rais joseph kabila wa congo drc na mugabe wa zimbabwe walipokuwa umoja wa mataifa mwaka jana. wote wako dar leo tayari kwa mkutano wa wakuu wa nchi za sadc kesho

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Jamani huko Zimbabwe hali mbaya. Mpaka kuna wakimbizi kutoka huko. Zamani kila mtu alitaka kwenda huko. Sasa huyo Mzee Mugabe sijui vipi tena.

    ReplyDelete
  2. Viongozi wa Afrika Mbaneni Mugabe aondoke Uraisi haraka.Mauaji ya kimbari yako njiani Zimbabwe.Msome nyakati.Msisubiri hadi watu wa ndani na nje waunde majeshi ya mamluki kupambana na Mugabe halafu ndio mjitie kuita vikao vya dharura.

    Muulizeni Mugabe nyumba zake na Akaunti zake za nje ya nchi zilizotaifishwa pesa alizipata wapi za kuweka huko na kununua hayo majumba? Mla rushwa mkubwa huyo.

    Suala la Ardhi Zimbabwe Rushwa ndio ilinyamazisha viongozi wa Zimbabwe wasishughulikie suala la ardhi kuanzia walipopata uhuru.Viongozi wa juu wa Zibabwe Waliwekewa mapesa na kupewa Majumba Uingereza,Ulaya na Marekani wakanyamaza.

    Walipotaka kudai rushwa zaidi kila mwaka kutoka kwa wazungu wenye mashamba Zimbabwe,Wazungu wa Zimbabwe wakagoma ndipo Mugabe akapanda hasira akasema mtatukoma akaanzisha sera za kuwakomoa wakulima wa kizungu Zimbabwe.

    Mugabe ana hasira na mataifa ya magharibi siyo kwa sababu ana uchungu wa Zimbabwe bali ana hasira ya nyumba zake zilizochukuliwa Ulaya na Marekani, na Akaunti zake na za washirika wake zilizokuwa frozen Ulaya na Marekani.

    Vita ya Zimbabwe ni kati ya viongozi waroho wala rushwa wa Zimbabwe na Wakulima wazungu watoa Rushwa wakikomoana baada ya kushindana dau.Mugabe anatimua wazungu ,wazungu wana-freeze Account na kutaifisha mali za viongozi wa Zimbabwe na ku-frustrate Economic System Za Zimbabwe.Matokeo yake Tembo wawili wakipigana nyasi ndio ziumiazo.Wanaoumia ni wananchi wa Zimbabwe.

    Dawa ya tatizo hili ni nini? Wazungu watoa rushwa wameshatimuliwa kilichobaki ni kuwatimua wala rushwa wazawa wa Zimbabwe(viongozi wa juu wa serikali ya Mugabe) akiwemo Mugabe mwenyewe apishe wengine walete mabadiliko Zimbabwe.

    Nchi za Afrika zimchukulie hatua Mugabe na serikali yake wasimchekee.

    Chanzo cha mgogoro mzima wa Ardhi ni Rushwa pamoja na kuwa Mugabe anajaribu kutumia watu kama "human shield" akisingizia eti anawatetea kuhusu ardhi siyo kweli ni mwongo mkubwa asiye na haya.

    Waafrika tusimchekee Mugabe kama Viongozi wa Afrika hawataki kumshughulikia wananchi wana haki ya kujitwalia sheria mkononi kumtimua.Na hili wala haliko mbali.Na mwenye macho hana haja ya kuambiwa tazama.

    ReplyDelete
  3. Nakumbuka medical school wanafundisha kuwa watu wengine uzee ukizidi inatokea brain degeneration,nadhani Mugabe ni mmoja wao.Huyu mzee aambiwe ukweli,asiogopwe.naona anazeeka vibaya!aambiwe upuuzi wake hakuna anaependa uendelee.mfumuko wa bei 1800% halafu anadai hali ni shwari?

    ReplyDelete
  4. HALAFU MUGABE NA KABILA WAMEOWA WANANDUGU.. (MTU NA DADA YAKE)NA WOTE WANA HISTORIA YA KUWAKIMBIA WAUME ZAO NA KUOLEWA NA MARAISI... MMH KWELI NAWATAMANIA KABISA

    ReplyDelete
  5. Wewe mtindiga uliyetoa maoni March 29 2.32 na hao wazungu unaowaabudu mnataka zimbabwe itawaliwe na vibaraka kama Tshangarai siyo? Huo utumwa Jongwe Mugabe hakubaliani, na kwa hilo namuunga mkono. Hayo mashamba kama wangenyang'anywa waswahili nobody could have cared.

    ReplyDelete
  6. Sir Issa Michuzi huyu anon wa (Thursday, March 29, 2007 8:36:00 AM )Kumbe watumwa bado bwelele...wakumwaga...

    ReplyDelete
  7. nyie wote hapo juu ni mafala.
    huyo mzee lazma atoke hakuna cha utumwa wala nini. wenzake wote wa rika lake wameshakufa au wametoka madarakani. yeye anangoja nini? au anataka azikwe kama rais? msiwe na mawazo finyu. hii ni karne nyingine.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...