taarifa za redio mbao zilizonifikia punde ni kwamba wanafunzi wa udsm waliofukuzwa juzi kwa kugoma kuingia darasani wametakiwa waandike barua ya kujieleza ikiwa imeambatanishwa na 100,000/- ya matibabu pamoja na ada asilimia 40 (kama laki nane hivi) kupitia benki na wawe wamezipeleka barua na risiti za malipo hayo ya benki kwa makamu mkuu wa chuo kati ya aprili 23 hadi mei 4 ili kuweza kufikiriwa kurudi chuo. nafanya juhudi kupata waraka kamili wa masharti yote. vuteni subira

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 36 mpaka sasa

 1. Aaaagh!!! Upumbavu huo? Aibu CCM!
  Ni nchi tatu tu Africa hii wana hayo matatizo na SISI ni wamoja wapo ha ha ha!!!

  KAMA HAUJASOMA KUFIKIA VYOUNI AU HAUNA EXPERIENCE YEYOTE....USITOE MAONI!!!! Kwani huna unalolijua.....

  ReplyDelete
 2. NOMAAA WABWELA.NOMAA HILO DUH JUA KALI MNALO MWAKA HUU. MIMI NIKIBEBA BOX AU KUSAFISHA CHOO WIKI MOJA TU AAAIIIIIIIIII LAKI NNE KAMA KUMSUKUMA MLEVI KWENYE CHOO CHETU CHA SHIMO MBAGALAAAA.
  MLIOGOMA NA HAMTAKI KUBEBA MA-BOX HIYO KILO NNE NDO MNAONA NYINGI SANA WAKATI WATOTO WADOGO WANASOMA KWA MILIONI MOJA KILA MWAKA NA HAKUNA MSAADA. KALIPENI KULE ACHENI KUPENDA DEZOOOOOO INAUAAAAA.

  ReplyDelete
 3. Kama itakuwa ni kweli, basi siri kali yetu itakuwa haina akili....
  wapi mtu atapata hiyo laki 8 katika kipindi kifupi namna hiyo...
  mwe mwe!!!

  ReplyDelete
 4. hiyo laki nane mi ndo nalipa kwa credit hr 1, fikiria nikisoma credit hrs 12. halafu hiyo ni semester moja tu piga hesabu semester 2 kwa mwaka. serikali imewaonea huruma sana hawa watoto hawana budi kuishukuru. hata hivyo sio lazima kila mtu aende up to college level, kama huna hela piga bunda wenye nazo waende changachanga ukizipata utasoma baadae. safi sana serikali na hiyo asilimia sitini ipewe benki kufatilia watu wazirudishe wakimaliza

  ReplyDelete
 5. We Anonymous wa April 19, 6:40:00, hiyo taaifa imesema laki NANE siyo nne kama unavyojigamba na mabox yako huko. Kweli wewe unatoka Mbagala hata akili yako na mawazo yako yanaonyesha hivyo.Pfffffffff

  ReplyDelete
 6. kwako wewe michuzi kutumia lugha za ajabu ajabu nadhani pamoja na kuwapotosha wasomaji wako, nadhani pia unajishushia hadhi.

  haileti maana kwako msomi, na mtumishi wa serikali kupigia debe lugha zisizokuwa na wafuasi.

  ni maoni tu, it's your blog unaweza kuandika chochote utakacho.but, it's not effective in a way, why breking nyuuz??

  ReplyDelete
 7. Yaani hiyo ndio ilikuwa sababu ya kuwatimua jamaa, mi najua laki nane kwa wiki mbili mbinde, cha kufanya ni kwamba jamaa wasiandike hata kama chuo kitafungwa kwa miaka kumi poa tu, ila wakiandika tu wameliwa na hii ndio njia wanayoitumia jamaa kukandamiza elimu sasa hapa ndio mwanzo wa ngoma ya mchezo mwisho wake wanaujua serikali.

  maamuzi butu yasiyo na fikra za kimaendeleo. Jamaa wakomae hapo ndio patamu tuone kama chuo kitafungwa kwa miaka 10 kama kina mukandala na msolla hawakosa ajira.

  ReplyDelete
 8. MAMBO MCHIBUYU!!!KUKU NI KUKU TU JOGOO JINA!!! TULISEMA HAPA HIYO NDO SOLUTION TUONE SASA WATARUDI AU WATAENDELEA NA HUO MGOMO UCHWARA.WATOTO WADOGO TU TUNAWALIPIA FEES HUKO BONGO NEARLY 800,000.IWEJE MTU ATAKE KUSOMA CHUO KIKUU BUREEEEEEEEEEE!!!J.K KAZA UZI BABA WATOTO HAO WASIKUBABAISHE KABISA AMBAYE HATAKI KULIPA BASI AACHE CHUO HAKUNA CHA 100% KWANZA MKOPO HUWA HAULAZIMISHWI KIIVO.WANGESEMA WALIPE AT LEAST 20% MAY BE WANGEFIKIRIWA LAKINI SIO FULL100%.

