mchungaji christopher mtikila akifafanua jambo leo juu ya mojawapo ya kesi kadhaa alizofungua

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 35 mpaka sasa

  1. hehehehehe..hizo simu mbili zilizopangwa hapo si mchezo

    ReplyDelete
  2. mchungaji kwa kesi tu anaongoza, kila siku yeye tu anaonewa na mwenzake lyatonga ,,duuuuuuhhh

    ReplyDelete
  3. mchungaji una vimeo vya nguvu hahahaaa!!

    ReplyDelete
  4. Sir Issa Michuzi huyu Rev... offisi yake imejaa makaratasi, sijui ana recycle bin...? Hivi hizi kesi anashindaga...?

    ReplyDelete
  5. hawa ndo watu maarufu bongo wanajulikana kila kona, cheki hali yao. ndo unaniambia mi nirudi bongo?

    ReplyDelete
  6. Kesi anazofungua Mchungaji Mtikila zina manufaa kwa wananchi wote (ukiacha zile zinazohusu haki yake binafsi. Kwa ajili hiyo si vema kumlaumu au kumfanyia kebehi. Mtikila anastahili kutiwa moyo, pongezwa na kuungwa mkono.

    ReplyDelete
  7. Mtikila amefanya makubwa.Moja ambalo sitasau ni Zanzibar tulikuwa tukienda na Pasipoti.Sasa Mtikila akaambiwa asajili wanachama wa Chama chake Zanzibar ili asajiliwe,Akagoma akasema hawezi ingiza kwenye chama chake Raia wa nchi nyingine(Zanzibar) ambako unaenda Kwa Pasipoti wawe wanachama wako.

    Matokeo yake kwenda Zanzibar kwa Pasipoti kukafutwa.

    Pia amesimamia suala la wagombea Binafsi kuwa ni haki ya mtu kikatiba na akashinda ni serikali tu ndio wanafanya kuchelewesha lakini hili litaiingiza nchi pabaya kwa kuwa sehemu isiyoheshimu haki za binadamu na kudharau katiba na maamuzi ya mahakama.Serikali inawajibika kuheshimu katiba na mahakama.

    Ukiona serikali inaanza kudharau katiba na maamuzi ya mahakama ujue inaanza kuwa ya madikteta.

    Kitendo cha kutoruhusu wagombea binafsi tayari kimeshaanza kuipaka matope serikali ya Kikwete chinichini kwenye duru za watetezi wa haki za binadamu kimataifa.Watu wameanza kulivalia njuga hilo suala na wanasafiri ndani na nje wakitumia kama kitu cha kuonyeshea ushahidi wa wazi wa udikteta wa Kikwete ambao kaanza kuujenga kichinichini kwa kukanyaga katiba na maamuzi ya mahakama.

    Lingine ambalo limeanza kuipaka matope Tanzania ni lile la Kesi ya Ditopile.Ndio maana Mtikila ameanza kulivalia njuga.Limeanza kutumiwa nje ya nchi kuonyesha jinsi majaji wa Tanzania walivyo dhaifu kiutendaji kwa kutochukua hatua yoyote wakati Ditopile aliidharau mahakama kwa kupita mlango wa majaji.Na wanatoa vielelezo vya watu waliodharau mahakama na wakafungwa.Kesi ya Ditopile imeidharaulisha fani ya majaji wa Tanzania.Watu nje wanaanza kuwaona kama siyo Competent.Na hii inaharibu CV zao na fani ya Ujaji Tanzania.MajajiWasishangae baadaye wakiomba post za kisheria nje ya nchi wananyimwa nafasi za ajira za maana au nafasi za maana kutokana na kuharibiana CV kulikofanywa na kesi hii ya Ditopile.

    Ni vizuri majaji wawe serious na CV zao Zisiharibike.Wajue kuwa kesi yoyote yenye high public attention inaweza ua CV au ikawajenga sana.Inaonekana majaji bado hili hawajaliona vizuri.

    Hizi kesi Mtikila anazofungua na kushinda haziishii kwenye milango ya mahakama tu zinaenda mbali sana.Hata kama serikali haitaki kuchukua hatua.Mtikila si mjinga mjinga kama wengine wanavyomdhania.

    ReplyDelete

  8. Dakika 30 zilizommaliza Mtikila


    Dakika 30 zilizomwachia
    majonzi makubwa Mtikila
    *Majaji 'wakwepa' suala la mgombea binafsi
    * Hata hivyo wamuunga mkono kwa 90%
    *Hukumu imeibua maswali zaidi kuliko majibu

    Na Hassan Abbas

    MWANAHARAKATI mashushuri wa masuala ya kisiasa na haki za binadamu, Mchungaji Christopher Mtikila, juzi alionja chungu ya kushindwa kesi ikiwa ni mara wa kwanza tangu alipoanza harakati zake kupitia mahakama mwaka 1993.

    Katika shauri hilo la juzi, Mtikila pamoja na mambo mengi alikuwa akiitaka Mahakama Kuu ya Tanzania, izuie kufanyika uchaguzi mdogo wa jimbo la Tunduru, Ruvuma lililobaki wazi baada ya aliyekuwa mbunge wake, Juma Akukweti kufariki dunia.

    Kama ilivyoandikwa na vyombo vya habari jana, Mtikila amekumbwa na kipigo cha kwanza katika harakati zake, tunapozungumzia kesi za kikatiba alizokwishazifungua.

