wadau, mnazungumziaje tupamba'katjshuo' twa bongo...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 45 mpaka sasa

  1. HEHEHEHEEEEEEEEEEEEE!

    ReplyDelete
  2. Mabuti na joto hayo, miguu inakuaje

    ReplyDelete
  3. pamoja na kuwapenda sana wanawake wa kitanzania na kuwapa sifa juu ya uzuri wao asili (the best in Africa by far), nasikitika sana jinsi wanavyoiga kila kitu Western... Yani wanawake wamepoteza values etc, na kila kitu lazima waige, kuanzia mavazi mpaka tabia. Madada zetu nashauri muige tabia na mambo mengineyo mazuri ya kigeni, na muachane na yale ambayo si mazuri. Na hamna haja ya kutuvalia uchi, mjiheshimu, you are more valuable than that....

    ReplyDelete
  4. mabuti kweli bongo sio kwenyewe....ila nimezia huyo mwenye white with gold stuffs

    ReplyDelete
  5. bongo bwana ukishika handbag club ....changu!!! si hivyo ndugu zanguni nyie ni mabinti lolote laweza tokea ukizingatia hasa na vijitambaa hivyo mlivyoviaa basi tia hata ka jitambaa kadogo na vikolokolo vingine mnavijua huyo mwenye gold ndie anajua maana halisi ya uanamke.

    ReplyDelete
  6. hehehe hahaha! michuzi usituchekeshe tuliojinunia leo....
    hhahahaaha! Bongo bwana.

    ReplyDelete
  7. well, hawa wadada wamependeza ila ndio hiyo mambo ya made in China by a designer named ChiChin..lol. Nguo hizo zinaunguza hata kama nyepesi kiasi gani...

    Wachina wanaleta vitu havina viwango. Watu wanavikimbilia ati ni cheap kumbe zinakuja kuleta madhara kwenye ngozi, kuanzia vipodozi, macheap perfumes, viatu (mnaota vigimbi na cons cos havina viwango)..

    Vipodozi vya China ukivisoma utaona wamekoseakosea, oh zis (this) ploduct(product) wirr(will) make your snik (skin) white..Nani anataka skin yake iwe white, yani kama karatasi ama?

    Jamani quality jama..Bora ununue second hand clothes za Gucci,Ralph Lauren kuliko kama hizo walizovaa hao wadada...Ohooo

    ReplyDelete
  8. binadamu kazi yake kutia kasoro vitu, wakivaa vizuri wanaringa wakivaa nguo rahisi wanasemwa sasa watembee uchi ? ndio mfurahi kila mtu anachaguo na nyie pia nachaguo lenu.

    ReplyDelete
  9. Watanzania mnaoishi ughaibuni acheni ushamba, mmeondoka huku kwenda beba maboski na kulea vizee mkiacha bibi zenu wakiomba, then mnaanza kudharau hali ya huku... wewe anony wa saa tano na dakika hamsini na saba.... bongo ndiko kuliko kukuza, unajua hali ilivyo kimaisha.. baada ya kubahatika kuzamia basi unaona kila kilichopo huku ni below quality.. pole sana. Kwanza binadamu ukienda huko ukaingia majina yenye maduka kununulia nduguzo vijizawadi utasikia... mbona unaenda kufanya shopping maduka very expensive... nawasikitikia sana..

    ReplyDelete
  10. Jamani eeeeee chondechonde, kumbe akina dada wabongo ndio wakiwa shoo wanakuwa hivyo, ndio maana vigimbi haviwaishi jamani duh, michuchumio yenyewe mibayaa, halafu hapo kaja kwa daladala katembea kimwendo kufikia kituo cha basi, matokeo yake haviwi vigimbi tena vinakauka kama vijimihogo vile! miguu inaharibikaa hiyo jamani. Akina dada wazuri ila mivao hopeless! ah bwana mie mwniudhiiiiii

    ReplyDelete
  11. Jamani msiwalaumu sana wengine wanaletewa zawadi na ndugu zao (Mabuti) walioko kwenye nchi za baridi sasa wakavalie wapi hivyo vitu, wa kulaumiwa na wanaotuma zawadi bila kujali hali ya hewa ya bongo (kama masweta, mabuti n.k)

    ReplyDelete
  12. Bwana michuzi nimekubali na hao madada wa bongo kwani mimi sio " a hater" au vipi? lakini swali langu ni kwamba je WAMEOGA? kwani nasikia huko kwenu hakuna maji? na kama wameoga je WAMEPIGA PASI?

