kutokana na ukumbi wa kawaida wa maonesho kuwa katika matengenezo, maonesho yote ya jukwaani pamoja na ufunguzi wa tamasha la sanaa katika chuo cha sanaa bagamoyo yatafanyika kwenye jukwaa la mwembeni kesho jumanne.


ratiba inaonesha kwamba makamu wa rais mh. dk. mohamed ali shein atafungua tamasha hilo saa tisa mchana ambapo atashuhudia ngoma mbalimbali za utamaduni na kukagua sanaa za mikono na pia ujenzi wa ukumbi wa kisasa.


usiku hiyo kesho kutakuwa na muziki na igizo toka kwa wanafunzi wa chuo, kabla ya kundi la sarakasi toka italy liitwalo antonella migliore kufanya vitu vyake, likifuatiwa na ngoma ya pwani toka kwa ruvu jkt na baadaye kundi la sanaa toka geita linalocheza na fisi.


jumatano mchana kutakuwa na kongamano kwa wasanii wote washiriki lililoandaliwa na wizara ya mipango na uwezeshaji. usiku ni libeneke kama kawa ambapo vikundi vya lumumba theatre, tht, mlingotini sanaa, chuo cha sanaa na selui art vitafanya mambozzz.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...