gonjwa hatari la ukimwi ni moja ya mambo mawili makubwa aliyozungumzia jk, ambapo alitangaza kwamba kampeni maalumu ya kutaka watu wapimwe ngoma kwa hiari ifikapo katikati ya mwezi julai mwaka huu ambapo alimwomba kila mmbongo akapime ili ajijue. akauhakikishia umma kwamba serikali imejiandaa kusaidia waathirika kwa madawa ya kuongeza muda wa uhai na pia sheria inapikwa ya kudhibiti wale wanaoeneza ngoma kwa makusudi baada ya kujua wamekanyaga miwaya. alivitaka vyombo vya habari na wananchi kwa ujumla kuhamasishana juu ya kupimwa ngoma kwa hiari ili kufanikisha vita dhidi ya gonjwa hilo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Wazo la Kikwete la kutaka kila mmbongo apime ngoma ni wazo zuri sana kwa hiyo basi aaanze yeye kupima hazarani pamoja na baraza lake la mawaziri ili wawe mfano wa kuigwa. Pia anapoenda ulaya kufanya cheki apu awe anatuhabarisha afya yake inaendeleaje kwa maana anaenda kutibiwa kwa feza yetu lakini yeye na wenzio wake wanakaa kimya tu

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 06, 2007

    Michuzi,
    Kwanza kabisa nasikia waandishi wa habari wa bongo mnampigia magoti huyo jamaa---maswali mnayo uliza ni yakimbea tu.
    Pili hivyo fifaa vya kupimia ukimwi bongo hadi sasa vina utata kwani kila siku tunasoma kwenye magazeti--Je mmemuliza kuwa hivi vya kupimia vina utata au mmekubali tu nakusema ndio mzee mkaondoka? Je mmemuuliza wale walioko remote area wanamkakati gani wakuwafikia na kuhakikisha wanapima hiyo kitu au watanzania ndio hao wanaoishi hapo dar tu? Tatu, je mmemuuliza kama yeye kisha pima na ni lini alipima mara ya mwisho? na mawaziri wake na makatibu wakuu wamepima, na stats zinasema vipi(wangapi wano na wangapi hawana--au mmekubali tu, ndio mzee mkaondoka---huo muda wa ndio mzee umekwisha.
    Nne, Hayo mambo yakutwa chunguza viongozi waliopita--sio kwamba anajisafishia tu njia yake? Na je kama tusipochunguza hayo tulioyasikia tujajuwa vipi kama ni ya kweli au ya uongo--je mmemuuliza njia ambazo yeye ameweka ilikuchunza. Na je huyo Mkapa anae mtetea, hiyo pesa yote ameilipa vipi(katoa wapi?)
    Next time mkikutana na huyo kiwete--mmwambie pesa yetu itarudi kama iatarudi leo au kesho lakini itarudi.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 06, 2007

    The problem we face can not be solved by the same mind that created them.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 07, 2007

    Obama na mke wake walipima mbele ya umati ya wakenya. Na yeye Kikwete awe mfano na apime mbele ya umati ya wabongo

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 07, 2007

    Huyo jamaa anayesema mmemuuliza JK maswali,huwezi kufanya hayo mambo Africa otherwise hukanyagi tena kwenye fuction Ikulu yaani inabidi kila kitu ndo mzee au unauliza kitu ambacho unajua kabisa mkuu atafurahia.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 07, 2007

    wewe anona wa June 6, 2007 11:01:00 PM EAT unayetaka Rais uchimbwe kwa undani zaidi hivi hujiulizi ni kwa nini WAHARIRI ndio wamealikwa hapo?

    Ni kwamba wameitwa watu wazima, na watu waliokaa kwenye fani muda mrefu ndio waongee na Rais. Hao ni watu ambao tayari wameshakuwa conditioned by the system, so they are not going to rock the boat.

    Unadhani kwa nini watu kama wewe ambao mko radical hawajaitwa hapo?

    Vikao kama hivyo ni:
    "Ndio Mzee",
    "Mzee hotuba yako ilikuwa nzuri sana",
    "Tehe tehe, tihi tihi tihihihii"

    We angalia topic zenyewe, eti UKIMWI na UTORO MASHULENI, sio topic radical kabisa. Ni topic za kawaida tu za kijamii. Watu wanajua UKIMWI upo lakini hawajali kwa hiyo Rais basically anapiga soga tu na wahariri kwa kuongelea UKIMWI.