    ReplyDelete
  13. Mijitu mingine bwana eti huko kwenu...wabongo...Nchi hizo kila siku nyie second classs citizen forever. Leo huko kwenu....wewe unaeuliza wameogo ulikua huogi ulivyokua boongo basi unafikiri kila mtu kama wewe. Kama wewe ulikulia kwenye shida ndio maana ukakimbia bongo usifikiri kila mtu basi life yake ni hivyo
    Acha kuwaonea wasichan wa watu wivu kwa vile wanaishi stress free life. Mbona wako kwenye catalog tu. Kwani party za TX si tunaenda kila siku? Lipi jipya, lipi tofauti a unaloona hapa???? Acheni wivu ....mko bored, hamna mtu wa kuongea naye mpaka time zako za kwenda kupiga another double shift sasa unaona kwa michuzi ndo mahali pa wewe hata uongee kwasababu hapo uliko na kazi yako inaelekea hata huna sauti.....

    ReplyDelete
  14. Hongera dada zangu!Tumetoka mbali sisi watanzania.Hapo ukitazama ni kama sehemu zote zingine za duniani,kama vile New York,Kingston,miami,london au brazil.The world is closing in.Big up yourselves my sisters,Fresh vegetables ti the max!!

    ReplyDelete
  15. SHENZI TYPE KABISA NYIE MNAOWASAGIA HAO WADADA.... KWANZA MIE NIWAPONGEZE KWA KUPENDEZA WHETHER NI NGUO ZA WACHINA AU HAO MADESIGNER MNAOWAFAGILIA HAPO JUU.

    MIMI NIKO HUKU UGHAIBUBI ILA KUSEMA KWELI HAO WADADA WANAPENDEZA.. HII DUNIA KILA MTU ANAIGA NA KAMA UNAIGA NA UNAPENDEZA MWAKEEEE!!!! ILA UKIWAWEKA NA WALE WA DALAS MICHUZI UNAWAKUMBUKA WALIKUWA WAMEAUKAAAAAAAAA NA KUCHOKAAAAAAA MPAKA PICHA YAO ILIKUWA INATOA HARUFUUUUU... NYIE KINA DADA MWAEGO MMEPENDEZA.. KEEP IT UP BONGO

    ReplyDelete
  16. WABONGO hacheni mambo ya kinafiki..mbona mnawasaga hawa wakina dada bure watoto wamependeza ile mbaya nisinge anza kusoma ningedhania ma- mtoni siyo well done Tanzanian girl for being up to date. hachana na washamba fulani wanaojidai eti wako mtoni. huku mtoni watanzania wangapi wanaingia kwenye maduka aliyo yataja jamaa mmoja hapo juu GUCCI. FENDI .DG ,LV e.t.c bei za umo unazijua au unadhania ni mambo ya longo longo za kibongo umo wanaenda watu wa class fulani mmsiwasikilize hao jamaa walioko ughaibuni mie napanda ndege nao sioni pamba ya maana walizovaa... hata huku ughaibuni nguo nyingi sizinatengenezwa china kwasababu ya cheap labour kwahiyo viwanda vyote vya kimarekani vinasalisha vitu china huyu anayesaga eti nguo za china zimejaa bongo huko mtoni zinatoka wapi??????? yaani watu na kukaa nje bado mna mambo ya kienyeji ohoo wanavaa uchi... sasa huku mtoni hutasemaje watu wanatembea na bikini
    Halafu jamani hacheni tabia ya kusagia watu walio baki nyumbani sie tupo huku lakini ni game of chance na ushukuru mungu siyo iwe kigezo cha kusagia watu na kuwadharau .nitashukuru kama educated people tutajirudi kidogo ...
    DOCTOR.//

    ReplyDelete
  17. Utakuta mademu hao wote kwenye picha pamoja na kupendeza kwa mavazi yao mazuri lakini bado wananuka VIKWAPA. Hapo inabidi uende umevaa Mask kupunguza harufu kali za VIKWAPA vyao.

    ReplyDelete
  18. Viatu vya baridi nchi ya joto? hee acheni kutetea ushamba jamani.
    Usisahau nywele za kupandika na jua la bongo 30C, nywele halali zote hunyonyoka utafikiria wametumia zazuu!
    dada zetu waliovaa nguo za wazi wamependeza sio hao wengine!