    Makala hii inajaribu katika lugha rahisi na hoja zisizotumia nguvu, kuipitia hukumu hiyo na kuona ni kwa nini Mtikila alishindwa na maswali magumu ambayo yanabaki bila majibu.

    Watu wengi waliokuwepo Mahakama Kuu, juzi, Ijumaa,
    saa saba kamili walikwishakuwa wameingia mahakamani tayari kuwasubiri majaji walioongozwa na Jaji Chande Othman, Jaji Robert Makaramba na Jaji Amir Mruma.

    Mchungaji Mtikila akiwa na wakili wake, Bw. Mpale
    Mpoki, waliwasili punde kidogo huku Mtikila akionekana mwenye bashasha kama ilivyokuwa kawaida yake; Hakujua dakika 30 tu baadaye angepatwa na mstuko wa aina yake.

    Baada ya mahakama kutulia, Majaji waliingia na hukumu hiyo haikutumia muda mrefu. Takriban dakika 30 hivi zilitosha.

    Jawabu laanza kupatikana


    Jaji Chande ndiye aliyeanza kwa kuisoma hukumu
    hiyo kwa niaba ya jopo la majaji wenzake.

    Kabla sijaanza kuziangalia sababu zilizomfanya Mtikila kuondoka kichwa chini niseme tu kwamba, kwa karibu robo tatu ya muda ambao Jaji alikuwa akisoma hukumu ile, kila mtu alishaamini Mtikila angeondoka na kicheko. Kumbe lo!

    Mahakama ilianza kwa kujibu hoja ya mawakili wa Serikali kwamba haina nguvu za kisheria kusikiliza suala hilo. Hoja hiyo ilishakuwa imejibiwa awali lakini mahakama ikawa ikiipitia kwa haraka haraka tu katika kujiridhisha zaidi.

    Katika hoja hiyo, jopo la majaji lilikubaliana kwamba mawazo hayo ya mawakili wa Serikali ni dhaifu mbele ya sheria.

    Wakasema Mahakama Kuu ina uwezo usio na ukomo (exclusive jurisdiction) na pia uwezo wa kihistoria (inherent jurisdiction), katika kusikiliza mashauri mbalimbali ya madai yakiwemo yanayogusa haki na wajibu mbalimbali wa raia.

    Mahakama ikaunga mkono hoja za wakili wa Mtikila aliyekuwa amesema kwamba uwezo wa mahakama hiyo katika shauri hilo si jambo la kuhojiwa kwani unajulikana kisheria na kamwe hakuna mtu anayeweza kuupoka.

    Wakisisitiza juu ya hilo majaji walinukuu vifungu vya 4, 8(1)(d) na 13 vya Sheria ya Kufungua Mashtaka ya Haki za Msingi (The Basic Rights And Duties Enforcement Act) ya mwaka 1994.

    Sheria hiyo kwa kifupi inaipa uwezo Mahakama Kuu, kusikiliza mashauri yoyote yanayogusa uvunjaji wa haki za kikatiba. Mpaka hapo Mtikila akawa amepata ushindi wa kwanza.

    Kutoka hapo ndipo Majaji walipoanza kuangalia kwa kina maombi ya kutaka Mahakama itoe maagizo kuwa uchaguzi mdogo wa Tunduru unaofanyika leo usimamishwe.

    Mtikila alikuwa na hoja mbili kuu katika suala hilo. Mosi alidai kwamba Mahakama Kuu ilikwisharuhusu wagombea binafsi, hivyo kufanyika uchaguzi huo bila wagombea
    hao kushiriki ni kuvunja haki za kikatiba za baadhi ya Watanzania na ni ubaguzi unaopingwa na katiba ya nchi.

    Pili alijenga hoja kwamba katika jimbo la Tunduru kuna wakazi wapatao 11, 552, ambao hivi sasa wana umri wa kupiga kura lakini watanyimwa haki yao hiyo kwa sababu tu hawakujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, kutokana na wakati huo wao kuwa chini ya umri uliokuwa ukiruhusu kujiandikisha kwa ajili ya kupiga kura.

    Kisheria aina hiyo ya maombi ni ya kutaka amri ya mahakama (Interim Injunction) ambazo ni utashi wa mahakama (prerogative orders) ili kuweza kuzuia jambo lisifanyike.

    Ili mahakama ikubali kutoa amri kama hiyo, hata hivyo huwa kuna vigezo vitatu vya kisheria vinavyopasa kuangaliwa.

    Vigezo hivyo viliwekwa siku nyingi na Mahakama Kuu katika shauri maarufu la Atilio Mbowe na baadaye kukaziwa zaidi katika kesi ya Glaxo Group Limited v Agri-Vet Limited.

    Katika hilo, kwanza mahakama inatakiwa kujiuliza Je, kuna kesi ya msingi ambapo mlalamikaji ana uhakika wa kushinda?

    Pili, ni je, kwa kutolewa amri hiyo nani kati ya mwombaji (Mtikila) na mjibu maombi (Serikali) angeathirika zaidi na tatu ni je, kwa kuangalia uwiano wa hasara na usumbufu unaotokana na ombi kutekelezwa, nani angeathirika zaidi.

