Wasilisha - Fahamisha - Elimisha

  ReplyDelete
 47. Hii habari inasikitisha sana ukizingatia jinsi hawa majangili yalivyo fanya kikatili. Na vilevile najua watu wako na wasiwasi na hawa jamaa wa polisi lakini ukweli ni kwamba mimi nitawaamini hawa kuliko wapelelezi wetu wa bongo, japo wanakuwa slow kwenye kesi za weusi lakini sio kwamba hawafatilii kabisa na hii issue sio kweli kwamba haiko kwenye TVs, huku Detroit wanaiongelea kwenye TV na wamekuja na kuongea na mzee Ayubu ambaye ndie mzungumzaji wa familia na wanaonyesha hiyo.

  Kwa hiyo mi naomba tuwape muda na kuwa na moyo kwamba hawa watu watakamatwa kama ndugu yangu hapo juu alivyosema muda huu tushughulike na kuhakikisha ndugu zetu wanapata kurudi nyumba kuzikwa

  ReplyDelete
 48. Brayan,Belinda polenisana katika kipindi hiki kigumu kwenu kwa kufiwa na watu wakaribu kiasi hiki.May God rest them in Peace,AMIN!!!

  ReplyDelete
 49. Hii Habari inasikitisha,maisha ya weusi huko Marekani inaonekana ni hatari sana,kifo mkononi,mmh inaonekana kuna bado ubaguzi mwingi,labda bora nchi zingine za Ulaya,kama Ulaya ya Kaskazini,Mungu azilaze mahali pema peponi roho za marehemu!
  Mengi yamesemwa machache yametendeka

  ReplyDelete
 50. haina maana kama kauwawa kwa sababu ni mweusi tuache kujiingiza kwenye maneno hayo kila siku watu wanauwawa huku weusi kwa weupe so please
  Chanzo hatukijui tuache kuanza maneno. Kama bongo ilivyo kuna mtu anauwawa na majambazi karibu kila siku na si wote ni weusi so wewe ulaya ndio nini

  ReplyDelete
 51. JACK PEMBA HUU NDIYO WAKATI MUAFAKA WA WEWE KUSAIDIA SIYO UNAMWAGA DOLLAR KWA MISS TANZANIA KWA SABABU UNATAKA URODA SAIDIA HATA KWENYE MISIBA KAMA KWELI WEWE NI MTU WA KUSAIDIA NA UNAJIDAI NI MPENDA WATANZANIA.

  ReplyDelete
 52. Kila nikiliwaza jambo hili linanitia simanzi nisiyoweza kuielezea. Namuomba Mwenyezi Mungu awawezeshe kwa kila namna wazazi, ndugu, jamaa, marafiki na wengineo wote wanaoguswa na tukio hili la kuhuzunisha kuwa na nguvu ya kulikabili.

  Mungu Awalaze Marehemu Pahala Pema Peponi, Amen.

  Ni miye maridhiya,
  F MtiMkubwa Tungaraza.

  ReplyDelete
 53. Yaani huko Marekani hakujabadika tu tokea nilivyotoka huko miaka 15 iliyopita? Duh! Poleni sana, nitafia Scandinavia mimi au Europe yeyote ile.

  ReplyDelete
 54. Sorry to hear the sad news . I convey my condolence to the whole family and friends. This is great loss for you personally and for everybody who knows them in a great way. Now what to do is to cherish their memories forever. May God remember their souls to his Kingdom. Amen.

  With best wishes,
  ©2006 MK

  ReplyDelete
 55. Boss - you will be truely missed. Your smile got me through the day. Thank you for all your kind words. All your worries are now gone and you two can enjoy peace together. My heart goes out to both your families and friends. I am so sorry for all that has happened. May God keep both of you safe now.

  ReplyDelete
 56. Muaji Mohamed Mustapha Mbelwa alikuwa na bifu na marehemu Mazula tokea Texas. Mbelwa ni mshabiki wa ile sinema ya kikatili SCARFACE. Mle kuna kupiga watu risasi nyingi kuchoma moto maiti na kuchoma watu visu. Mtafute huyo Mbelwa.

  ReplyDelete
 57. JAMANI KAMA HAMNA CHA KUONGEA ACHENI KUONGEA UJINGA....SASA MBELWA KAFANAY NINI HAPA TUNAMWOMBEA MAREHEMU MTANZANIA MWENZETU WENGINE MNALETA UTANI...WATANZANIA ATUTAENDLEA KWA MAMBO KAMA HAYA NDIO MAANA NCHI INAZIDI KUWA MASKINI KWA AJILI YA WATU KAMA NYINYI MLIOZALIWA CHOONI...R.I.P WALTER!! WE GOONA MISS YOU

  ReplyDelete
 58. ANONYMOUS WA 2:12Am - Una maana Mbelwa asiwe suspect? Keshaua na anaweza kuua tena. Staili zake ni za kikatili halafu Detroit ni karibu na Chicago. Lazima awe suspect.

  ReplyDelete
 59. Kama wanayosema watu kwamba mbelwa yuko Chi ni ya ukweli kwa nini sasa mnazungumzia huku kwenye blogs wka nni hamuendi polisi kuripoti issue kubwa kaama hizi huyu ni suspect wa mauaji kama unajua kitu toa taarifa na acha kuzungumzia huku kila siku.