  ReplyDelete
 9. Nilifanya jambo la maana sana kujilipua, huu ndo upumbavu watu wasio hutaka. Kama mtu alishindwa kulipa ada ya sekondari mnazania hatawaza wapi kulipa hiyi milioni. JK na hao mawaziri wake waliosoma hapo mlimani wao walilipa au walisoma bure. Sasa hawa watoto wanaomba mkopa wa asilimia 100, serikali haitaki kuwapa, wakati wao wenyewe wame ove spend bilioni 950 kwa kipindi cha mwaka mmoja kwa vitu vya upumbavu. JAMANI HUU NI MKOPO SIO KWAMBA WANATAKA WASOME BURE!!!

  ReplyDelete
 10. Michuzi kama hii ni kweli basi tanzania tumekwisha, itabidi tuanze kujilipua tu make hapa kitakuwa kizungu zungu. Watoto wenye pesa ninavyojua hawawezi soma chuo kikuu cha dar. Kwanza ni kwamba hawana akiri ya kusoma pale.

  Hawa huwa wanapelekwa majuu ambako wanabembelezwa angalau kusoma na kunywa uji. Sasa mtoto wa mkulima ambaye wakati mwingine kuingia chuo huwa ni mara yake ya kwanza kufika bongo, hiyo hela ataipata wapi? Tusidanganyane watanzania itabidi tupiganie haki.

  Changamoto kwa serikali ni kuweka utaratibu mbadala kuhakikisha watoto wanasoma hata kama ni kuingia mikataba na mabenki hili yasaidie katika kuwakopesha hawa watanzania wasiokuwa na uwezo.

  Lakini si busara kuwatwisha mizigo isiyo bebeka. Kwa sababu watu wanajipatia hela za vikao bure na kula rushwa wanafikiria kuwa hata wale wa vijijini wana uwezo.

  Chondechonde JK angalieni hata kijijini kwako bagamoyo ni watu wangapi wanaweza pata hata laki nne kwa wiki mbili.Wekezeni katika kuangalia mkakati wa watanzania kupata elimu bila kudhalilika nafikiri akina dada/kaka wataumia sana make hizi hela zinaweza kukuingiza katika mambo yasiyokuwa ya lazima.

  Kutangaza hiyo hela ni sawa na kutangaza hali ya hatari

  ReplyDelete
 11. Ni bonge la AIBU kwa serikali ya Kikwete, wanaacha kukamata na kuwafukuzana na wauza madawa na na wavyonzaji wa umma ....na kufukuza SHULE wanafunzi ambao ndio taifa la kesho. WHAT DO YOU THINK HUYU MWANAFUNZI ATAISAIDIAJE TAIFA AU SERIKALI YA KESHO???? Kikwete, Lowassa .....you better do something !!!!

  ReplyDelete
 12. Kwa kweli nijitahidi kufikiria kama haya baadhi ya maoni humu ndani yameandikwa na Watanzania au Watanza-european, au Watanza-american, kwa kweli ni aibu kubwa sana kwa baadhi ya maoni hayo.

  Hivi kwa vile ninyi mko nje au mna uwezo wa kifedha ndio mnafikiri kila mtanzania yuko hivyo? Hata hamjui world bank records zinasema vipi kuhusu average income per capita ya Tanzania ni U$350.00 (kumbuka ni kwa mwaka mzima), ambayo ina maana Mtanzania kwa wastani anaishi for less than a dollar per day?

  Pamoja na kuwa na ukweli kwamba baadhi ya hawa wanafunzi wazazi na walezi wao wanaweza kulipa hiyo Tshs.800,000/-, lakini nina imani wengi tu hawana uwezo wa kulipa kiwango hicho, na sasa wanaambiwa walipe kwa muda usiozidi wiki mbili kutokea sasa, kwa kweli serikali yetu imelewa madaraka na labda huu ndio utakuwa mwanzo wa watu kuanza kuchallenge ahadi za wanasiasa, nanukuu, " hakuna mtoto wa maskini ambaye atasimamishwa au kuachishwa masomo kwa kuwa hana fedha za kulipia ada" Jakaya Kikwete kwenye moja ya hotuba zake kuhusiana na maswala ya elimu bongo.