    "Ndio Mzee"
    "Yaani kwa kweli UKIMWI ni tatizo kubwa sana, na umefanya jambo jema kulizungumzia leo hii"
    "Tehe tehe, tihi tihi tihihihi"
    "Mzee hii suti yako safi sana"

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 07, 2007

    Nimsikitishwa na anony wa hapo juu anayesema kwamba kila swali wanalouliza lazima liwe NDIYO MZEE,kama ni hivyo mnaenda kufanya nini?hakuna haja ya kwenda IKULU kama ndiyo hivyo.Sasa nimemuelewa Mkapa kwanini alikuwa anawakandia waandishi wa habari wa Tanzania,kwa sababu mnashindwa kuliza maswali yasiyonamaana.Naamini kweli kwamba anayoyasema anony hapo juu ni yakweli.Kwa hiyo WAHARIRI wanafurahia kumshika Rais mkono baasi!WATANZANIA TUMEKWISHA.Maana ukiona makala wanazoandika jinsi zinavyoosha UOZO WA SERIKALI lakini mkimuona mnashindwa kuuliza maswali ya maana BASI HUO NI UNAFIKI MKUBWA,unless mtuambie yale mnayoandika kwenye magazeti yenu hamna uhakika nayo ni uzushi tuu.NAOMBA KUWASILISHA

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 07, 2007

    Hapo ishu ya wauza unga na wala rushwa imeishasahaulika sasa hivi wanajifanya kuzungumzia ukimwi serikali yetu ya bongo kwa kusahaulisha mambo anywayz may ne siku moja atatokea mtu atafunua kila jambo lilifonywa na serikali zilizopita

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 07, 2007

    JK: Why I won`t do business from Ikulu

    THISDAY REPORTER
    Dar es Salaam

    PRESIDENT Jakaya Mrisho Kikwete yesterday made a categorical declaration that he is not interested in pursuing personal business dealings while occupying the highest public office in the land, in contrast to his predecessor Benjamin William Mkapa.

    Answering a series of questions from local media editors after addressing the nation from State House in Dar es Salaam, the president said he has no plans to start his own private company with the first lady at Ikulu, like Mr Mkapa and his wife Anna did.

    Instead, Mr Kikwete said after retirement he would be content with being just a simple farmer.

    Asked about his predecessor’s reported controversial ’entrepreneurship’ pursuits while at State House, the president said his administration was prepared to let go the matter of Mr and Mrs Mkapa starting and operating a private business company, ANBEM Limited, from State House.

    However, President Kikwete maintained that the government of the day would not hesitate to take action against any proven allegations of serious wrongdoing in the matter.

    Delving further into the subject, Mr Kikwete said he personally believed it was not prudent for a middle-aged person to choose to make a debut into the world of private sector enterprise.

    ’’There is a British friend of mine who once told me that you can’t start engaging in business after reaching the age of 40,’’ he said in response to a question from one local Kiswahili tabloid journalist.

    Mr Mkapa was pushing 61 years old when he registered ANBEM Limited with Mrs Mkapa in 1999, with the official registration documents describing the then State House couple as ’entrepreneurs’ and sole directors of the limited liability company.

    Referring to a series of exclusive reports published by THISDAY in recent weeks on ANBEM Ltd and related business dealings, the president asserted that there was no need to pursue further investigations, noting that the hefty loans the company reportedly received from two local banks were repaid in good time.

    He also tried to discourage such investigations into the personal affairs of retired presidents such as Mkapa and Ali Hassan Mwinyi before him.

    ’’Sometimes that is why (political) leaders are tempted to change national constitutions to prolong their stay in power, for fear of being so investigated once they retire from office,’’ he remarked.

    The ANBEM Limited reports published by THISDAY have drawn very mixed feelings and ignited much heated debate amongst political observers, commentators and even actors, over the ethical considerations of Mr and Mrs Mkapa’s actions while still at State House.

    While some have argued that the couple did not break any law in registering their own private company while at Ikulu, others contend that the move - being mainly geared at ensuring personal gain - could well be interpreted as an abuse of office.

    For example, it has been widely asserted that the reality of Mr Mkapa, as sitting president, having personal business interests or participating in personal business activities outside his official portfolio is likely to have in some part interfered with the exercise of objective and independent judgement, on behalf of Tanzanians as a whole, while on the job.

    One seasoned lawyer and politician has gone so far as to point out various issues of serious conflict of interest and undue influence to consider in trying to balance such presidential and personal business affairs in a manner not likely to raise public questions and generate controversy.

    ’’Tanzanian laws may be silent on the issue of the president doing business while in office�but is there any bank manager in the country who will say no to the president when he applies for a loan?’’ he queried.

    ANBEM Ltd was granted hefty loans of $500,000 (approx. 620m/-) and 250m/- from the National Bank of Commerce Limited and CRDB Bank in 2002.

    Although it was eventually very quickly repaid, the NBC Ltd loan to ANBEM Limited was granted at a time of heated national debate over the privatization process surrounding the once state-owned bank, which the government formally sold off to South Africa’s ABSA Group for a reported total price of just 15bn/- for 70 per cent majority shares in April 2000.