    Hapana urembo huu!

    ReplyDelete
  19. LOL....maanonymous wengi huko juu mwafurahisha...mara haaogi....usiniambie nduguzo (dada zako) uliowaaha huku wanakwambiaga hawaogi.

    China...hata hao madesgner wana viwanda china....na ndo china wanatoa copy na watu tunatoka.

    michuzi kumaliza ubishi tuwekee picha hapa ya wadada wa bongo na wa huko ulaya......wanapopaona mbinguni... wakati watu tuna kazi ya kuwanunua vitu na kuwaagizishia huko huko waliko....na madesgner wapishana nao...msonyoooooooooooo

    ReplyDelete
  20. Yaani, napenda sana wale waliosupport nchi yetu. Wewe hata kama uko ughaibuni na makaratasi au bila makaratasi TANZANIA BADO NI KWENU. Naomba tukumbuke hilo. Kusagia nyumbani haikufanyi uwe bora zaidi. Maisha ni popote lakini HOME IS THE BEST. Tuwe wazalendo jamani, tafadhalini sana. Huko majuu watu wangapi wanaweza kwenda kwenye designer shops? Wachache au kama hamna kabisaaa UK, watu wanaishia 'Primark" na US mnaishia 'Ross - Dress For less', halafu mnazungumzia designers! Wabongo tuko home lakini maisha yenu tunayajua....msitudanganye. Mtabeba maboksi na wazee na kutukanwa na wazungu milele...Kisa unakaa kwenye apartment yenye AC na kuendesha gari la mtumba. MR II aliimba 'Bongo New York' sio lazima ukabebe boksi ulaya ndio uwe na maisha mazuri.......na nyumbani ni nyumbani tu......MSIENDEKEZE UTUMWA WA KISASA!11AMKENI NA MKUMBUKE KWENU NA WAZAZI WENU WANAOLALA NA NJAA WAKATI MKIVINJARI NA VIDOLLAR/VIPAUNDI VYENU AMBAVYO HAMUWEZI HATA KUSAVE. UZALENDO MUHIMU...UZALEENDO JAMANI......KAENI CHINI MFIKIRI!HAMNA KISICHOKUWEPO BONGO, KUANZIA MAVAZI, MAGARI MPAKA NYUMBA ZA KIFAHARI.....USILINGANISHE MAISHA YENU YA TANDIKA SOKONI NA APPARTMENT YA USWAZI HUKO UGHAIBUNI HALAFU UNAJIONA UMEWIN, MAISHA BADO............UZALENDO.....UZALENDO JAMANI. AKILI KICHWANI, BEBA BOKSI MILELE, KUWA MTUMWA NA KUCHUKIA KWENU AU UJIJENGE NA UENDELEZE KWENU! CHAGUO LAKO

    ReplyDelete
  21. Shamim, you are very right sister, mdharau kwao mtumwa... eti wako majuu, majuu nini hawana kitu wapumbavu hawa, kwanza utakuta hata majina yao asili wamebadilisha ili wapate uraia, still they will always be second class citizens. Hilo hawajui, ukute hao wanaosiliba ndio walioshindwa maisha ya amani huku na kukimbilia kuuza utu wao kwenye nchi za watu. Tena nikisema kuuza utu I mean UTU in capital letters, pumbavu kabisa.....mnaishia kuwekwa ndani baada ya kushindwa kutengeneza a decent living na kuishia kuwa majambazi wa pesa na vifaa vya watu. Bongo muiite mnavyotaka lakini bado it is the most peaceful country. Nitaendelea kuwaita Wapumbavu ambao wanafikiri Marks and Spencer's wanauza bidhaa zilizotengenezwa Marekani na Uingereza.

    ReplyDelete
  22. Kwa taarifa yako anonymous unaesema niko ugaibuni kama ulivyopaita, wala sipo huko..Niko Bongo hii hii na naenda nje ya nchi kutembea tu, wala sina mpango wa kuishi kubeba maboksi..Sawa?