  Kama nilivyosema hapo siku za nyuma, HUU NDIO MWANZO WA TANZANIA KUJENGA MATABAKA, kwani ni wale ambao wazazi/walezi wao wanauwezo wa kuwalipia ndio watakao weza kwenda kubukua na wengine labda wapate misaada kutoka wapi sijui maskini. Halafu ndio tunasema usawa, haki na uhuru.....

  Nafikri ujumbe kwenye yale mabango tuliyoyasoma yamewaudhi sana wakubwa serikalini, na wameamua kuwafanyizia sasa, maskini wanafunzi.

  Jamani hizo hela hawapewi bure, ni mkopo, ni haki yao ya msingi kabisa kama raia wa Tanzania, watazilipa wakipata ajira muafaka...wekeni njia bora za ufuatiliaji tu. Inaniuma sana nikiangalia wale wote wanaoongoza serikali kwa sasa wamesomweshwa na serikali wengine hadi ng'ambo pamoja na watoto wamepata scholarships za bure, na wakirudi wanafanyiwa mipango ya kupata post za maana.....naona kabisa kwamba Tanzania ya matabaka inakuja kwa kasi mpya, nguvu mpya na ari mpya.

  Tumesoma na watu shule za sekondari tu ambapo school fees ilikuwa haizidi hata Tshs.300,000/- kwa mwaka na bado watu kibao walikuwa wanafukuzwa kwenda kutafuta fees kwa vile hawakuwa na uwezo wa kulipia, sasa unaniambia hiyo laki nane kwa wiki mbili....kama sio ubabe wa serikali ya Kikwete kupitia uongozi wa Chuo Kikuu ni nini?

  KAlaga bao, Wakenya na Waganda wanazidi kupeta, na Tanzania ndio siku zote itashika mkia pamoja na kujivunia bila chochote cha maana kwamba sisi tuna amani na utulivu, halafu hizo zenye ukabila na vita, wametuacha kiuchumi ukiangalia ripoti za benki ya dunia.

  Tunatoa visingizio eti Mwl. Nyerere alituulia uchumi, mbona Museveni alichukua nchi ya Uganda miaka ishirini iliyopita wakati karibia kila kitu kilikuw hakifanyi kazi, fedha yao ilikuwa haina thamani ;lakini angalia sasa, wanatuzidi kiuchumi, hela yao ipe miaka miwili mingine tunalingana nayo thamani.....

  Wabunge wanalipwa Tshs. 100,000/- kukaa bungeni kwa siku moja, mshara wa Tshs1,600,000/-, na marupurupu mengine, na kiinua mgongo cha Tshs.22,000,000/- kila baada ya muda wa miaka mitano kuisha, na ndio wengine wananenda kuongea pumba wakati junior Doctors wanaoma walipwe Tshs.587,000/- kwa mwezi kama mshahara inakuwa ngumu, halafu tuwe na sera bora za afya kweli?

  Vitu vingine imebidi niviweke katika kufafanua mifano wa unyanyasaji unaofanywa na serikali kwa watu waliopo kwenye vitengo nyeti vya uchumi na maendeleo ya nchi. Sitaki hata kuongelea walimu kwani wao ndio wanadharaulika kabisa. Chelewesha hela ya wabunge siku mbili uone......mbona hao hao ambao ni mashuhuri kwa kudai zao, na katikati mwaka jana walitaka waongezewe mishahara (wabunge) iwe zaidi ya Tshs.2,100,000/- kwa mwezi, wanashindwa kusimamia au kuwapigia debe walimu waongezwe mishahara?

  Mungu ibariki Tanzania....

  Concomitant13 or
  concomitant13@yahoo.com

  ReplyDelete
 13. we fly high no lie you know this ballinnnnn mnasema sana watu wanaoishi njeee .kutwaa mitatizo sasa hata laki nane acheni dezooooo lipeni serikali hawajafanya bayaaaa

  ReplyDelete
 14. Hao jamaa wanaojiita wako nje waache upuuzi. Nani hayupo nje? Mbona fikra zenu si endelevu? Nani asiyefaham matatizo ya Watanzania wengine? Michuzi nilikuwa Tanzania, nadhani maximum fee ni 800,000 kwa hiyo times 40% ni km 320,000 kwa kozi nyingine ni laki 6.
  Nipo nje ya nchi ila natambua hiyo ni ada kubwa sana kwa Watanzania wengi. Tuache hoja zisizo na msingi, tuwape ushauri mbadala na si chuki.

  ReplyDelete
 15. Safii sanaa..hapo sasa ndio mtatia akili. Kagomeni basi huko Bank muone..serkali iweke huu utaratibu na isiwe inajihusisha..Wanafunzi waende moja kwa moja Bank kuomba mkopo waje shule kusoma tuu.