    Mtikila aonja tamu na chungu

    Katika kujibu maswali hayo, Mtikila aliongoza kwa kupata alama zinazoweza kufikia 90 kati ya 100, lakini hata hivyo mshindi hakuwa yeye kama ilivyotarajiwa na watu wengi!

    Ikijibu suala la kuwepo kesi ya msingi, Mahakama Kuu ilisema kesi ya msingi ipo, ingawa haijazipitia sana hati
    za mlalamikaji, lakini suala linalohojiwa ni la kikatiba
    kwa mujibu wa sheria. Hapo Mtikila akachukua pointi.

    Katika suala la nani hasa angeathirika kwa kutolewa amri ya kuzuia uchaguzi, mahakama ikasema ili kuamua hilo, idadi na ukubwa wa namba haupaswi kuangaliwa katika kupima athari.

    Mahakama ikasema kwamba kuna watu 11,552 tu ambao mlalamikaji anaeleza kuwa watakosa haki yao ya kikatiba ya kupiga kura dhidi ya mamilioni ya waliokwishajiandikisha.

    Ikaendelea kusema watu hao ni idadi ndogo ikilinganishwa na wale ambao wamejiandikisha, lakini Jaji Chande akaonya na kuonekana akimpa ushindi mwingine Mtikila, kwa kusema:

    " Watu hao (11,552) kwa uchache wowote unaoweza kuonekana nao wana haki ya kikatiba na kwa mujibu wa sheria za uchaguzi kupiga kura. Haki hiyo haiwezi kuthaminishwa kwa thamani yoyote ya pesa."

    Mtazamo kama huo, majaji waliutumia kujibu sehemu ya kwanza ya hoja ya tatu ambapo pia walikiri kwamba thamani ya haki ya mtu huwezi kuikadiria kwa kutumia kipimo cha pesa.

    Mpaka hapa ikawa dhahiri kuwa Mtikila alikuwa anaelekea kusimamisha uchaguzi wa Tunduru. Nini kikamsibu sasa?

    Hapa ndipo ulipo ugumu wa taaluma ya sheria, taaluma ambayo, wapo ambao wanasema huwezi ukawa na uhakika
    na haki yako, isipokuwa tu mpaka pale, Jaji/Hakimu atakapotamka sentensi ya mwisho. Ndivyo ilivyojitokeza.

    Mwisho mchungu kwa Mtikila

    Baada ya kuona kwa karibu asimilia 90, hoja zake zimethibiti kuliko zile za Serikali, bila shaka si yeye tu Mtikila, bali wengi tuliokuwepo mahakamani mle, mioyo ilikuwa ikijisema: " Mtikila sasa anaweka historia nyingine."

    Hali haikuwa hivyo, neno "LAKINI" ndilo neno lililoubadili upepo na kufanya mapinduzi makubwa katika uamuzi wa kesi hiyo.

    Hali hiyo ilikuja baada ya Jaji Chande kuanza kuangalia upande wa pili wa watu wengine ambao uamuzi wa mahakama ungewaathiri (kisheria wanajulikana kama third parties).

    Wakiliangalia hilo majaji, walisema tayari kuna wagombea wa vyama ambao wamekwishaanza kampeni zao na ambao hawakuweza kusikilizwa mahakamani hapo(hakuwashirikisha).

    Ikasema inatambua haki na gharama ambazo wameziingia katika kujiandaa na uchaguzi huo kisha ndipo ikaja
    sentensi ya mwisho iliyokuwa fupi lakini nzito ikisema:

    " Kwa kuzingatia hayo tumeyatupilia mbali maombi haya."

    Maswali magumu

    Wachunguzi wa masuala ya sheria hata hivyo wanasema hukumu hiyo, ambayo Mtikila ameahidi kuitumia kufungua kesi nyingine ya kubatilisha uchaguzi utakaofanyika, imeacha maswali magumu na mengi zaidi katika maendeleo ya demokrasia hapa nchini.

    Kwanza haikujibu hoja ya wagombea binafsi ni ruhusa kushiriki chaguzi ndogo au mpaka uchaguzi mkuu ujao?

    Hilo Mtikila, akizungumza na gazeti hili jana alisema bayana kuwa bado linamfanya aweweseke.

    " Tumeshangaa mahakama kutoijibu hoja hiyo. Wakati wa kujenga hoja (submission) tuliitetea, hatukuwa tumeiondoa. Mimi mpaka sasa sielewi nini kimetokea," alisema.

    Pia hukumu kati ya maswali mengi iliyoyaacha ni lile la kama imetambua na kukubali kuwa wale watu 11,225 wasipopiga kura haki zao za kikatiba zitakuwa zimevunjwa tena kwa hasara ambayo haiwezi kuthaminiwa kwa thamani yoyote
    ya pesa, ni upi basi utakuwa uhalali wa uchaguzi huo ?

    Hoja ya mwisho kwa leo ni je, ni ipi nafasi ya mahakama katika kulinda katiba isivunjwe hasa inapokuwa imebaini kuwa kwa kitendo cha watu 11,552 kuzuiwa kushiriki uchaguzi huo, haki za msingi zinakuwa zimekiukwa?