    Na niko very informed na msikilizage BBC Focus on Africa,etc..Wachina wanatengeneza very high quality as well as very poor quality goods...Hizo zenye viwango vidogo ndio wanazileta Africa..Zile zenye viwango vikubwa ndio wanatengeneza (cheap labor) kwa ajili ya developed world, na ndio hapo unakuta kaTshirt ka DKNY or GAP,etc kameandikwa made in China, lakini ina kiwango...

    Ishu ni kwamba, muelewe kuwa wadada hawa ndio wamependeza ila nimeongelea quality ya nguo hizo cos najua what's goin on in our country, africa in general na hata huko mnakokuita ugaibuni...Ni mambo ya exposure tu...Acha kubwata bila kuelewa points wanazotoa watu..

    Lmao kwa anony ulosema wanatembea na michuchumio na wananuka vijasho..that is very true indeed..Lmaoooooooo!

    Na wewe anony unaelekea ni mnyakyusha eti hacheni, hutasemaje..Hukusoma shule ya awali nini wewe...

    ReplyDelete
  23. hahaha, heri ya mshamba anaweza kubadilika, kuliko LIMBUKENI. kwani ulimbukeni ni kilema. Wabongo wengi walio nje ya nchi ni malimbukeni, na wachache tulio ndani ya nchi ni washamba. Ushamba wetu huwa unaisha pale tunapojifunza.

    Hapo juu utaona dada aliyevaa Boots, huyo ni mshamba, kwani unaweza kukuta katoka UK au nchi za Ulaya na kaja kutesa na boots zake bongo. Bila kujali kama kuna joto etc.

    Anonymous wengi waliochangia hapo juu ni MALIMBUKENI, kwani wako nje ya nchi basi kila kitu kilichopo bongo ni kibaya. Hawa hawatabadilika wataendelea kuwa washangiliaji tu. Wenzao wanasonga wao wanashabikia. Hawa ni Vilema, tena vilema wa kitamaduni, kifikra, kifalsafa na kiutashi.

    Jamani Bongo kama New-York. kila unachokiona New-york na kina umuhimu Bongo basi ujue kipo Bongo. Ukituambia sijui nguo za wachina, blah blah. ungejua kwamba hao madesigner unaowaona wewe wakali woote wanatengenezea nguo zao china, taiwan, hong kong usingejaribu kuongea ujinga. Na ndo maana mnakuja na vitu vyenu mlivyonunua bei kubwa US na UK, unakuta mbongo wa manzese katesa the same, tena kwa bei rahisi ya kariakoo. unabaki kulalamika ooh hiki siyo original, nani kakwambia cha kwako ni original? Vitu vinatengenezwa China, vinakuja kuuzwa US kwa bei ya kufa mtu, wakati watoto wa mjini wanavifuata huko huko kiwandani kwa bei ya kulialia, afu wanakuja kutuuzia kwa bei ya nyumbani.

    jamani Bongo ya Nyerere siyo hii ya leo, kila kitu kipo, tatizo matumizi tu. na ukija bongo ukakosa kitu unachokihitaji basi wewe ni mshamba, watafute wajanja wakupeleke kinakopatikana.

    ReplyDelete
  24. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  25. Kwa kweli mnaosagia wenwetu alio nyumbani hamna umaana kabisa. Vitu vingapi vinazalishwa china,taiwan, etc sababu ya cheap labour?sio nguo tu hata vyombo vya nyumbani n.k.Mimi nipo nje japo nina decent lifenikimaanisha nimeridhika na maisha niliyonayo kwa kweli huko kwa designer shops naendage pale kukiwa na sales "masalia after x-mas na mwanzoni mwa summer.....na nafahamu watu wengi tu wanaofika huko wakati kama hizi na hapo japo ni sale bado naonaga expensive ..kwa hiyo jamani acheni hiyo laana ya kujitafutia kabisa.....na dharau za kijinga

    ReplyDelete
  26. jamani tuipende nchi yetu na tuiheshimu,ila kuna haja ya kuwa realistic.hizi porojo za kwamba kila kilichopo new york Bongo pia kinapatikana zinaonyesha aidha hatuijui new york au tunajaribu kudanganyana.mac donalds,KFC,winter sports,village cinemas,MRI,subway,escallators to mention a few.vipo pia vinavyopatikana bongo ambavyo new york havipo kuku wa kienyeji,mlenda,sindimba,makatambuga na vinginevyo.sasa tunachopaswa kufanya sio kung'ang'ania kuwa na vitu vilivyopo new york ila kubuni mbinu za kuwafanya watu wa new york na kwingine duniani waheshimu hivi vyetu(iwapo tunavipenda na kujivunia navyo).

