WANAFUNZI WA MWAKA WA KWANZA CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA ELIMU CHANG'OMBE (DUSE) WAMEGOMEA MASOMO LEO WAKIWA NA MADAI KADHAA MOJAWAPO IN ANAYOSEMEKANA KUSABABISHA MGOMO HUO NI KUSTUKIZWA MITIHANI KWA TAARIFA YA WIKI MOJA, INGINE NI KUAMBIWA KWAMBA WATAFANYA MITHANI MITATU KWA SIKU NA PIA WANAFUNZI KUSACHIWA VITABU VINAVYOSADIKIWA KUIBWA MAKTABA KWA NAMNA YA UNYANYASAJI WA KIJINSIA AMBAPO ASKARI WA KIUME HUSACHI WANAFUNZI WA KIKE
WAKATI HUO HUO LIBENEKE LA MGOMO CHUO KIKUU CHA ARDHI LINAENDELEA JAPO CHUO KIMEPIGWA MKWARA KWAMBA WANAFUNZI WATAKUWA WAMEJIFUKUZISHA MASOMO ENDAPO WATAKAIDI KURUDI MADARASANI AMBAKO WAMESUSA KWA SIKU TATU MFULULIZO KINYUME NA TARATIBU ZA CHUO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. bongo TAMBARARE..

    ReplyDelete
  2. Yaani kwa kweli Elimu yetu ya kitanzania inaudhi maana inalirudisha taifa nyuma.
    Wenzetu nchi zilizoendelea wanajitahidi wanafunzi waelewe na wafanye vizuri darasani sio kukomoana.Kwanza walimu wanatoa ratiba ya semester nzima..NO SUPRISES. YAANI SISI MAMBO YETU NI KINYUME! mfano mzuri ni kwamba wanafunzi wanaopata division 1V ndo wanaopelekwa ualimu, NA WALILIMU NDO WANAOLIPWA KIMA CHA CHINI.NCHI ZILIZOENDELEA NI KIMYUME TEACHERS ARE BEST PAID, NA WANACHUKUA WALE WAIOFALU! TANZANIA TUTAFIKA HUKO LINI JAMANI??????????????
    Mdau
    Alumni York Univerity Toronto.
    BA Hons.Social Justice
    www.yorku.ca

    ReplyDelete
  3. WAACHE UJINGA WAO.ETI KUSTUKIZWA
    EXAMS.KAMA WAMESOMA HAKUNA HAJA YA
    KUOGOPA EXAMS HATA SIKU MOJA.HAPA
    NIPO BOGAZIC UNIVERSITY NAWEZA
    KUFANYA EXAMS 4 KWA SIKU MOJA NA
    KOZI NI BIOMEDICAL.HAO NYAMBAF
    KABSA WATAKUWA WAMEIBA VITABU.
    KAZI WIZI TU NDIO HAO KESHO WANA
    KUWA CORRUPT MINISTER NA WANASIGN
    BOGUS CONTRACTS.WAONE MACHO YAO KAA
    SUNGURA MWITU.NYOOOO!

    ReplyDelete
  4. Upumbavu tu huu. Mi mngenipa hicho chuo ningekuwa natoa adhabu instantly. Unagoma siku moja unafukuzwa shule kesho yake. Hakuna huruma wala kuchekeana. Hakuna kusubiri wagome wote. Hata nikipata taarifa za maandalizi ya mgomo tu, wahusika wanaoandaa wote nawafukuza kabla mgomo wao haujaanza, nione kama mtaenda kugomea huko kwa wazazi wenu? Hata wakigoma wote, nafukuza wote a kuanza upya (waliogoma sipokei hata wakitembea kwa magoti kuja kuomba). Msimamo kama huu unafaa sana katika kuweka nidhamu. Seminari za kikatoliki zimeutumia kwa miaka mingi na matokeo yake tunayaona, wanafunzi wanakuwa na nidhamu, utulivu wa akili na maendeleo mazuri sana ndani na nje ya darasa. Kama wadau mlikuwa hamjui, siri ya mafanikio makubwa ya kitaaluma katika seminari za kikatoliki ni moja tu: NIDHAMU. Sijali kama ni ya woga, lakini NIDHAMU inasaidia sana. Mengine yote baadae, lakini NIDHAMU kwanza. Nakaribisha maswali na mjadala. Wenye hoja za kupinga hili walete ushahidi. Nina uhakika wapo wengi wenye kukubaliana nami kwa hoja hii kwa kutumia uzoefu wao binafsi. Karibuni.

