ze comedy wakingoja uamuzi wa wakubwa baada ya onesho lao lililotaka kufanyika bustani ya mnazi mmoja gaden kusherehekea uzinduzi wa mfuko wa uadilifu, uwajibikaji na uwazi kuingia kashkash kutokan na msongamano wa watu mbele ya makamu wa rais ali mohamed shein aliyekuwa mgeni rasmi. msongamano huo sio tu ulitishia usalama wa viongozi bali pia hata watazamaji walikuwa na wakati mgumu. sherehe hizi ziliandaliwa na sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma na lengo la mfuko huo ni kusaidia taasisi za umma, sekta binafsi, vyama visivyo vya kiserikali na vyama vya kitaaluma nchini viweze kuwa na uwezo wa kusimamia uadilifu, uwajibikaji na uwazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hahahha Ze Komedi mambo yenu makubwa na yanagusa maish aya kila siku ya Mzt wa kwaida.

    Seki na washirki wa ze Komedi kazi nzuri, nawatakia kila la kheri ktk shughuli zenu.

    ReplyDelete
  2. Usalama wa viongozi kitu gani? Tatizo la viongozi wa kibongo wanadhani hawatakufa. Watu wamekuja kuwaona wana Ze Comedy waki-perform live, viongozi eti wanahofia usalama wao!!! Kweli bongo kuna Miungu watu. Mtu mmoja anasababisha kundi kukosa burudani. Bora niendelee kubeba maboksi hapa mamtoni, bongo ubinafsi wa viongozi ulinishinda.

    Nawakilisha Michuzi.

    ReplyDelete
  3. Mithupu eeeeh!!!
    Tafadhali kaka tupe majina ya hawa jamaa.Mimi namkumbuka joti na masanja mkandamizaji.Wengine bahati mbaya nimewasahau.Hawa jamaa ni wasanii hasa.
    Majita

    ReplyDelete
  4. Huyu joti kweli kiboko maana watoto wote sasa hivi wanatembea kama yeye, ukiwakuta wanacheza basi wanashindana kumuiga mwendo wake

    ReplyDelete
  5. mimi nawafagilia sana ze comed,aise iyo kumbukumbu ya mwaka;lakin bwana mkandamizaji punguza msitu kichwan uwe kama bwana hamijeiiiiiiiiiiiiiii alonga

    ReplyDelete
  6. kha eti mnakaa chini kabisa mnasupport ze comedy ni noma.. kweli hamna la kufanya.. ujinga mtupu.. hao jamaa wanaifunza nini jamii? yaani ukiishi sana bongo hata mawzo yanakuwa mafupi hebu fikirieni vitu vya maaana, kigamboni liwekwe daraja ama nini kitendeke.. sio mnakaa mnaongelea ze comedy..!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...