    ReplyDelete
  27. Nguo zinakwenda na weather sio kujivalia tu

    ReplyDelete
  28. Namshukuru tena kaka Michuzi kwa kutuletea picha mbali mbali ambazo zinasababisha mazungumzo yanayosababisha hisia mbalimbali za wasomaji kujitokeza. Huu ni uwanja mzuri sana kwa mwanasaikolojia kuanalaizi hisia na reactions za watu katika jamii.

    ReplyDelete
  29. Wewe Mvuvi na wenzio eleweni anony alichowaambia. Hizo bidhaa za China zipo duniani pote. TOFAUTI ni kuwa Bongo kwa sababu ya Rushwa, elimu duni, ujinga na ubishi wa watu kama nyie, bidhaa zinazoletwa na hao Wachina hazina quality kabisa!! Chukulia vitasa vya milango vya Kichina kwa mwaka unaweza kubadilisha vitasa kumi na mbili. Au ukinunua pasi ya umeme ya Kichina moto wake hauwezi ku-adjust. Hata nguo ni hivyo hivyo. Lakini kwa sababu wabongo mmezoea utapeli manaona ni sawa tu.
    Eti Bong kama New York acheni ujinga kulinganisha bwawa na bahari. Halafu siyo kila aliye ughaibuni anabeba box. Kwa kuwa ninyi hamna elimu mnadhaniwatu wote wako hivyo?

    ReplyDelete
  30. WE MICHUZI UMESAFIRI SANA KWA HIYO UNAJUA MAMBO MENGI AU VIPI? KWANZA NGUO ZINAENA NA WEATHER, VIATU PIA HIVYO HIVYO. DADA MWENYE BUTI NYEUPE INANABIDA ANGEKUWA HAPA KANSAS CITY KWA SASA KWANI NILIKUWA BONGO JANUARI 2007 NI KAMA MOTO WA KUZIMU. HALAFU SUALA LA VIKWAPA INAONEKANA DEODORANT HAMNA KABISA HUKO BONGO HASA KWA MABINTI HATA HAO MA-MISS WENU. SIO KANA KWAMBA TUNASAGIA BONGO ILA NI UKWELI TU. WABONGO WALIOKO BONGO HAWATAKI KUSIKIA UKWELI HATA KIDOGO. MICHUZI EBU WASOMESHE HAO?

    ReplyDelete
  31. i think ppl should worry more about doing better things that wat others do!! engage urself in things like education, wadada wabongo all they care about is dressing up...that doesnt give them a dignity as a real woman bila education! i dont find a dressed up woman bila education to amaze me. further more they get all they have from what they call kuchuna!! am a lady and i dont like that i do better things that dress up and expose myself.

    ReplyDelete
  32. Jamani msitugeneralized wote na kutuita malibukeni sijui nini. Wengine tuko huku lakini tunakuja home. Na home sweet home. Huyo aliyesema huko kwenu ni mjinga sana. na pia mjue sababu ya kupaita huko kwenu ni kwa vile hana papers za kutoka nje ya nchi. lakini msahau kwao ni mtumwa....na anatukana mahali palipo mkuza ni mjinga...
    Mimi nipo huku na kama nilivyosema hao watu wako kwenye catalogy kishenzi. Kila siku tuko kwenye party wala watu hawavai vya kutisha...
    Anayesema sijui mdada aliyevaa white... you just wait and see...the coming spring, and summer fashion ni mng'ari mng'ari tu anything shimmering, black and white ndio in....

    Beauty fade but dumb stays forever

    ReplyDelete
  33. kumbe tatizo vikwapaaa.... yaonesha wengi uliobahatika kupishana nao walinuka vikwapa na kikwapa cha mtu utakisikia ukimpitia karibu zaidi kama si kumkumbatia isije ikawa kaka ulikuwa unasalandia mahouse gilrs au ulienda kariakoo ukapishana na wanaume wametoka kufanya kazi za nguvu kikwapa kinakuwepo tu.......na kama haikutokea hayo ya juu utakuwa umesikia kikwapa home kwenu cha maana ukija au huko uliko watumie mabox ya deodorant na perfum ili wasikunukie tena

    la sivyo bear in ur mind kikwapa ni kama kaugonjwa hata huko uliko ughaibuni kuna watu wananuka vikwapa...midomo...na kumbuka sio wote wenye uwezo wakununua perfums cos watu hela ya kula tu issue... we mwenyewe uje tutembezane kwenye ukoo wenu ambao ni watz kama hatutakuta vikwapa.....