  ReplyDelete
 16. laki 4 itatoka wapi jamani-imebakia wiki moja tu.

  Naomba kuuliza, ni kwa nini Serikali haitaki kutoa 100%? Ukizingatia kuwa huu ni mkopo na sio bure?

  Mambo yamebadilika, lakini uchumi wetu haujaendena na haya mabadiliko. Sio rahisi kwa wanafunzi kujiajiri kuzipa hilo pengo. Nafikiri itabidi kupunguza kuchangia vifo na harusi, ili watoto waande shule. wengine mnasemaje?

  ReplyDelete
 17. Nyie wabongo mlioko nje (japo sio wote) acheni kuwa mafala...
  mnaacha kutoa maoni ya kujenga mnatoa kejeli zisizo za mpango.

  hizo habari zenu za "Mabox" nani kawauliza? Mnamwaga siri zenu wenyewe zikiwarudia mnaaza kujigamba kwa vitu visivyo vya msingi "kubeba mabox".

  mkataa kwao mtumwa na nyinyi ndio mnaproove hivyo.

  wengi mnaojidai kuwa mnasoma nina uhakika mlitafuta hifadhi huko mliko kwa sababu hamkuwa na qualifications za kuingia UDSM. Acheni vipanga wasome na sio kutoa kejeli zisizokuwa na mpango wowote kenge nyie!...
  Majisifia kuwa mahausgeli na mahaus boy wa wazungu!..
  Uafrika gani huu...

  Naamini huko ughaibuni kuna wabongo wenye akili zao timamu, tatizo ni hawa mijusi wanaombata na mamba na wao kujifanya mamba....
  Mnakuwa watu wa kutaka misifa tu kila kukicha.. Mkija bongo kujipendekeza kwa Michuzi ili 'awaweke hewani' kwenye tovuti yake..

  kwa taarifa yenu sasa nyie mijusi mlioko huku nje, WATANZANIA wajanja ni wale wanaokwenda nje na kurudi bongo sio nyie mnaobaki huko na kugeuzwa mayaya wa watoto wa kizungu.

  Acheni hizoooooooo...........

  ReplyDelete
 18. wanafunzi wasitoe hata kidogo. simameni na msimamo wenu 100% hii ni loan ambayo watarudisha. Iwapo serikali yetu ina uwezo wa kukopesha mamilioni kwa watu ambao hawana hata business plan kufanya biashara inakuwaje isiwakopeshe watoto ada ya shule ambao wana invest katika Elimu ambayo ndiyo kitu muhimu sana katika maendeleo ya taifa lolote duniani? Je wazazi wa Tanzania mbona mko kipya namna hii ?kwa nini hamuungani na watoto wenu kugoma na kuilazimisha serikali itoe mikopo. Je invstment ya Tanzania ni kununua magari ya kifahali ya wabunge na wala si elimu. Je kuna mtoto yoyote wa waziri au mbunge amefukuzwa au ni watoto wa wakulima peke yao ?

  ReplyDelete
 19. Ndiyo maana Tanzania maendeleo duni kwasababu wenye hela kama nyie hapo juu ndio mnaoenda shule, tatizo mabwege woote nyie, mnapata degree kichwani hamna kitu!
  unafikiri akili zipo kwenye international na hizo St. Mary na wengine mnaolipa mamilioni? wanafaulu hapo kwasababu kila kitu kipo, ukitaka kuona akili haswa nenda Mzumbe, Kilakala, Ilboru, Tabora, Msalato, watoto wa walalahoi wengi, walimu hamna lakini vichwa vimetulia!
  and yes, I am talking from experience, nimesoma huko!

  ReplyDelete
 20. Yaani sijawahi kuona watu hawana akili kama wewe mbeba mabox huko uliko.Kama wewe shule haipandi beba box acha wenzio wapige kitabu.Hayo mabox ungebeba mjinga wewe kama asingekuwepo msomi wa kuligungua hilo box na kilichomo ndani ya box.

  Kwa kweli hapo ni kuendelea kugoma.Maana najua wanafunzi hawakawii kuanza kutajana na wengine wenye uwezo kuandika hizo barua na kulipa hiyo ada.Tuwe na umoja na ushirikiano mpaka mwisho.Maji ukiyavulia nguo lazima uyaoge.Sasa waendelee kukaza kamba tu.Tuone kama hao walimu watalipwa miaka 10 bila kufundisha

  ReplyDelete
 21. Sasa ndio wakati umefika wa kutimua madarakani serikali ya CCM. Wasomi wa chuo kikuu mpo? Jiwekeni mkao wa kula, uchaguzi mkuu ujao CCM iondoke.