    B.J.Y Kithuku

    ReplyDelete
  5. yaani bongo tambarare mitihani mitatu na surprised test mnagoma..????
    kweli mnadeka....hamtaweza kufanya credit 18-21 na kubeba box ili umlipe mama mwenye nyumba.

    ReplyDelete
  6. HAHAAA,
    MIGOMO MINGI VYUO VIKUU BONGO HUTOKEA WAKATI KARIBU NA MITIHANI. WAJINGA WACHACHE AMBAO WAO WALIKUA WANATANUA NA BUMA LA TIRDO HUANZISHA MIGOMO NA KUWAINFLUENCE WALE AMBAO NI WAVIVU KUFIKIRI.

    ANGALIA SASA HIZO SABABU, KWA KWELI NI ZA KUOKOTEZA TU!!!!

    LAZIMA WAJUE WAO NI WANAFUNZI TUU HAWAWEZI KUFANANA NA WATU AMBAO HAWAKO KATIKA MIFUMO YA KIELIMU NA WAACHE KUSHINDANA NAO KUZURURA MITAANI.

    ReplyDelete
  7. Wakuu wa vyuo, tafadhalini. Kwa nini hamuwafukuzi hao wagomaji? Mnalea uozo namna hiyo. University ni mahali pa wanaotaka kusoma. Mtu asiyetaka kusoma anafanya nini huko? Fukuzeni hiyo midebwedo! Kama ni suala la sheria (by-laws au kitu kama hicho), badilisheni tu, mamlaka hayo mnayo. Watu wakileta upuuzi, timua. Ukali (strictness) ni lazima katika kuhakikisha nidhamu ya kitaaluma inakuwepo.

    Hivi wakuu wetu wa vyuo, mnapowabembeleza watu wenye tabia za kugomea tu kila kitu, mnalea wasomi wa aina gani? Ni mfumo gani wa ajira utakaopokea watu ambao wamejifunza katika CHUO KIKUU kwamba migomo inakubalika kama suluhisho la chochote kile? Hawa si wataanza kugomea maagizo ya kazi? Imagine hapo wanagomea mtihani waliyopewa taarifa ya wiki moja nzima, wanadai ni muda mfupi! Kwenye kazi challenge zinatujia kila siku bila taarifa, na tunapaswa tuzikabili! Madaktari na wauguzi hawapewi taarifa kwamba kipindupindu, ebola, ajali nk zitakuja lini. Askari hawataarifiwi lini uhalifu utatokea. Waandishi wa habari hawajulishwi "mapema" lini tukio la ghafla litatokea wakaripoti, wao wakisikia tu muda huohuo wanawahi kwenye tukio kuchukua habari. Sasa hawa wanafunzi walitaka wajulishwe kuhusu mitihani kabla ya muda gani? Ina maana siku zote walikuwa wanafanya nini huko vyuoni?

    Mie naona wakuu wa vyuo mnawachekea hao watoto, sasa wamewafanya watani zenu kama babu na wajukuu!

    Ndugu Michuzi, nipigie debe kwa Mzee wetu JK anipe chuo kimoja, nakuahidi miaka mitatu tu, sitaki zaidi, muone kazi.

    B.J.Y Kithuku

    ReplyDelete
  8. Ndugu Michuzi naomba unifikishie comments zangu (hii hapo juu na ile inayohusu Chuo cha Ardhi) kwa wakuu wa Vyuo husika. Waeleze kuna watu tuna uchungu sana na hali hii.

    B.J.Y Kithuku

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...