    Hata hao mamiss unaowaita mamiss...hawakushushwa na mungu waje kuwa mamiss wamepitia process uliopita weye sema ndo hivyo kwenye kuhangaika wakajikuta wanavishwa mataji..sawa na hao macelebrate wa huko fuatilia historia za wengi wengi wametoka vichochoroni......so ichanganue akilini mwako kama muelewa utaelewa na kama hutaki elewa tuchukulie poa...sio kiivyo unavyofikiria

    ReplyDelete
  34. Mimi nataka kuuliza hao watu walio ughaibuni wanaokandia bongo wakifa wanapelekwa wapi? Si wanaletwa kuja kuzikwa hukuhuku? tena wanazikwa na haohao ndugu zao wenye vikwapa teh teh teh

    ReplyDelete
  35. Shamim nataka uelewe one thing kuna tofauti ya deodrant na perfum! kama ukipaka pafyum bila ya kupaka deodrant lazima kikwapa kitajitokeza in a few na sijapenda point yako ya kusema kuhusu MAHAUSIGELI kwasababu wao pia ni madem wa maana kama unavyojiona wewe na wao pia wanauwezo wa kununua deodranti ok? RESPCET!!

    ReplyDelete
  36. Kwanza mwanaume akianza kumsema mwanamke kama ananuka na makwapa hivi na hivyo,ujue huyo mwanaume anakasoro.Jamani bugieni "Viagra" basi, msianze kuwakashifu mabintiz.

    ReplyDelete
  37. Jamani deodorant sio lazima utumie hela kununua. Na ukipaka perfume bila deodorant ndio utakua unanuka tuuu vitu visivyoelewka.

    Your sweat is odorless. It is the entrenched bacteria feeding on it that makes smells. You can never completely rid yourself of these bacteria, although they may temporarily be gone after zapping.

    Homemade ways to reduce bad odor na zinafanya kazi vizuri tu.. ,

    a) Milk of Magnesium dabbed on with a cotton ball.

    b Pure alcohol such as vodca with a cotton ball each morning, it will last all day! If it burns dilute with water.

    c) Baking soda use it to wash your armpit or mix one part of it, one part water and one party cornstarch mix it well before use and store in a tight container.

    d)Lemon Juice works fine too

    e) Ditto bar soap blocks the bad odor

    f) Midomo isinuke baking soda and salt works 100% better than total colgate. Salt water makes a good mouthwash.

    g) Foot powder dust your feet with baking powder or you can go extra mile by mix together baking soda, cornstarch and peppermint essencial oil. Let it dry overnight and store in a tight container

    Hey sio lazima kununua hizo deo na gharama isiwe excuse za kunuka. There are many ways to eliminate the ordor

    ReplyDelete
  38. jamani kwanini kunakuwa na ugomvi kati ya watz home vs watz abroad..
    sisi wote ni wamoja inatakiwa tuelimishane kwa maneno mazuri sio kutukanana na kudharauliana,ningependa kujadili hii issue ya viatu
    1.huyo demu amevaa hivyo viatu ni usiku hakuna jua kihivyo kiasi kwamba miguu ichemshe
    2.huko huko ulaya kuna watu wanavaa hivyo viatu summer inategemea unaenda wapi na time yenyewe
    3.sidhani kama kuna mjanja yoyote wa ulaya anaeweza kusema hivyo viatu FAKE kwa kuangalia picha hii
    4.ni kweli vitu vingi vinatengenezwa china lakini vinatofautiana quality hilo halina ubishi kama unajua unachoongea
    5.wanawake wabongo ni wazuri miongoni mwa wanawake weusi duniani,watu wote weusi wanakiri hilo na wabongo wanajua kuvaa na wamejifunzia bongo sio ulaya mimi mmojawapo
    4.suala la kunuka kikwapa ni personal inategemea umekutana na demu gani hata ulaya wapo wengi tu wananuka vikwapa na hao wazungu mnaowaabudu ndio balaa
    5.bongo sio new york...naipenda tz sana lakini ukweli lazima niseme.....bongo sio new york...kuna kila kitu kinachooneka na new york i dont think so najua wengi mnapenda kuzungumzia magari mnataja magari ambayo tz nzima hayafiki 5..hummer wamiliki wanajulika bakhresaa...sijaona hata FERRARI 360 SPIDER,BENTLEY,ASTON MARTIN etc bongo sio new york tho i prefer bongo to new york......BONGO FOR LIFE....RESPECT
    6.kuna malimbukeni wengi sana ulaya ndo hawa wanacomment za kijinga na kudhani bongo ni kama jehanamu labda wana refer walikotoka ndo tz nzima
    7.sio kila mtu kaja ulaya kubeba box...kuna watu wengi kila mtu anafanyakilichomleta kwa faida yake
    8.stress is everywhere kama uko responsible...kama kula kulala hutajua stress ni nini,there is no stress free life