    Kwa hoja hizi ni wazi hukumu hii ya Mtikila kimsingi, wanaharakati wengi, wanasema, imeibua changamoto zaidi kuliko wachache wanachokiona kuwa ni Mtikila kushindwa.

    source :Majira

    ReplyDelete
  9. watanzania wenzangu serikali yetu inahitaji watu kama mtikila, kama unamfuatilia vizuri utagundua kesi zake zote huwa ni za msingi na mantiki, kwanza huwa hakurupuki lazima apitie kwa wanasheria zaidi ya watatu na pia kupata maoni ya maprofesa chuo kikuu ndipo aenda mahakamani i like the gy's guts. he is strong and brave tanzania needs challenges to move on and to correct our system!

    ReplyDelete
  10. We annon unayesema Mtikila kachoka na kwa hiyo utaki kurudi kwenu nakushangaa sana! Ulivyokaa huko uliko unadhani nani kakufanya kuwe kama hivyo?!
    Acha upuuzi, njoo kwenu ujenge nchi na si kubebabeba ma-box na kujifanya mambo yenu yako fresh! Hao wanaodai kuwa mambo yao fresh hivi huwa wana maana gani? Huku sisi tunawaona dada zao na mama zao na baba zao wakiwa hoi bin taabani! Sasa hayo mambo kuwa fresh ndiyo maana yake nini?!

    Rudi kwenu. Usiangalie magari ya watu huko na nyumba nzuri ukadhani zilishuka kutoka mawinguni!

    ReplyDelete
  11. Kwa hakika huyu ndo mwanademokrasia hasa na ninamhakikishia anaonymous hapo juu kwamba huyu jamaa kesi anazopeleka mahakamani si sababu ya matakwa yake ukienda kwake ndo utajua watu wanampelekea yaani kiufupi angekuwa na uwezo angeanzisha NGO ya kuendesha kesi.

    ReplyDelete
  12. anon 4:52 am wewe kurudi bongo sio kwa sababu hali za watu kama Mtikila zinafkufanya usije bali huna NAULI ya kurudia, mabox unayobeba hayalipi kukufanya usevu nauli pamoja na kwamba unakaa ghetto watu 15.Mbona ulishindwa kuja kwenye msiba wa babaako?

    ReplyDelete
  13. Naungana na anony wa hapo juu ni Rev peke yake ambae kasikilia patriotism ya kibongo huyu kwa macho ya wengi ni msaliti lakini kwa wachache wanaoheshimu utaifa,haki kwa wote na wapinga rushwa,huyu mzee ni shujaa na mfano wa kuiigwa.Watu kama hawa wanahifadhiwa vizuri huku ughaibuni kwani wao ndio wenye uwezo na nguvu za hoja zinazolinda maslahi ya wazawa hivyo kuwanyima ulaji wahamiaji kwa vipigamizi vya mabungeni.

    ReplyDelete
  14. we anony wa Wednesday, April 04, 2007 4:52:00 AM, Mchungaji Mtikila ni "mtetezi wa wanyonge" kwa hiyo anajitahidi kuishi by his brand. Sio mwanamuziki au mfanyabishara huyo, ndio maana yuko simpo. Haimaanishi kwamba ni "mlalahoi" kama anavyoonekana.
    Anyway uchunguzi zidi unahitajika. Mwenye ripoti kamili kuhusu huyu Mchungaji atupatie.

    ReplyDelete
  15. Watu wa ughaibuni inaonekana hamfuatilii mambo ya huyu mchungaji! Kwa kweli ana asili ya kutaka haki sana huyu bwana, na hata kesi hiyo inayotajwa hapo amefungua kwa ajili ya wengine. hebu fuatilieni sana mambo yake mtaona jinsi alivyo mtaifa. kwa kweli nampa sifa nyingi sana huyu bwana. Acheni kuangalia simu zake mpeni sifa zake.
    Kama kuna mtu anafaa kupewa nchi hapa tz ni Mtikila sijaona mwingine.

    moshi

    ReplyDelete
  16. Watu kama Mtikila ni Muhimu sana ktk Nchi corrupt kama TZ.
    huyu jamaa nadhani sirikali inapoplan kufanya vitu vya utumbo huwa inamfikiria kwanza huyu jamaa ata-react vipi? Anasaidia sana kutetea maslahi ya wanyonge pindi mambo yanapoenda Ndivyo sivyo...

    ReplyDelete
  17. Wengi wa wachangaiaji katika blog hii huwa hawasomi wanachostahili kuchangia.wakati wote wanakimbilia kuhitimisha mambo kwa lawama au kuonyesha kabisa upeo wao ulivyo kidogo.

    ukitaka kugundua au kufahamu mawazo ya watanzania walioko nje ya nchi hawana busara jaribu kusema kuwa huko mnafanya kazi gani? watatukana matusi yote na hata ya nguoni.Mimi pia niko nje ya Nchi na tena Europe ukweli maisha ya huku ni magumu huu ni ukweli.

    wengi wetu huwa hatupendi kuusema ukweli kwani siku zote tunataka kuonekana kuwa tuko katika matawi ya juu tu.na hii ndio kazi ya watanzania sifa sifa sifa hatakama sifa haistahili yeye anaweka sifa tu.

    Mtikila anapigana vita iliyokamili mtikila na upeo wa kuona mambo angalia ameshinda kesi nagpi na ana hoja kimsingi kabisa katika jamii.