  ReplyDelete
 22. Hii ni kazi kwa vile sasa hivi kila mtu yuko kwao na wengine watatoa na wengine watakaoshindwa kutoa basi ndio hivyo chuo kimeisha. Kama kweli wanasolidarity walivyoamua kugoma basi waendelee hivyo hivyo.

  Kwani ocntract zao zinasemaje hapo? Kani walitakiwa kutoa hiyo 40% toka mwanzo? Kama walitakiwa basi hawatakua na any saying lakini kama hiyo issue imekuja tu from no where they have the right to say no and find a legal help.

  Si tuna malawyer wengi tu bongo sasa hivi? This is the time for them to earn some extra money too.

  Lakini utakuta wanagoma tu bila kuangalia contract zao zinasemaje...Ukiingia hizi nchi za watu kwenye student orientation unaambiwa ...before you sign anything...READ FINE PRINT. Je walisoma zao

  ReplyDelete
 23. Eee bwana Kwanza wacha nikupe hongera bwana Issa wa Michuzi, Pili naomba nikwambie wala usipate taabu kupata hiyo copy ya press release we nenda tu chuo watu kibao wana copy au ukitaka kuipata kiurahisi basi we shuka kwenye computer labs kule mabwenini maana wanafunzi ambao wanaenda kuendelea na kazi zao wengi wao wanazo, pili naomba nijaribu kuelezea kwa kifupi kuhusu hii 40% ni kwamba si wote ambao watatakiwa kulipa laki nane hapa inategemeana na kozi unayochukua, ni kweli wapo wengine watatakiwa kulipa mpaka laki tisa lakini wengine pia pia nhiyo 40% watatakiwa kulipa about 200,000/= but all in all kwa research ndogo niliyoifanya mimi hapa mlimani kwa kweli wanafunzi wengi ni wala wanaotoka kwenye familia za masikini,, na unakuta mtu huo mkopo anaopewa ndo huo huo anautumia kusomesha na wadogo zake huko kwao kijijini na kusaidia wazazi wake angalau waweze kusogeza siku,, sasa leo ukimwambia aje chuoni na laki nane kwa kweli hapa mimi naona haitawezekana,, na watu wengine wakisikia hili wanasema wawaambie wazazi wao wauze ng'ombe huko kijijini kwao sasa si familia zote zina ng'ombe pili na hii riftvaley nani anayenunua ng'ombe??
  JAMBO LA PILI
  Kwa upande wangu mimi naona hii Serikali imekurupuka kwenye hili swala la mikopo,, unajua kuna watu mpaka leo wanadaiwa na hiyo bodi ya mikopo na jamaa wanafanya kazi nzuri tu na wengine wameshakuwa mabilionea lakini serikali haitambui kama mtu huyu tunamdai, kwa kifupi bongo bado mimi nilitegemea Serikali ingekaa chini kwanza then ijiange kisawa sawa kwa mfano wangeandaa system kwa nchi nzima kwamba kila mtanzania awe na social security number then hutaweza kupata kazi bila kuwa na hiyo social secuity number na kila mwajiri asiajili mtu asiye na social security number, hapo ingekuwa rahisi sana kwa wao kujua ISSA MICHUZI yupo wapi na anafanya kazi gani na ameajiriwa na kampuni gani, sasa hapo ndo wangeanza kusearch hizi sec no,wangekupata kiulaisi sana na wangekuwa wanakata pesa yao kila mwezi. Asante bwana Michuzi kwa kazi yako nzuri... keep it up

  ReplyDelete
 24. Hao wasomi wa chuo wanashindwa hata kutumia Technology ya Internet ili kupanga strategy zao ili kieleweke....kwanini hawafungui website yao ili kuweka mambo yao live na ijulikane cha kufanya...fungua website haraka sana na weka sehemu ya PRESS,chat room,forum ili mjadiliane cha kufanya lakini hawa mbumbu najua hawawezi

  ReplyDelete
 25. UJUMBE KWA WANAFUNZI NA PIA KWA RAIS KIKWETE...