    ReplyDelete
  39. offcourse anonymous hapo juu naheshimu saana MAHOUSEGIRL...lakini kuwataja wao sikumaanisha saaana kuwabonda nilitaka kumuonyesha huyo aliyekandia kuwa kama alisikia vikwapa alitoka na visichana vidogo ambavyo havijajua kuoga au wale wasio na uwezo wakununua...hata mie b4 sijawa na akili ya kuweza kuoga na kuwa na uwezo wakununua hizo nilikuwa nanuka kikwapa... who knows....so ni sawa na kusema nyumba fulani ina harufu....kumbe ulikuwa unashinda chooni utashindwa kwepa harufu ya chooo....hope umenipata

    Na pole kama umekwazika

    ReplyDelete
  40. nyie watu mnaoishi huko mnakoita majuu mnakasumba gani ya kukandia kwenye nyie mnaokandia bongo inaonyesha kabla ya kuondoka mlikuwa mafukara sana basi mnajua kila mbongo yuko kama ulivyokuwa wewe maisha ni popote ili mradi ujue kuitafuta pesa wengine mkirudi mkifika airport tu mnaona hata aibu jinsi mlivyo pauka unashangaa unavyokuta wabongo waliokuja kuwapokea wameiva na wanayawezea maisha kuliko baadhi yenu mnaoona ulaya ndio kila kitu wakati huko mnanyanyasika na kudharauliwa na wazungu

    ReplyDelete
  41. Jamani kuhusu suala la watu wa Bongo kunuka KIKWAPA wala msibishe kwa sababu ni kitu ambacho kinajulikana na wengi. Na tena asilimia kubwa ya wanaonuka KIKWAPA sio kwamba hawana uwezo wa kununua deodorants, wengi wao wana pesa na kazi nzuri tu lakini nadhani wanaona hakuna umuhimu wa kutumia Deodorant. Mtu unakuta anajipaka perfume au Cologne lakini anashindwa kuweka Deodorant, sasa hapo lazima harufu kali itoke tena ukiongeza na joto la bongo basi harufu yake ni mbaya na kali kama mzoga wa kuku.

    Badilikeni watu wa Bongo na muanze kutumia Deo ili msitutese kwa harufu mbaya tukija Bongo.

    Halafu kitu kingine sio kila mtu alieko Bongo ananuka KIKWAPA kwani nimeshakutana na watu wanaonukia vizuri sana pale Bongo na wanajiweka fresh muda wote. Nyinyi mnaotumia Deo hapo Bongo hebu waelimisheni wengine nao waanze kutumia.

    ReplyDelete
  42. Dah sasa ina maana Jk anajua kama wananchi wake wana nuka kikwapa kama anajua basi ina bidi akienda ulaya aagize deodorants..zingie bongo kwa msaada kama condom maana ni balaa hehehe

    ReplyDelete
  43. Eboooooooooo! jamani imeshakuwa vita kati ya wabongo wa bongo na waishio juu? anko michuzi kauliza tu mmeona madada? khaa! BTW kuhusu vikwapa hata huku majuu kama kawa tu.. jana nimepanda train na mbongo anasmeli kwapa dunia.....

    ReplyDelete
  44. Mimi naogopa kutoa maoni yangu,maanake wachangiaji waliowengi hawalijui neno KUJENGA wanachojua ni KUBOMOA tuu!!!!!1

    ReplyDelete
  45. Shamim 'zeze' Amakweli Mungu amekujaalia...hongera sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...