    ReplyDelete
  18. Watu kama huyu ni muhimu sana kwenye nchi iliyojaa na woga kama TZ. Watu wanamambo mengi yanawakera ila wanaogopa kuyatamka hadharani ama kwa kuhofia nafasi zao za ulaji au maisha yao. Huyu mwanaume wa shoka haogopi mtu na kila siku yupo strong na utashi wake uwe mzuri au mmbaya. Mi namkubali kwani anafanya nchi ioekane ya kidemocrasia zaidi na kuwapa ujasiri wale wanaoogopa kutetea haki zao.

    ILA BWANA MKUBWA ILE KESI YA KUUWA BILA KUKUSUDIA ALIYOISHIKIA BANGO IMEISHIA WAPI AU ALIVUTWA PEMBENI AKAPEWA MRAHABA? ATULIZE MZUKA, MAANA INATIWA WASI WASI ZAIDI YA WIKI SASA NAE ALISEMA WIKI HAIISHI ATAKUWA AMETUMIA KIFUNGU CHA KATIKA KUIBADILI JINA. EBU AFAFANUE HAPO KUNANI?

    ReplyDelete
  19. Mzee wa shoka huyu unajua kuna kinywaji fulani kikali yaani ukipata hukui muda stimu imepanda walikibatiza jina ''Mtikila'' kwa kudhamini makeke ya mchungaji

    ReplyDelete
  20. Akifa huyu atazikwa kitaifa, maana serikali itapumzika na kushukuru. Ila nadhani hana "system", yuko kivyake vyake, kwa hiyo wanampuuzia, otherwise angekuwa Segerea huyu ili kulinda usalama wa wenyenchi (wananchi, sorry).

    ReplyDelete
  21. kwanza wewe unayesema watu wanaokaa juu maisha ni magumu ila hawasemi ukweli...thats flat bogus na huna tofauti na wapika majungu,OK lets go back to the topic....Mtikila anafanya kazi nzuri lakini tatizo lake is too much extremist ambacho ni kitu hatari sana katika nchi na dhambi yake kubwa amabayo wengi hawatamsamehe ni pale alipoanza ubaguzi wa wazi wazi kisiasa juu ya wahindi ambao wengi wao ni watanzania asilia kabisa na kuwaconvince wafuasi wake wahindi ni wezi na kilichotokea walianza kupigwa mawe mitaani na kuitwa majina ya kashfa kama magabachori,kwa wenye akili walimdharau sana na alifanya kitu hatari sana na hakuishia hapo maana alianza kufingerpoint watu wanaotoka mikoa ya border kama waha na wahangaza sio watanzania...it was so bad mpaka watu wengi wakaanza kuishi kwa wasiwasi kwa ajiri ya upuuzi wa huyo jamaa,anyway sio yote anyofanya mabaya lakini akili yake ya kibaguzi kwa kutumia jina la uzawa is a very dangerous game ambalo linaweza kucost ile nchi big time

    ReplyDelete
  22. nadhani hata huyu BUBERWA ana undugu wa akili na Mtikila

    ReplyDelete
  23. Mtikila nimeanza kumsikia nikiwa form 2, 1991 pale kazima secondary kipindi hicho tukisikia mpinzani tunamuona kama adui wa nchi. Ili upate A kwenye somo la siasa lazima ukariri katiba ya chama. Kwa kweli nilimchukia kutokana na kupandikizwa katiba na fikra za mwenyekiti. lakini kadiri nilivyokuwa nakua na kupata akali ya upambanuzi nimekuja gundua kuwa mtikila anastahili kuingizwa katika historia ya nchi yetu katika suala zima la kutetea haki za wananchi. nakumbuka aliisha wahi kusema alipokuwa jela hakuona gabachori hata mmoja, akimaanisha wenye nazo, mambo ambayo sasa hivi tunayaona dhahiri baada ya kujificha kwa muda mrefu.

    mtikila kafanikiwa kubadili mawazo yangu yaliyonifanya nipate A ya siasa form 4, na kuona kuwa haki ni kitu cha msingi katika kuendeleza utaifa na usalama wa Tanzania kuliko kupata A ya kukariri katiba

    Mtikila anapofungua kesi anapigania utaifa na usalama wetu, japo vyombo vya sheria vinamuangusha kwa kufanya maamuzi yao kisiasa (e.g kesi ya kupinga uchaguzi wa mwezi uliopita).
    mchungaji nakutakia maisha marefu na yenye afya ila usichoke na harakatu zako, wengi tupo na wewe.

    ReplyDelete
  24. Ni Heri Rev Mtikila aneyepiga kambi mahakamani kutetea kunndwa katiba ya kweli, kuliko wanasiasa wengine wa kambi ya upinzani wanaoshinda kuota Ikulu na Ubunge.