  WATU WENGI HUMU MNAPIGA YOWE ISIYO YA MSINGI SERIKALI ILITAMKA MAPEMA KABISA KWAMBA MWAKA HUU KILA MWANAFUNZI ATALIPA ASILIMIA 40, NA KAMA HUWEZI BASI ACHANA NA SHULE SASA IWEJE WANAFUNZI ZAIDI YA MILLION MOJA HAWANA HIYO LAKI NANE WAKATI KILA KUKICHA WATU WAKO BAA WANAENDESHA MAGARI MAZURI SASA NI KWELI KILA KIJANA WA CHUO KIKUU KAKOSA ADA? HUU NI UPUMBAVU KUONA KILA MWANAFUNZI ANAANDAMANA INGEKUWA VIZURI WALE WACHACHE WASIYO JIWEZA NDIYO WAGOME LAKINI MIJITU MIZIMA NA AKILI ZAO YANAENDESHWA NA HAYO YANAYOJIITA ETI PUNCH, PUNCH MY ASS...SORRY MICHUZI KWA LANGUAGE YANGU, KAMA HUNA UWEZO WA KULIPA BASI JALIBUNI NJIA MUUAFAKA YA KUDAI HIZO HELA NA WENGINE WENYE UWEZO WA ENDELEEE NA MASOMO KAMA KAWAIDA KULIKO KUSABABISHA WATU WENYE UWEZO KUKOSA MASOMO KUNA WATU WANATOKA NJE YA NCHI WANA SHOLARSHIP ZAO LAKINI WAABIDI WAKOSE MASOMO KWA SABABU YA ISSUE ZA KIPUNGUANI.

  KIKWETE... NA WEWE KIKWETE UNAKOSAJE HELA ZA WANAFUNZI WAKATI UNAPATA HELA ZA KUWALETA WACHOVU REAL MADRID KUCHEZA DAKIKA TISINI KWA POUND MILLIONI 150? JALIBU KUFIKILIA KWANZA KABLA YA KUWATIMUA HAO WANAFUNZI. TIMUA REAL MADRID NA DEAL ZAO FAKE, HAO WALIO KUTAPELI RADA WAMBIE WAKURUDISHIE PESA UWAPE WANAFUNZI, HAO WALIOINGIZIA HASALA TAIFA KWA MIKATABA FAKE YA MADINI WAMBIE WALIPE FIDIA UWAPE WANAFUNZI,HIZO RUSHWA NA UKWEPAJI KODI ZA KUINGIZA MAJENERETA WAMBIE WALIPE KODI WAPE WANAFUNZI WASOME... ACHANA NA USANII KIKWETE WATHIBITISHIE WANAFUNZI HAKUNA HELA KABLA YA KUWATHIBITISHIA REAL MADRID KUNA PESA YA KUWAKODISHIA NDEGA NON STOP FROM SPAIN!

  ReplyDelete
 26. SIKATAI WANAFUNZI KUCHANGIWA LAKINI MUUNDO HUU WA KUMLIPIA MWANAFUNZI HADI HELA YA KUNUNULIA DAWA YA MENO NDILO LINANITATIZA NI KUMDUMAZA UWEZO WAKE KTK SUALA ZIMA LIHUSULO UBUNIFU KIJANA HUYU AKIMALIZA SHULE ATAULIZA .....SASA KAZI ZIKO WAPI? AKIKOSA ATASEMA SERIKALI HAIMJALI, LAWAMA NAITUPIA SERIKALI LAZIMA IELIMISHE WANANCHI WAKE KTK HILI PIA ONGEZEKO LA SHUGHULI AMBAZO KIJANA WA HIGH SCHOOL ANAFIT KUFANYA KUWEZA KUJIWEKEA CHOCHOTE HATA INAPOFIKA WAKATI WA KUINGIA CHUO BASI AWE NA CHOCHOTE CHA KUMSAIDIA AWAPO CHUONI NA KWA UPANDE MWINGINE ATAFUNGUA MACHO KUJUA NINI ATAFANYA HATA MARA BAADA YA KUMALIZA ELIMU YAKE YA JUU HIYO

  ReplyDelete
 27. kwanza nakushukuru sna mr. MUHIDINI MJCHUZI. kwa kazi nzuri sana unayofanya katika kulisaidia taifa letu la tanzania kusambaza taarifa nzuri na zinazo sikitisha sana zinazo endelea hapo nchini hususani sana kwa watu kama sisi tuliokuwa nje ya nchi, Mimi ningeweza kusema kwamba serikali inabidi ifikirie sana juu ya swala hili maana kuna vijana wengine hali yao kwao kimaisha ni duni sana kwa hiyo wanavyo sema wachangie gharama za masomo imnakuwa ni ngumu sana bse laki moja mpaka nane kwa sasa kwa maisha ya mtanzani ni pesa ni nyingi sana hivy ni wazi kuwa wanafunzi hawa watashindwa kumuda malipo hayo kwa hiyo mimi ningeshauri sana serikali pamoja na viongozi wengine wote husika wafokirie swala hili kwa umakini zaidi. kwani iliwezekana vipi hapo zamani wazee wetu na viongozi wetu wote walikoko serikalini walisoma bure bila kuchangia gharama yeyote? anyway mwishp maweza kumalizia kwamba katika idara inayohusika na maswala haya ni wakubali kwamba suala hili halina ujanja nilazima wawarudishe vijana hawa chuoni na sivinginevyo na kama walipanga kutengeneza pesa basi wajue kwamba kwa njia hiyo ni ngumu sana na itawatokea kooni maana sisi watanzania wote tunakerekwa sana na swala hili au hawataki vijana wetu waelimike? au hawataki tuwe na taifa la wasomi?
  'TUNAOMBA WAHESHIMIWA MTAFAKARI SANA JUU YA SWALA HILI'