  Na kwa watu wa Chi kweli kama kuna mtu anajua kwamba huyu jamaa ameua na yupo mitaani tu mtakuwa watu wa ajabu sana huna haja ya kutaja jina lako kwa polisi wewe ripoti alipo na ingia mitini acha kukaa na wauaji mpaka aje kuua tena ndio mtajua kwamba mnacheza na moto. Mi nawaomba watanzania wote tumalize hii issue ya msiba iliyo mbele kwetu na baada ya hapo kweli tukae kuhakikisha hawa watu walio fanya hivi wanapatikana na kumbuka kama unamweka muuaji na wewe una kesi yu kumlinda murderer so toa taarifa sasa b4 its too late

  ReplyDelete
 60. Nyinyi mlioko huko USA mnatushangaza kidogo tulio huku nyumbani, mnapenda kuongelea juu ya Mbelwa kila wakati lakini hatuoni nini mnafanya kumsaidia mwenzenu akijerekebishe na kujirudi. Jitahidini kuwa WAMOJA na kuhakikisha kuwa WAUWAJI wa hawa vijana wetu wanapatikana, na kama mnatiliana mashaka wenyewe basi tupeni taarifa zaidi ili tupate kushughulikia jambo hili mapema na kama mnashindwa basi tumieni ubalozi kusaidia katika swala hili. Kumbukeni kuwa mpo ugenini na mara zote huko wageni hawathaminiwi kama huku kwetu ambako hata wakiibiwa na vijana wa huku tunasikitika na huwa tunahakikisha wanaishi salama. Asanteni.
  RIP Walter&Vonetha

  ReplyDelete
 61. Polisi watakuwa huko kwenye Calendar Party.

  ReplyDelete
 62. jamani kama kweli kuna mtu anayejua muuaji atoe taarifa mapema ili atua za kisheria zichukuliwe mapema wabongo maneno mengi action hakuna

  ReplyDelete
 63. munaomba mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi amini usuamini mtu aliyefanya hivi adhamu yake ataipata hapa hapa duniani kabla hajafa
  mshahara wa dhambi ni mauti
  dear god rest their soul in peace

  ReplyDelete
 64. watu wengine hawana akili kabisa yaani nyie mnaona huu ni muda wa kufanya jokes kweli?watu wakaribu na msiba huu tunaomba saaana tena saana muache mambo ya sijui mbelwa sijui nani,kwani kama anon alivyosema hapo juu kama mnajua huyo mbelwa aliko na nyinyi mna uchungu kiasi hicho,simnajua hatua gani za kuchukua jamani.

  sisi hapa tuna deal na issue yetu na tunaomba tafadhali mjue huu sio muda wa utani utani.natanguliza shukurani zangu za dhati kwa wale wote walioweza kutusaidia kwa chochote kile walichonacho.

  MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI.......AMEN.

  ReplyDelete
 65. jacky pemba tunasubiri mchango wako
  rest in peace mr n mrs mazula!

  ReplyDelete
 66. kuna mijitu nyoko humu!nawakemea katika jina la bwana MSHINDWE!

  ReplyDelete
 67. Si vema jamani kutajana majina kwa ajili ya kutoa michango.Mathalani kumtaja Jack Pemba si kitendo cha kiungwana kwani kila mtu anatoa kwa wakati wake kulingana na kipato chake.Asanteni

  ReplyDelete
 68. Anony 5:22, hebu fafanua hiyo mijitu ishindwe kwa jina la BWANA gani?

  ReplyDelete
 69. Tabia za baadhi ya wanadamu wa Tanzania hazibadiliki.Secondary schools zote nilizosoma, ilikuwa UMEME UKIKATIKA KUKAWA GIZA, kila mtu anakuwa anonymous...... SI MATUSI na LUGHA CHAFU!!!!!! Nilidhani ni UTOTO!!! Naona tabia hii ipo hata kwa watu wazima kwenye hii blogg kisa ANONYMOUS!!!sema sasa sijui ni utoto pia,au ni UPUMBAVU.

  ReplyDelete
 70. wewe hapo juu ndio mtoto na nina hakika ukikua utaacha....

  ReplyDelete
 71. nilikuwa napitia hizi comments asilimia kubwa ni watu mnaoishi nje ya nchi ndo mmetoa maoni,kwani huku blog haijulikana sana,hakika mlioko nje wachache wanaelewa nini wanafanya huko,lakini wengine vichwa ni maboksi hakuna kitu ni bangi,pombe starehe ndo maana mnashindwa hata kurudi bongo,msione aibu kurudi wenzenu tunapiga bao huku,mmebakia kuandika upuuzi kuliko vitu vya maana hadi maadili mliyokuwa nayo kabla hamjaenda majuu yamepotea mrudi tujenge nchi nasikia wengine mnaishia kuuza drugs na kufanya pati,kama hamna kitu nitawaajili muishi kwa amani mpate hela,ughaibuni muwe mnaenda kutalii,na siyo kuosha sahani kwenye migahawa na kazi za kipuuzi ambazo huku bongo hamkuwahi kufanya....mtaishia kuuawa kila siku,rudini nyumbani mjenge nchi,wengi wenu hata kusoma hamsomi.poleni sana.

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...