    ReplyDelete
  25. MAONI YALIYOTOLEWA NI MENGI MNO NA YAMELALIA UPANDE WA HALI ILIVYORIPOTIWA.
    MIMI BINAFSI SINA TATIZO NA MCHUNGAJI, ISIPOKUWA IPO HAJA KWA WANAZUONI WETU KUANZISHA KOZI MAALUMU ZITAKAZO WAFANYA WAHITIMU WA-SPECIALIZED KATIKA MAENEO KAMA SIASA ZA NDANI, VIONGOZI WA KITAIFA NK
    HII ITASAIDIA WANANCHI WENGI KUJUA HATA TABIA ZA VIONGOZI WA ZILE NZURI NA HATA MBAYA.
    HEBU TUJIULIZE KATIKA COMMUNITY ZETU REVEREND ANAJISHIRIKISHA NA AKINA NANI? JE KATIKA WATU ANAOSHIRIKIANA NAO, WANAMWELEZA KUWA NI MTU WA NAMNA GANI?
    JE, TUNAJUA KIVIPI ANAITWA MCHUNGAJI? JE HUYU MCHUNGAJI ANA KANISA LOLOTE ANALOONGOZA KWA SASA?
    JE, HUYU NDUGU ANAJIKIMU VIPI MAISHA YAKE KWA MAANA ANAFANYA SHUGHULI GANI ZINAZOMUINGIZIA KIPATO?
    KAMA HUMJUI HUYU MCHUNGAJI BASI JITAHIDI UMFAHAMU KABLA HUJAKUWA DISSAPOINTED, HE IS NOT AS YOU THINK.

    ReplyDelete
  26. wether ameshinda au hajashinda ni mtz pekee mwenye kujiamini kwa hali ya juu sana asiyetaka kunyanyasika watz wengi kazi kupepeta midomo chinichini kila wakati na kulalala mika kusikoisha hamna hata step moja wanachukua huwa kila wakati najiuliza huyu Mtikila ni mtz kweli? maana hana damu za kiuoga oga kama za watz niliowazoea bora ya sie wachache tunaojinganya huku ughaibuni tunafunguka macho na kujua kumbe kuna sulala linaitwa HAKI YA MTU...na kwamba ukiisimamia kila mtu atakuheshim mnatucheka tunabeba mabox lakini tunapanuka sana kimawazo.

    ReplyDelete
  27. Suala la Mtikila ni nani kidini halina maana yoyote.Mtu ana uhuru wa kuabudu chochote na kuabudu popote iwe kwenye dini iliyosajiliwa au isiyosajiliwa na aweza abudu mti,ngedere,Shetani,kenge,mtu alye hai au aliyekufa,au akajiabudu mwenyewe n.k na aweza akaabudu kwenye jengo,Msituni,Kaburini,kwenye baa,na hata aweza abudu hata chooni kwenye mavi ili mradi anafanya hivyo kwa hiari yake bila kulazimishwa na mtu akiwa anatekeleza uhuru wake wa kuabudu.

    Kwa uhuru huo huo mtu aweza tumia vyeo vyovyote vya kidini aweza jiita au mwita mtu mwingine kwenye dini yake ,shehe,Profesa,Imamu,kafiri,Maruhuni,Mchungaji,Papa,Kenge,shetani,n.k.Vyeo vya kidini haviko katika katiba ya nchi hivyo huwezi zuia mtu ajiite nani kidini.Ndio maana tuna hadi akina Profesa Maji Marefu ambao si maprofesa wa vyuo vikuu bali ni waganga wa kienyeji.Mtu anaweza akawa peke yake akisali yeye na hawara yake na akijiita Imamu au Askofu.Huwezi kumshitaki au kumzuia eti hana waummini.Inawezekana imani yake inatambua kila anayesali kwenye hiyo dini kuwa ni Imamu au askofu.
    Idadi ya waumini siyo issue katika uhuru wa kuabudu na mtu kujiita chochote kidini.

    Kuna dini hazina mpango wa kuwa na waumini wala majengo.Mfano wanga wa imani za uchawi na wapenda imani za matambiko makaburini,husali kila siku makaburini lakini hawana mpango wa kujenga majengo ya kuabudia wala kusajili dini zao na wala serikali haiwaingilii sababu serikali sio masheikh au mapadri wa kuelekeza watu wasali wapi,wasali vipi na eneo gani.

    Suala la Mtikila anaishi vipi yule ni mpigania demokrasia.Hata wewe ukijitokeza kufanya yale anayofanya mtikila hata mimi nitakupa hela hata bila kuniomba.Tunapenda watu wajasiri kusimamia haki za watu kama Mtikila.

    Mtikila sasa amekuwa kama Taasisi anajulikana kila kona ndani na nje

    ReplyDelete
  28. We annon hapu, sisi huwa hatuwacheki wala kuwabeza Watanzania waliopo majuu. Ila tunajaribu kuwafanya mkumbuke kwenu. Kubeba ma-box ni moja ya kazi kama zingine. Ila tatizo la wenzako huwa wanachonga sana na kutamba bila sababu za msingi. Unaweza kudhania kuwa kukaa majuu ni bora kuliko TZ. Kwa kufanya kazi nje ya nchi pia mnapunguza msongamano usio na maana kwenye nafasi za ajira chache nchini. kaeni huko huko tu.

    Tukurudi kwa Mtikila, ni kama ulivyosema, huyu jamaa hana aibu, pia ana confidence mia! KWa kweli wabongo wengi wangekuwa hivi, nchi hii usanii usio na maana wa wanasiasa ungekoma kabisa! Lakini ni suala la time. Mambo yatabadilika tu.

    ReplyDelete
  29. Dini za kutoka nje ya Nchi zenye matawi yake nchini hazitusaidii kupata haki za kikatiba sana sana zinatuongezea matatizo.Hongera Mzawa Mtikila mwanzilishi wa kanisa la kitanzania.

    Hivi nauliza dini za kutoka nje zina matatizo gani?

    Mimi naona Dini za kutoka nje ya nchi zina mashetani maana zimechangia kuongezea matatizo ya Mwafrika.