  ReplyDelete
 28. Poleni sana Vijana, kwa hilo janga ninaita janga kwasababu ninaelewa maisha ya Tanzania laki nane kwa wiki kazi sana, kwa sisi tunaotoka kwenye familia za wakulima.
  Msolla, Msolla wafikikirie wakulima, wewe ukikaa mahali unataka pesa yote ije kwako, kopesha vijana hawa wasome wawemaprof kama wewe , wewe isingekuwa bure elimu ya juu ungefika hapo?, na huyo Kikwete?.

  ReplyDelete
 29. HURUMA IMENIINGIA NIMEAMUA KUWASAIDIA VIJANA WA MLIMANI KURUDI SHULE,kwa wale mnaotaka msaada oredhesheni majina yenu halafu mi nitawalipia hiyo ada. kuna hela fulani ya box nilikuwa nime-save nadhani itatosha kulipia wanafunzi wote mlimani hiyo asilimia 40 kwa miaka kadhaa

  ReplyDelete
 30. Hivi nyie mnaotoa maoni ya kuisupport serikali mtakuwa HAMJASOMA wala HAMJUI SHERIA yeyote ile kuhusu hao WANAFUNZI!!!!
  So shut your CHOO up!!!
  Mnajua serikali inatumia kiasi gani kwa mambo ya MATUMIZI na SIFA kwa nchi za jirani kwa mwaka???
  Mnajua wamepanga kutumia pesa ngapi just kwa mafunguzi ya uwanja wa Taifa??
  Mnajua ni misaada kiasi gani inamiminika kutoka nje kila leo???
  Mnajua wabongo tunahitaji wasomi kiasi gani????
  Give me a break guys!!!
  Fanyieni uchunguzi bila ya kuropoka, sio wajinga au teenagers hao....watu wazima na akili zao.

  ReplyDelete
 31. we anon Friday, April 20, 2007 9:30:00 PM,toa pumba hizo kichwani kwako.
  bottom line is hakuna kitu cha bure, ukimaliza shule utaanza kutengeneza laki kadhaa au milioni kama unataka kwenda shule kakope bank.
  mawazo duni kabisa ulishazoeshwa kula kulala wewe, eti "mnajua tunahitaji wasomi kiasi gani" we unajua kuna wasomi wangapi mitaani hawana kazi?
  kama huna hela kalime kahawa kijijini kwenu, unajua serikali inahitaji wakulima kiasi gani? tunawahitaji sana nyie wakulima. lima miaka mitano changa hela ndo nenda kasome sio lazima umalize chuo ukiwa na miaka 25

  ReplyDelete
 32. Kazi ipo Bongo.Mie naona watu tunachanganya kati ya Mkopo na Udhamini.
  Ili watu watoe fact, kwanza tafuteni ule mkataba waliojaza hao wanachuo alafu na bajeti ya mwaka jana waliyopewa Bodi ya Mikopo.

  Alafu fany estimation ni wanachuo wangapi wanahitaji mkopo huo.

  ReplyDelete
 33. DAMN! pole zao sasa hao watakaoshindwa kupata hizo pesa watafanyaje.! Idadi ya madenti pale UDSM itapungua kweli!

  ReplyDelete
 34. Hivi ni kweli hii mikopo inatumiwa na wanafunzi kwa matumizi muhimu ya mwanafunzi.


  Watu wanataka kujenga kwa mkopo huo,kununua magari,kusaidia familia nk.Sasa jamani tutafika kweli.

  JK angalia ukweli wa mambo na fanya vitu kutokana na ukweli wa mambo.Najua wewe ni msanii sasa hawa watoto wa chuo sijui na wao wanataka kukuletea usanii wakighani wewe hujui.

  Mikopo itolewe kwa wasiojiweza.Ikiwa na maana wasiojiweza kweli kweli na si kama inavyotolewa sasa.

  ReplyDelete
 35. Kwa ufahamu wangu, mkopo haulazimishwi. Huwezi kumpangia mtu yeyote akukopeshe kiasi unachohitaji wewe, atakukopesha kwa kadri ya uwezo alionao na vipaumbele alivyonavyo. Mikopo wapewayo wanafunzi inazingatia uwezo wa serikali na vipaumbele vya taifa.