    This was despite much opposition from a good number of legislators representing both the ruling CCM and opposition parties, all of whom were quite amazed by the cheap price quoted in the divestiture deal.

    Privatization of the giant bank was also fiercely opposed by the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, until his death in 1999. Mr Mkapa’s two tenures as president covered the period 1995-2005.

    Outlining major priorities for his incoming government in a historic state-of-the-union speech on assuming the presidency on December 30, 2005, President Kikwete underlined the increasing need to root out corruption and unethical conduct by public officials before it all got out of hand.

    ’’We must tighten mechanisms in place to ensure public officials do not use their offices for personal gain and self-enrichment,’’ he said, adding for good measure: ’’I am not against people getting rich. Indeed, I want everyone to have a better life. What I am against, is people using public offices for self-enrichment.’’

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 07, 2007

    Naungana kwa hoja na mchangiaji Maricha hapo juu, kuwa ni vyema viongozi wetu wakawa watu wa mwanzo kabisa kupima na kutuambia hadharani afya zao, ili nasi tuhamasike kupima kwa hiari. Mbona katika michango ya hiari kama vile ujenzi wa shule, makanisa, misikiti nk, viongozi wanakuwa mbele sana kuchangia, nini kinawafanya wawe wanasita kupima na kutuambia afya zao? Sasa tutahamasika vipi? Wao wanapima afya zao nje ya nchi kisirisiri na wanarudi kimya kimya na wanatulazimisha sisi kupima hapa hapa, kwa nini? Nitafurahi sana siku moja nikisikia mtu Kama Lowassa ama Kikwete ama waziri au mbunge yoyote kaenda Angaza kupima na kutangaza hadharani matokeo ya vipimo, nadhani mpaka hapo Watanzania tutahamasika. Nadhani ni mwaka jana tu ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar Bw Kandoro alipima hadharani, ila hata hivyo hatukuambiwa majibu yake, inabidi na mawaziri wamuige. Tumechoshwa na ripoti za vifo vya wakubwa, kuwa wanakufa kwa shinikizo la damu ama kiharusi wakati wengine tulikuwa tunaishi nao na tuna uhakika walikuwa ni waathirika. Ina maana hapa Tanzania hakuna kiongozi hata mmoja aliyewahi kufa kwa Ukimwi tangu ugonjwa uingie hapa nchini mwaka 1981? Kweli? Naomba viongozi wetu wabadilike,wawe wa mwanzo kupima na kutangaza majibu ya vipimo hadharani vinginevyo Ukimwi utaendelea kutumaliza kwa kuoneana aibu!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 07, 2007

    Baba wa taifa tungeomba kuhamasisha na kuongeza changamoto tungeomba wewee na bunge na baraza la mawaziri mnekua wakwanza kupima.

    ReplyDelete
  12. Michuzi, picha hiyo nzuri sana!

    ReplyDelete
  13. Maoni yangu sio kujibu maswali tu lkn hatua serious sichukuliwe kuhusu hizo points.
    Kupimwa si hoja lkn kuna mengi ya kuangaliwa:
    -Kwanza hilo jina eti "WAATHIRIKA" libadilishwe maana kuaathirika ni kitu cha aibu. Liwekwe jina la kawaida mfano "watu wanaoishi na virus"
    -Serikali ichukue mzigo wa kuwatibu wagonjwa magonjwa yanayo sababishwa na ukimwi bure au kwa bei ndogo sana bila ubaguzi.
    -Wazazi/Mashule/NGOs waelimishe na wafundishe watoto/vijana matumizi ya kondom wakiwa wadogo, kusudi mara yao ya kwanza ya kufanya mapenzi iwe kwa kutumia kondomu kusudi wa zoe maana kutumia kondomu baada ya kuanza bila mara nyingi watu wanaona ngumu. Kanisa lisizuie hilo eti ni kuwafundisha watoto vibaya NO! tunaishi kwenye era hii na hilo gonjwa limechagua pabaya, ukiwa kijana uko curious kugundua what is behind sex? na kwa vile vijana ni taifa la kesho then we have too tell the youth the truth to help protect them!
    -Watu wanaofanya kazi kwenye conselling should be serious hata kwenye mahospital afya ya mtu ni siri yake lkn bahati mbaya kuna umbea/speculation sana na hii inasababisha wengi wajifiche na kufa kimya kimya, too bad wakati sasa dawa zipo za kuongeza maisha.
    -Jamii ichukulie huo ugonjwa kama ugonjwa wowote ule na una weza mpata yeyote sio lazima mtu awe m*l*y*
    -Kupimwa ni uhuru wa mtu sheria haiwezi pitishwa eti lazima wabongo wote wapimwe!(human rights) On the other hand kupima ni vizuri maana unajua healthy status yako.
    -UKIMWI unatugusa wote direct au indirect therefore ni vita vya pamoja ndoo tuta shinda!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...