    Mfano Waafrika wa makabila tofauti walikuwa na dini tofauti kufuatana na kila kabila lakini hata siku moja huwezi ona mtu wa kabila hili mwenye tofauti ya kidini ya kikabila na mwenzie wakigombana au kutukanana kuwa dini ya nani bora kuliko ya mwingine.

    Lakini toka hizi dini za wakoloni toka Uarabuni,Ulaya na Marekani Za Uislamu na Ukristo ziingie, ugomvi Afrika kwa waafrika haushi.

    Waislamu na Wakristo hawaivi.Wanatukanana na kudharauriana waziwazi ndani ya madhehebu ya Uislamu na Ukristo na kati yao.

    Wakristo Wenyewe vita ni kali mno wao kwa wao.Wakatoliki hawaivi na walutheri,Anglikana,Pentekoste n.k

    Vita kati ya Ukristo na Uislamu imetoka Uarabuni,Ulaya na Marekani imehamia Afrika.Sasa watu wanashindana kidini kila moja akijiona bora kidini kuliko mwingine na anatangaza ugomvi na wenzie.Amani kati ya waafrika hakuna.Kila kona kuna vita kuanzia mihadhara ya usiku kucha hadi kugombea vyeo vya nchi hadi kupigana risasi mfano Nigeria na Sudan.

    Dini hizi za kutoka nje ya nchi (Uislamu na Ukristo) Ni dini za Mungu kweli hizi? Mbona hazina uvumilivu kama dini zetu za asili ambazo watu walikuwa hawagombani pamoja na tofauti zao za kuabudu kikabila?

    Mimi naona hizi dini za kutoka nje ya nchi ziwe za Kiislamu au Kikristo zina Mashetani kabisa.Maana unakuta kila mtu akishaziamini tu dini hizo za nje kwa moyo wake wote mashetani ya ugomvi na dharau yanampanda.Anakuwa na dharau dhidi ya waumini wa dini zingine au kwa wale wasiokuwa na dini yake na anakuwa mkorofi na mgomvi asiyependa watu wa dini nyingine iwe kwa wazi au kwa siri.

    Iko haja watanzania tuanzishe dini zetu wenyewe hata kama ni za Kiislamu au Kikristo ziwe za hapa hapa zinazolingana na mazingira yetu pengine zitatusaidia kupata haki zetu za kikatiba na kupunguza ugomvi kati ya waafrika hasa ule utokanao na maruhani na mashetani ya dini toka nje yanayotugombanisha na kutufanya tudharauliane kiimani na kugombana.

    ReplyDelete
  30. Mheshimiwa Kaka MIchuzi na blog yetu ya nguvu. Naomba upokee mawazo ya Watanzania waishio huku kwa Mzee wa Vita a.k.a Kichaka kama siyo american worst BUSH.

    Kuhusu simu za mshindi za Mchungaji Mtikila naomba nimshauri kama anayo address inayoeleweka tutamtumia simu zenye kamera, ndogo na zinazoenda na wakati huku Watanzania huziita AISHA MADINDA.

    Pia naomba kuwakilisha rasmi kuwa simu zenye kamera hata huko nyumbani ziitwe AISHA MADINDA.

    ReplyDelete
  31. WEWE ANOMY KABLA YA 'mtaka cha uvunguni' ULIONAO NI USHABIKI NA UWEZO TU WA KUTUMIA KEYBOARD. LAKINI UNASHINDWA KUPAMBANUA NA KUJIBU MASWALI AU KUJENGA HOJA. NA HILI NDIYO TATIZO KUBWA LA BAADHI YENU. HAMTAKI KUUMIZA VICHWA VYENU KUZALISHA HABARI AU MASUALA MBALIMBALI. SIKU ZOTE MNATEGEMEA KULISHWA HABARI, THEN KILA MTU HUJIFANYA FUNDI WA KUCHAMBUA AU NDIYO ANAJUA ZAIDI YA HATA ALIYEANZISHA HABARI YENYEWE. UKITAKAKUHAKIKISHA HILO HEBU CHAPISHA WASIFU WA MCH. CHRIS.

    ReplyDelete
  32. Wengi wanahangaika na kupoteza muda bure kufikiria eti Mtikila ni mfuasi wa dini ya uongo.

    Watu wengi duniani wanasumbuka na sawali la Dini ipi ya kweli na ipi? Na Dini ya uwongo ni ipi?

    Jibu ni rahisi.Dini isiyo yako ndiyo ya uwongo na dini yako ndiyo ya kweli.Sababu mafundisho yasiyo ya kidemokrasia ya kidini hufundisha kuwa dini uabuduyo ndiyo ya kweli na zingine zote ambazo si zako ni za uwongo na za matapeli,mashetani na wapenda pesa!! Hivyo kwa Mwislamu,Ukristo ni dini ya Uwongo na utapeli na kwa Mkristo huona kuwa Uislamu ni Dini ya Uongo na utapeli vilevile.

    Na vita hizo huendelea ndani ya vidhehebu ndani ya kila dini.Kila kipande cha dhehebu kilichoko ndani ya dini husika huona kipande kingine kuwa ni cha cha waongo na matapeli.Hadithi huendelea.