  Kama wanafunzi wanataka kukopeshwa 100% ya mahitaji, ningewashauri labda wajadiliane kwanza wakubaliane namna ya kupunguza wanafunzi chuoni ili wabaki wachache ambao fedha zilizopo zitawatosha, so watakaobaki wapewe hizo 100%. Ni mwanafunzi yupi yuko tayari kupungua chuoni aachie wenzake wasome? Basi ikiwa sote tunataka kusoma tuwe wazalendo tugawane kidogo kilichopo.

  Hili suala la kugoma kila mara tena kwa sababu zisizo na mantiki tumechoshwa nalo kabisa. Watu wenye matatizo Tanzania ni wengi tu, sio wanafunzi peke yao. Pesa zinazotolewa za huduma za jamii zinapaswa ziwafaidishe wote, si wanafunzi peke yao. Kwa nini wang'ang'anie 100% sponsorship bila kuwafikiria watanzania wengine wanaohitaji fedha hizohizo? Mbona wagonjwa mahospitalini wanachangia gharama za huduma za afya, wao nani atawasaidia kugoma ili watibiwe bure 100%? Kuna matatizo ya njaa, barabara, nishati, makazi, usalama, n.k, yote yanahitaji fedha. Mbona hawa vijana wanakosa uzalendo? Na hata hivyo serikali ilikwisha waahidi wawe na subira, hatua zinapangwa kuboresha hali iliyopo.

  Kwa maoni yangu, vijana hawa wamekosa hekima na tena hawana adabu. Huwezi kumlazimisha anayekukopesha akukopeshe hela yote unayohitaji. Kopa kiasi kwake, nyingine jazia kutoka kwa mkopeshaji mwingine au kutoka vyanzo vyako vingine vya mapato. Na la zaidi, ni ukosefu wa nidhamu uliokithiri kumpa Rais wa Nchi ultimatum, ati atoe majibu ndani ya siku mbili! Wewe ni nani? Rais wetu yuko kushughulikia matatizo ya wanafunzi tu? Au hilo lilikuwa na dharura gani hadi likashindikana kusubiri?

  Huu ni ulevi wa madaraka ya kitoto, mtu anachaguliwa kuwa rais wa wanafunzi, nafasi ya mwaka 1 tu, basi anajiona naye ni Rais kama Mh Kikwete, anaweza kumtishia hata Rais wa Nchi! Anampa ultimatum! Uchuro kabisa huu! Rais wa wanafunzi ni mwanafunzi, na urais huo unakoma anapokoma uanafunzi. Waelewe hivyo. Waache kuyumbishana wanafunzi kwa kutumia vyeo feki hivyo na kudanganyana ati "solidarity", hakuna solidarity hapo wakati huna cheti! Subiri upate cheti (degree) ndipo utaweza kumsumbua mwajiri wako kwa masharti kwa sababu atakuwa anahitaji utaalam wako. Sasa hivi huna utaalamu wowote unabwabwaja ati "solidarity"! Utaula wa chuya kwa uvivu wa kuchagua!

  Nashauri UDSM wachambue vizuri wale waliosababisha fracas hii wapewe adhabu ya kukomesha kabisa. Wakomolewe kabisa hao, wala siwatetei ng'o! Uongozi uwe tu makini wasije wakaumiza wale wasio na hatia.

  Kuhusu haya masharti mapya mie naona safi sana, kwanza wameyataka wenyewe hao wanafunzi. Nasema University ikaze uzi, masharti ndio hayo, naunga mkono kabisa na naomba serikali isimamie hilo. Hakuna jipya hapo, kwani hata wagonjwa hospitalini wanalipia gharama, sembuse hao wazima kabisa! Walipe hizo hela. Kama kweli yupo asiyeweza kulipa, abaki kwanza nyumbani tuone wangapi wanaweza tuendelee nao kwa kipindi hiki, tena itasaidia kupunguza fujo. Hao watakaoshindwa kabisa watafutiwe mpango wa kuwasaidia (mfano kama kampeni za michango mbalimbali n.k) na fedha zikishapatikana ndipo waitwe chuoni. Hata watoto wanaopelekwa kutibiwa India, ni fedha zinachangwa kwanza zikishatosha ndipo wanapelekwa. Tufanye hivyo kwenye elimu pia. Pesa mbele, hakuna huduma inayoweza kupatikana bila fedha.

  Nasema tu poleni sana lakini mmevuna mlichopanda.

  ReplyDelete
 36. michuzi nimeogopa kumbe ya zamzni hii 2007 we mkali kichwa kinauma du

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...