    Ndiyo maana wajenzi wa demokrasia wakaona dawa ya kukomesha huo upuuzi, kila mtu awe huru kuamini dini yoyote iwe ya uongo au ya kweli,iwe ya matapeli au malaika, ana hiari ya kuifuata ili mradi moyo wake umependa na hajalazimishwa na mtu kufuata huo ukweli au uwongo ulioko kwenye hiyo dini ambayo anaifuata.

    Na serikali na Mabunge yapendayo demokrasia yakaweka katiba zake kuwa hayana dini katika katiba zake ili kujitoa katika upuuzi wa vita za kidini za kijinga za kusimamia nani mwongo au mkweli kidini na kukataa katakata vitu au agenda za kidini kuingizwa katika bunge au serikali.

    Na ndiyo maana juhudi zote za Serikali za kujaribu kuingiza kitu chochote cha kidini kiwe suala la Bunge au serikali kiwe suala la Kadhi au chochote hakikubaliki kidemokrasia. Serikali inabidi ibaki kama serikali na kuabudu kuachiwe watu binafsi wenyewe waamue kama wataamua kuabudu Shetani,Mwanga,au Wakiamua wamwabudu Issa Michuzi Hiyo ni juu yao.Mambo ya imani au kuabudu yawe makubwa au madogo si suala la Serikali wala Bunge

    Dini za ukweli na uwongo ziko duniani kote na zina wafuasi mamilioni na zinatambuliwa na kukubalika hata na Wafalme na Maraisi na Wanasikia raha kuzifuata.Wanazifuata kwa hiari yao na hutoa mabilioni ya mapesa kama sadaka bila kujisikia vibaya hata kama viongozi wanazichukua na kuzila hapohapo hawaziachi hizo dini.

    Kwa ufupi dini ya kweli kwa wataalamu wa demokrasia ni ile ambayo mtu binafsi anaiona yamfaa.Kwa hiyo Mtikila ni mfuasi wa dini ya kweli machoni pake.

    Cha msingi kidemokrasia ni kila mtu kufuata dini ile mtu anapenda na kuabudu atakacho akionacho sawa machoni pake kuwa ndicho chamfaa bila kuingiliwa,kuelekezwa na kulazimishwa na serikali, bunge,Raisi,Waziri,au Ofisa yoyote wa serikali namna ya jinsi gani aabudu,mambo yake ya kidini aendesheje,Migogoro yake ya kidini aitatuaje,n.k

    Sheria ya kadhi ina lengo la kulifanya Bunge litoe maelekezo ya namna ya Waislamu wanavyotakiwa watatue migogoro yao kupitia kadhi.Hiyo si kazi ya Bunge wala Serikali Tafadhali.Wataalamu wa Demokrasia ndani na nje ya nchi tumeshaliona hilo na tunafuatilia kwa karibu sana juhudi za chini chini zilizojificha sana za uvunjaji Demokrasia kupitia Bunge na Serikali ambapo serikali na Bunge zinajiandaa kutoa tamko la kidini la namna waislamu wanavyotakiwa kutatua migogoro yao kupitia kadhi kwa kupitia mswada unaotakiwa kuandaliwa na kupelekwa Bungeni ambapo maafisa wa serikali sasa hivi wanakula pesa kibao za posho za hela za walipa kodi kuhangaika suala hilo la kidini.

    Kesi ya kuchezea hizo pesa za walipa kodi kwa ajili ya suala hilo la kidini na yenyewe iko njiani inaandaliwa kwa taarifa zisizo rasmi Zilizopo.

    ReplyDelete
  33. Mch. Chris naona umeamua kujitosa mwenyewe sasa, haya tunasubiri hiyo kesi ya kuwatetea waislam uliotaka kuwanyang'nya msikiti pale mtaa wa Bukoba.

    ReplyDelete
  34. Hongera Mtikila kwa kuwa na kuanzisha kanisa lako mwenyewe bahati mbaya sijui hilo kanisa liko wapi siku moja ungeniona nakuja na ningetoa na sadaka na kukupongeza.

    Watanzania lazima tujenge utamaduni wa kuwapongeza watanzania wenzetu wakiamzisha vitu vyao iwe ni Biashara,Kiwanda,Duka,Kanisa, Msikiti,dini au dhehebu au hata wakitengeneza baskeli ya mti n.k.Siyo tu tukae tunashangilie vya Wazungu, waarabu au wahindi tu kama mabwege.Tufikie mahali tutukuze vitu vya watu wetu pia wanavyoanzisha hata kama ni shoka lilotengenezwa kwa jiwe.

    ReplyDelete
  35. Nadhani iko haja ya kuwatimua baadhi ya wanasheria wa Serikali.Hawamsaidii Raisi Kikwete kabisa.

    Kwa kawaida Hoja yoyote kabla ya kuipeleka Bungeni au kuitengenezea Mswada inabidi utumie kanuni ya Kisheria inayoitwa "KUNUSA" unainusa hiyo hoja kwanza ukiona ina harufu ya udini unaitupilia mbali.Hoja ya Kadhi ukiinusa ina harufu ya Dini.Huwezi peleka vitu vyenye harufu ya dini bungeni.

    Mwanasheria Mkuu na Waziri wa Sheria na Katiba Mama Nagu siwaelewi hivi huko chini mna watendaji wazuri au mna wahuni waliojipanga kumwangusha Raisi Kikwete aonekane kituko huko mbeleni?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...